Serikali kuondoa udhibiti wa sukari kutoka nje kisheria. Bashe adai anaenda kuwatikisa 'Big Boys'

Kwa umeme huu watashindana vipi bila kuwabeba labda waambiwe wafunge viwanda! Au serikali ipunguze makodi tuu!
Kama kwa umeme huu hawawezi kuzalisha kwa bei ya tija, wa nje waruhusiwe tu.

Yani ni bora wananchi wapoze maumivu ya kutokuwa na umeme kwa chai yenye sukari, kuliko kukosa umeme na kukosa sukari pia.
 
Mwezi wa 6 mbali Sana.
Aruhusu sukari ya Zambia, Malawi na Uganda haraka Sana.
Kama tatizo sheria Raisi atoe presidential decree kibabe kama katazo la Magufuli la mikutano basi aruhusu sukari ya nje.
Au waitishe kikao cha dharula cha bunge (hati ya dharula ya muswada wa mabadiliko ya sheria),
wabadili sheria husika.
 
Kwa umeme huu watashindana vipi bila kuwabeba labda waambiwe wafunge viwanda! Au serikali ipunguze makodi tuu!
Lawama zote kwa January Makamba kuchezea nishati ya umeme na majaribio yake ya ajabu pale TANESCO.
Hizi ni chain reaction za makosa yake.
 
Wananchi wapunguze matumizi ya sukari.
Maji na Umeme nazo tupunguze matumizi kisa nchi imeshindwa upatikanaji wake? Unakuaje ndugu yangu kwa kufikiri?
Kitu kipatikane kwanza suala la kuounguza ni option nyingine baada ya kuona umuhimu wa kukipunguza.
 
Safi Bashe ingawa amechelewa sana.

sukari,petrol,bandarini n,k kuna mapapa wanakula,washakusanya bilions of money kwa miaka na miaka.

bado hawana huruma hata kidogo wana roho mbaya,wapo radhi wananchi wataabike huku wao wakikusanya fedha kwa mataabiko ya umma wa wa Tanzania,hawatosheki!
 
Waziri yuko sahihi wamelondwa vya kutosha, wameshindwa kutumia fursa, acha washindane.
 
I
SUKARI inaweza ikatoka Brazil mbali Huko na still tukainunua kwa sh 2000 kilo MOJA.believe it or not.hakuna haja ya kuprotect majizi.
Magine watu wamepewa tenda kuagiza tani elfu 10..wanaagizi buku moja tu..majizi ya mwendo kasi.
 
Wahujum uchumi mmefikiwa,jiandae kulima mpunga maana biashara ya sukari mmeshindwa,Inatia uchungu sana kuona hii hali inajitokeza kila mara wahusika wakikingiwa vifua.Bora sukari iagizwe nje tu wananchi wapumzike kulanguliwa.
 
Kwa akili kama hiz, watanzania na Afrika Kwa ujumla tuna safari ndefu sana.

Utumie akili kupambana na watu wanaokudidimiza Kwa makusudi? Wewe utakua rais au mtumwa wao?

Hiyo akili wananchi watasubilia wakiumia Hadi Lin?

Hao wenyewe hawana akili unayoiwaza wewe?

Intelligence ya wafanyabiàshara ni kubwa. Hata huko mnakokwenda kununua sukari nje wanaweza Fanya mtanzania yoyete anujue Kwa bei juu Ili bei hapa nchin isishuke. Wanamuungano na sio mtengamano.

Vibari vya kuagiza sukari vinatoka Kwa masharti Gani, unayajua? Hivyo vibari havitoki kiholera, ni deal za watu. Usipoweka asilimia yao hupati kibali.

Unashangilia Kwa wenzako kutengeneza mianya ya kupiga pesa duuhh.

Hatari sana.
 

Kwa nini unakwama kuongelea vibali wakati vibali vyote vinaondolewa na biashara inakuwa huru kwa yeyote anayeweza aingize sukari?

Vibali viko hapo kwa sababu kuna zuio la kuingiza sukari. Zuio likiondoka, na vibali vinaondoka. Mbona huelewi?

Sasa kama intelligence ya wafanyabiashara ni kubwa ndiyo serikali itaweza kupambana nao kwa nguvu kwa kukimbizana nao kuwashika ulanguzi? Baada ya strategy hiyo kushindwa tangu enzi za Waziri Mkuu Sokoine?

Huoni kwamba point yako kwamba intelligence ya wafanyabiashara kuwa ni kubwa ndiyo inaongeza sababu za kupambana nao kimfumo kwa kubadilisha sheria na soko, na si kukimbizana nao kufunga walanguzi?

Huoni kwamba unajipinga mwenyewe?

Yani unasema wafanyabiashara ni wajanja sana, usikabikiane nao kwa kutumia akiki, tumia nguvu tu.

Wakati mfanyabiashara mjanja anaweza kukupiga pigo la Ju-Jitsu, akatumia nguvu za serikali kuidhibiti serikali yenyewe.
 
Naunga mkono hoja ,najua amemueleza mama akampa go ahead.

