Serikali kutochapisha takwimu za kiuchumi: Ifahamu IMF

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Kuna mjadala kwa sasa unaendelea kuhusu serikali kugoma kuruhusu kuchapisha taarifa za majadiliano ya kiuchumi yaliofanyika, baina ya serikali na wadau wa IMF takwimu zinaozoonyesha uchumi wa Tanzania kukua kwa 4% badala ya 7% ilotarajiwa.
sababu zimeelezwa katika tafiti

Mjadala huu ningependa uwe wenye tija ,kwa maana ya kulisaidia taifa,dhidi ya kitu kinachoitwa vita vya kiuchumi,

Sina uzoefu sana na masuala ya kiuchumi,ila naamini wachumi wabobezi wazalendo wa kitanzania kwani nia ya dhati kabisa watatueleza kama ni kweli,
kwa nini serikali imegoma kuruhusu kutolewa tafiti hizo,kuna faida zipi na hasara ipi kwa kuzitoa au kutozitoa.

Pia ningependa kufahamu historia ya IMF ,

1,kuanzishwa kwake

2,kusudio la kuanzishwa kwake

3,Malengo ya kuanzishwa kwake

4,uaminifu wa taarifa zake kwa wanachama,especially nchi zinazoinukia kiuchumi

5,kilicho nyuma ya pazia kuhusu shirika hili ambacho hatukielewi,ispokua wachumi wabobezi mnakielewa.

6,chombo hiki cha kimataifa hakiwezi tumika kama siraha kwa baadhi ya mataifa yasiokubaliana na baadhi ya sera?

7,kama nchi, inajinasuaje na hali hii?.maswali ni mengi lakini naamini wachumi wabobezi wazalendo wasio na mlengo wowote wanaweza kutusaidia kujifunza kupitia uzi huu.
 
Ukipingana na WB na IMF jiandae kula nyasi ,mwalimu Nyerere yalimkuta haya, maisha hayakuwa rahisi,kupata vitu kwa foreni mpaka aliposalimu amri,haya mabeberu sio ya mchezomchezo
Unataka kunieleza ya kwamba serikali inashinikizwa kufanya vitu visivyo halali kwa lengo la manufaa ya hawa jamaa kwanza, na si 50/50
 
"Miaka ya sasa unakwepa utandawazi unajifungua ndani utakula kunguni"


Walipochapisha kwamba uchumi unakua kwa 7% kwanini hamkulalamika bali mkashangilia?

Mmefanikiwa kuwalisha Watanzania matango pori sasa na wazungu mnataka kuwalisha matango pori?

Mnasema hamtaki msaada lakini mkiadiwa tu kidogo pesa mnatangazia umma kwamba tumepata mkopo....

Deni la taifa limeongezeka maladufu kuliko utawala wowote ndani ya miaka 4 lakini mnasema tunakusanya kodi ya kutosha iko wapi?..

Kidonda mnachokifunika kimeoza sasa"
 
Watangulizi wote wa mtukufu ukifuatilia kwa makini utangundua walikuwa na washauri wabobezi wakubwa wa Historia, huwezi ukajua umuhimu wa IMF kama ina ignore history.
 
Unataka kunieleza ya kwamba serikali inashinikizwa kufanya vitu visivyo halali kwa lengo la manufaa ya hawa jamaa kwanza, na si 50/50
Sasa kama mnajua hayo yote kwanini mmekubali kuwa mwanachama wa imf? Mlilazimishwa? Siyo kila uchafu ni wa kutetea. Usijifanye unajua kila kitu hapa jf.....siasa zako za kijing.a mwisho uwe chalinze.
 
Sasa kama mnajua hayo yote kwanini mmekubali kuwa mwanachama wa imf? Mlilazimishwa? Siyo kila uchafu ni wa kutetea. Usijifanye unajua kila kitu hapa jf.....siasa zako za kijing.a mwisho uwe chalinze.
Najua huwezi chambua huu uzi kama mchumi,umetawaliwa na unazi,linajidhihirisha kwa aina ya uchangiaji wako
 
Back
Top Bottom