KWEZISHO
JF-Expert Member
- Jan 29, 2016
- 7,519
- 6,511
Tulivyofundishwa shuleni IMF na WB ni mikono ya ubeberu na hutumia mikopo au misaada ili kututawala. Waswahili husema baniani mbaya kiatu chake dawa. Na kipindi tulifundishwa fedha sio msingi wa maendeleo. Nilikuwa najiuliza saaana hivi kwa nini hawa mabwana kama ni mabeberu yaliyojaaa uhafidhina, kwa nini bado tunawakimbilia na kuwakaribisha kwa mbleko na bashasha?
Tuliwahi kuandamana kumpongeza Nyerere kwa kukataa kurudi nyuma ili tusigeuke kuwa jiwe. Nyimbo na mashairi ya kizalendo yalitungwa, na chamoto tulikipata. Mwishowe mzee akasema nang'atuka. Hawa jamaa sio wepesi kama tunavyojifariji, tusije tukaanza kushikana uchawi!