Izack Mwanahapa
JF-Expert Member
- Apr 21, 2011
- 497
- 236
HONGERA SERIKALI KWA JITIHADA ZA KUMALIZA KIBURI CHA MABENKI YA BIASHARA
Hatua ya Serikali kuhamishia fedha zake zote kutoka kwenye mabenki ya kibiashara inatajwa kuwa inalenga kumaliza kiburi na mikogo ya MABENKI ya biashara dhidi ya wafanyabiashara na wajasiriamali wa kawaida.
Tanzania inatajwa kuwa moja kati ya nchi zenye mabenki mengi lakini inakadiriwa kwamba ni asilimia ishirini tu ya wananchi wake ndio wananufaika na huduma za kibenki japo kuwa fedha zao za kodi kupitia mashirika mbalimbali ya umma ndizo zinazoendeleza mabenki hayo. Kwa sasa Tanzania ina mabenki yapatayo 52.
Kutokana na Serikali na taasisi zake kuweka fedha zake na kufanya miamala mikubwa na mabenki ya kibiashara baadhi ya benki zilijiziuka sana na kuanza kupuuza wafanyabiashara na wajasiriamali wa kawaida wanaohitaji kufanya biashara na benki hizo kutokana na benki hizo kuwa na uwezo wa kujiendesha kwa miamala ya Serikali pekee hivyo wateja wengine kuonekana kama ZIADA.
Hatua ya Serikali kuhamisha fedha zake kutoka kwenye mabenki hayo na kuzielekeza BOT itazilazimisha benki za biashara kurejesha heshima kwa wateja wake (wafanyabiashara/wajasiriamali) wa kawaida ili waweze kujiendesha kwani hakuna namna tena ya kujinufaisha na kujiendesha kwa fedha za Serikali na taasisi zake.
Kwa muda mrefu kumekuwa na urasimu mkubwa kwa mabenki kutokuwa tayari kuelekeza nguvu katika kuwawezesha wajasiriamali wa kawaida kwa kigezo kwamba HAWAKOPESHEKI kwakuwa si walipaji wazuri. Sasa ni wakati wa mabenki kutenga fungu la elimu kwa umma waelimishe wateja wao wa kawaida ili wakopesheke na si kuwakimbia kama walivyokuwa wakifanya Mwanzo kwani kila linalotokea linasababu ya kutokea.
Ni wazi kwamba kutokopesheka kwa watanzania walio wengi kunatokana na kukosa uelewa kuhusu masuala ya kifedha, katika karne ya sasa mabenki yetu yanapaswa kubadilika na kuanza kufanya Business Development Services (BDS) ya mara kwa mara kwa wateja wake badala ya kukaa tu wakisubiri kuuza dhamana baada ya mtu kushindwa kurejesha mkopo. Vikwazo vingi vya kibiashara vinavyomkwamisha mtu/watu kulipa mikopo kwa wakati vinaweza kuepukika ikiwa mabenki yataamua kuwekeza kwenye elimu ya biashara kwa wateja wake.
Hatua hii haimaanishi kwamba sasa ni wakati wa neema kwa wananchi kukopa tu hata kama huna shughuli au kukopa kwa matumizi ambayo si ya kibiashara la hasha! Wananchi wajasiriamali tunapaswa kubadilika pia ili kuunga mkono jitihada za Serikali kwa sisi wenyewe kujitengenezea mazingira ya kuaminika na kukopesheka.
Mabenki pia yanapaswa kuanza kudhamini mawazo mazuri ya kibiashara kama hatua ya msingi. Wasomi wengi katika nchi yetu wanashindwa kuendelea kwasababu ya kukosa mitaji, wanamawazo bunifu mazuri ambayo yakitekelezwa yanaweza kuleta tija katika nchi lakini kwakuwa mabenki yetu hayathamini mawazo (ideas) nzuri za kibiashara badala yake inadhamini hati za nyumba, viwanja, mashamba na magari basi ni wazi ndoto za wasomi wachanga wanaochipukia katika ujasiriamali haziwezi kutimia na ndio maana wanakimbilia siasa.
Mabenki yetu yanapaswa kubadilika ili kuendana na hali halisi ya maisha ya watanzania, uwekezaji mkubwa unatakiwa kufanyika katika kuanzisha na kuendeleza biashara mpya bunifu, zitakazozalisha ajira mpya kwa wingi kwa vijana wa Taifa hili vinginevyo tutakuwa na kundi kubwa la wasomi mizigo ambao asilimia 90 ya taaluma yao itatumika kukosoa na kuhujumu maendeleo ya watu wengine baada ya wao kukosa kazi na fursa za kujiendeleza katika nchi yao.
Nchi nyingi zilizoendelea zilidhamini mawazo na ubunifu wa wataalam wake katika uvumbuzi na uendeshaji wa mambo mbalimbali ya kibiashara. Hakuna sababu ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi katika vyuo mbalimbali kama wote wanategemea kuajiriwa na si kutengeneza ajira kwao na kwa wengine pia.