Mitume na manabii ni wagonjwa wa akili waliochangamka?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Sayansi inathibitisha kwamba kiasili kila binadamu ni kichaa (uchizi wa akili), kinachotofautisha ni viwango vya asilimia, utashi na uthubutu

Asilimia zikiwa kubwa utashi huwa mdogo sana na uthubutu huwa wa kiwango cha juu mno, ndio maana kichaa anaweza kufanya chochote ambacho wewe huwezi kukifanya.

Kwahiyo kwenye mudulla uwiano wa utashi na uthubutu kwenye kila jambo na kila kitu ni muhimu sana. Kimoja kikimzidi mwenzake kwa asilimia kubwa tayari ni tatizo.

Binadamu pia anaota ndoto. Hili ni tendo la kiasili lisilodhibitiwa na ufahamu (involuntary action) lakini ndoto hizo huwa na asili, huwa na chanzo! Ni ngumu kuota kitu kisicho na kaliba nawe kimatendo, mawazo na maneno kupitia milango sita nane ya fahamu.

Kwenye makundi ya ndoto kuna kitu kinaitwa ndoto za mchana ama ndoto za kufikirika! Watoto huota sana hizi ndoto na ndio asili ya vikaragosi kwenye luninga (cartoons), kadiri mtu anapoacha umri wa utoto na kuelekea ukubwani hata ndoto za kufikirika hubadilika.

Hapa kile kipengele cha unataka kuwa nani maishani, hiki nacho ni ndoto lakini leo si sehemu ya mjadala.

Sasa ugonjwa wa akili unahusikaje na ndoto? Tunarudi kwenye uwiano wa utashi na uthubutu. Kuna ugonjwa wa akili bila kutaka na kuna ugonjwa wa akili kwa kutaka na kwa asilimia. Si uchizi fresh la hasha, bali ni uchizi (kujitoa ufahamu kwa ajili ya manufaa fulani) kwa mukatadha huu kipato na umaarufu.

Manabii na Mitume wengi ni wagonjwa wa akili waliochangamka, ni machizi wenye kiwango kikubwa cha kujitambua. Ni washindwa wa ndoto za utotoni za kuwa fulani ukubwani na kuamua kujilipua kivingine!

Changamoto za maisha kwenye kipato, ajira, mahusiano, utajiri umaarufu, nk, na ukosefu wa utatuti umewapa mwanya washindwa wengine walioamua kuyatumia hayo matatizo na changamoto za wengine kutengeneza kipato.

Mwanzoni ni uhuni na uongo wa kawaida wenye kautapeli ndani yake, lakini kadiri siku zinavyoongezeka na wahitaji kuwa wengi, jamaa huona kumbe inawezekana hata kupitia uongo wa kufufua wafu, kuombea mtu apate mali, kuombea mtu apate mchumba, kuombea mtu apate mtoto nk.

Uongo ukirudiwa mara nyingi hadhira huuamini na kuufanya ndio ukweli. Hapa ndio kile kichaa kutokana na uwiano kwenye utashi na uthubutu huibuka na kuja na mauzauza ya ajabu ajabu; chupi za upako, mafuta ya upako, vitambaa vya upako nk.

Hawa watu kufikia hapa na sheria ikiwaangalia tu ndio uchizi wao huongezeka na kufanya mambo ya ajabu zaidi kama; kuwabambia wanawake hadharani ili wapate watoto/waume, kutoa shuhuda za kufika mbinguni, kumcharaza shetani bakora, kunywa jik ili kusafisha dhambi, kuvaa maputo na kupanda juu ya miti ili Kristo awanyakue nk.

Watu hawa wenye majina ya Manabii na Mitume ni vichaa waliochangamka kutokana na kuota ndoto za mchana na kutaka kuzigeuza kuwa halisi. Utashi wao wa kutenda unakuwa umezidiwa na uthubutu na serikali kukaa kimya bila kuwachukulia hatua.

Kuna mahali huko duniani waliachwa wakiaminika ni viongozi makini wa kiimani na kusababisha majanga makubwa ya vifo, ulemavu na uharibifu mkubwa wa mali.

