Serikali kuondoa changamoto zote uwekezaji

Serikali kuondoa changamoto zote uwekezaji

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
1583425388298.png


SERIKALI itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kuondoa changamoto zote zinazokwamisha sekta ya uwekezaji nchini. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hayo juzi alipotembelea Kiwanda cha Saruji Simba jijini Tanga ambapo alizungumza na uongozi pamoja na wafanyakazi wa kiwanda hicho.

“Uwekezaji huu una tija kwa serikali kutokana na kodi zinazolipwa na wawekezaji kutekeleza miradi ya maendeleo na uzalishaji wa saruji tunajitosheleza ndio maana hatuagizi nje,” alisema. Kuhusu changamoto za kiwanda hicho alisema atakutana na uongozi Machi 10 ofisini kwake Dodoma na mawaziri wa sekta za madini, uwekezaji, viwanda na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini(TRC) ili uongozi wa kiwanda utoe mapendekezo waweze kukisaidia.

Kuhusu changamoto ya usafiri kwa kiwanda hicho, alisema serikali imeagiza mabehewa 100 na kati ya hayo, 40 watayaleta katika kiwanda hicho kinachohitaji mabehewa 80 kwa siku ili kupunguza changamoto ya usafirishaji saruji. “Serikali imeagiza mabehewa 100, kati ya hayo tutayaleta Simba Cement kuondoa changamoto ya usafirishaji. Mnahitaji mabehewa 80,” alisema.

Kuhusu umeme, amesema serikali inatekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji umeme na muda si mrefu changamoto itaisha. Waziri wa Madini, Dotto Biteko alisema kiwanda hicho ni moja ya viwanda ambavyo vimekidhi masharti na vigezo vya viwanda nchini hivyo kuhusu changamoto ya upatikanaji wa changamoto ya makaa ya mawe wataitua.

Mkurugenzi wa Simba Cement, Reinhardt Swart alimweleza Waziri Mkuu, Majaliwa kiwanda hicho kina changamoto ya nishati, usafirishaji, uzalishaji ni mkubwa lakini usafirishaji mdogo. Alisema sehemu kubwa wanatumia usafiri wa treni kusafirisha saruji lakini mabehewa ni kidogo ukilinganisha na uzalishaji mkubwa. Alisema kiwanda hicho ni muhimu kwa uchumi wa nchi na watu wa Tanga kwani kimeajiri wafanyakazi 360 na ajira zisizo rasmi 600.
 
Back
Top Bottom