Mwisho Rais ajitokeze kukemea hii sio kukaa kimya huku Mawaziri wanajiuliza Kauli za kutamka
 
Sasa manake nini?
Kwani hiyo sukari inayotegemewa kuingizwa si inalimwa au inazalishwa viwandani?
Kwangu mimi ingekuwa vyema waziri wa Kilimo angejitanabahi Kwa Kuongeza uzalishaji wa miwa na utengenezaji wa sukari.
Hivi mahela ya serikali aliyotumia kuwaweka vijana wa mjini wa ccm makambini eti kuwafundisha Kilimo hela yote hiyo iliyotumika kufanya huo upumbavu ingeelekezwa yote Kwenye kuongeza uzalishaji wa sukari tungekuwa tumefanya la maana kama nchi yenyewe yakaona ni kheri yatengeneze kamfumo( Big nini sijui) wazile wana ccm wengi kidogokidogo.
Seriously kabisa waziri anakomalia kwenda kufuta Sheria inayowalinda wazalishaji miwa wa ndani ili kuruhusu sukari inayotengenezwa nje kuingizwa nchini.
Mabonde yote tuliyonayo waziri ameshindwa kueleza namna ya kuboresha Kilimo cha miwa .
 
Tatizo si uwezo wa nchi kuzalisha sukari, hilo lingekuwa tatizo, kuongeza uzalishaji wa sukari kama ulivyosema, kungeweza kutatua hilo tatizo.

Tatizo ni wafanyabiashara wa sukari ku manipulate supply ya sukari, kutengeneza uhaba makusudi ili bei ipande.

Na tatizo hili linatatuliwa na serikali kuruhusu sukari kutoka nje iingie Tanzania bila vikwazo.

Wafanyabiashara wa ndani wakileta janja zao ku manipulate supply, hata wewe uweze kwenda Malawi na Zambia kuleta sukari ya huko ya bei nafuu na kupata faida.

Usichoelewa ni kipi hapo?
 
Porojo nyingine lakini utekelezaji ni ZERO siku si nyingi Bashe atasema Nguruwe pori wameingia kwenye Mashamba ya Miwa.
 
Kwa hiyo nilivyokuelewa kwamba tatizo sio uzalishaji wa ndani wa sukari Bali tatizo ni wafanyabiashara ambo kuwadhibiti ndio kama alivyoelekeza waziri kuagiza sukari kutoka nje.
Ndio hivyo au?
 
Kwa hiyo nilivyokuelewa kwamba tatizo sio uzalishaji wa ndani wa sukari Bali tatizo ni wafanyabiashara ambo kuwadhibiti ndio kama alivyoelekeza waziri kuagiza sukari kutoka nje.
Ndio hivyo au?
Naam.

Na si kuwadhibiti wafanyabiashara wa sukari tu.

Soko la bidhaa zote inabidi lifunguliwe, si bidhaa za nje ziweze kuingia ndani tu, bali hata bidhaa za ndani ziweze kuuzwa nje kwa urahisi bila ukiritimba wa vibali.

Bei zipatikane kwa nguvu za supply and demand, si kwa serikali kulazimisha bei au kwa a heavily protected market.

Protectionism Tanzania haifanyi kazi. Inasababisha rushwa na matatizo ya oligopoly cabals.

Oligopoly ni market ambayo inakuwa controlled na suppliers wachache.

Hapo ndipo wanene wachache wanapanga bei ya sukari kwa ku control supply. It is because if oligopoly. Ukiondoa hiyo oligopoly, hiyo cabalnitashindwa ku control supply, na hivyo itashindwa ku control bei.

This is what Bashe is doing.

Ingekuwa wafanyabiashara wa sukari Tanzania wana nia ya kujiendeleza, kuongeza uzalishaji, kupunguza bei ya sukari kwa ubunifu kwenye uzalishaji bila kuathiri faida, ku kidhi haja ya soko la ndani, ku expand mpaka ku export sukari nje, kwa miaka hiyo ambayo wamepata protection ya serikali, wangeweza.

Tatizo hawana nia hiyo, wana nia ya kuzalisha sukari kidogo na kuiuza kwa bei ya juu, ili kuoata faida kubwa kwa kuuza sukari ndogo.

Huu ni uhuni. This is proce gouging. Ni uhujumu uchumi.

Ikiwezekana hata TANESCO iondolewe monopoly turuhusu makampuni mengine yauze umeme, utaona baada ya mwaka tu TANESCO wananyooka. Sasa hivi wanaringa kwa sababu hakuna competition, ni kazima ununue umeme kwao.

Tanzania hata ikiwa mtu una uwezo wa kutengeneza umeme wa excess, kwa mfano wa solar, huwezi kuuuza umeme back into the grid, kwa sababu TANESCO wana monopoly ya kuuza umeme. Halafu tunalalamika umeme hautoshi. Ujinga mtupu.

Mtu aliyesoma uchumi akajua matatizo ya oligopoly ataelewa kwa nini sukari imekuwa ya bei ya juu Tanzania.

Ukielewa matatizo ya monopoly utaelewa kwa nini umeme ni shida Tanzania.

Ondoa hizo monopoly na oligopoly kwenye umeme na sukari respectively halafu uone matokeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…