Mmoja wiki hii katrend sana baada ya kusema naye kafika mbunguni na kuongea na watu wa huko! Hakuna aliyethubutu kumuuliza kama kafika mbingu gani? Ya ngapi!? Kaenda na mwili wake? Waliongea lugha gani? Au ile ya rakabasha....rakoshoko... kibudeniiiiicccc.

Huko angani ni vast emptiness. Mbingu ni dhana pana sana!
 
Manabii na Mitume ni hekima ya Mungu... Mungu ni Yule ule, jana, leo, kesho na hata milele...

Nitaharibu hekima ya watu wenye hekima na kuzi kataa akili za wenye akili.

Kwa maana huu ‘ujinga’ wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, na ’udhaifu’ wa Mungu una nguvu ipitayo nguvu ya wanadamu.
 
Kuna mpumbavu mmoja alimuombea mtoto baada ya kumaliza sala ambayo mtoto alikua akilalamika kuumizwa kichwa wakati anamuombea ( alikua ana mbinya kichwa na kumgongagonga ) akaomba aandike jina la mtoto kwenye horodha ya watu wanaokwenda kutoa ushuhuda akaulizwa inakuaje mtoto ambae hana akili ya kujielezea akatoe ushuhuda!!?

Akasema atamuelekeza vya kusema, aya akaambiwa muelekeze jamaa anamwambia mtoto akapande madhabauni akaseme yeye ni mchawi akaulizwa je mtoto hapo mbele akiulizwa uchawi kautoa wapi atasemaje hapo ndio utata ukaanza, akaambiwa hiyo ni ramli chonganishi, tutolee upumbavu wako hapa.

Lilikuja kutokea swala moja zito sana, hao manabii sijui makuhani huko kimara ni zaidi ya wachawi ibada zinaendeshwa katika mazingira ya kuchonganisha watu na kudhalilisha, hawana tofauti na waganga wa ramli chonganishi
JamiiForums2044379132.jpg
 
Ulichokisema ni kweli japo hujakiwasilisha kitaalam. Tatizo ninaloliona ni wewe kichaa unayeamini ulozi, uchawi na astral projection ( hallucinations) unapojaribu kuwanyooshea vidole vichaa wenzio. Kiufupi watu wengi wanaoamini haya mambo ya kufikirika ni wagonjwa wa akili( delusional schizophrenic)
 
Huyu aliyesema alienda mbinguni kuna mwenzake wa dhehebu moja anapinga kuhusu habari za mbinguni akidai hawezi kuhubiri habari za mbinguni kwa sababu hajawahi kufika mbinguni. Sasa hawa wote wanachanganya waumini wao kuhusu dhana ya mbinguni. Waumini watachanganyikiwa wamuamini nani kati ya hawa wahubiri maarufu japo mmoja ameibuka siku za karibuni na mwingine ni wa siku nyingi. Ukija kwa hawa mitume na manabii ndio utopolo mtupu ni rahisi kwa mtu mwenye akili timamu kubainisha abrakadabra zao. Chupi za upako na keki za upako ni kielelezo tosha cha abrakadabra za mitume na manabii hawa. Shuhuda za ajabuajabu zenye utata ni abrakadabra zingine kulaghai watu
 
Manabii na Mitume ni hekima ya Mungu... Mungu ni Yule ule, jana, leo, kesho na hata milele...

Nitaharibu hekima ya watu wenye hekima na kuzi kataa akili za wenye akili.

Kwa maana huu ‘ujinga’ wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, na ’udhaifu’ wa Mungu una nguvu ipitayo nguvu ya wanadamu.
Point yako ni Nini anko? Wanachofanya Hawa manabii ni sahihi?
 
Ulichokisema ni kweli japo hujakiwasilisha kitaalam. Tatizo ninaloliona ni wewe kichaa unayeamini ulozi, uchawi na astral projection ( hallucinations) unapojaribu kuwanyooshea vidole vichaa wenzio. Kiufupi watu wengi wanaoamini haya mambo ya kufikirika ni wagonjwa wa akili( delusional schizophrenic)
Ok basi sawa...!
 
Back
Top Bottom