Serikali kujenga uwanja Manyara kumuenzi Bayi

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Serikali imeahidi kujenga kituo cha michezo katika Mkoa wa Manyara kutokana na eneo hilo kuwa na vipaji vingi vya mchezo wa riadha.

Ahadi hiyo imetolewa bungeni na Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Martha Umbulla.

Amesema mbali na kujenga uwanja katika Mkoa wa Manyara, wanazingatia zaidi kuujenga katika Wilaya ya Mbulu kwa ajili ya kuwaenzi wanariadha walioliletea Taifa heshima kubwa kama Filbert Bayi.

Katika swali la msingi Umbulla alitaka kujua ni lini Serikali itasikiliza kilio cha muda mrefu na kujenga kituo cha michezo ya riadha mkoani Manyara ili vijana wengi wenye vipaji waweze kunufaika.

Waziri amesema Serikali ya Mkoa wa Manyara imepanga kujenga kituo cha michezo cha mkoa, mara baada ya kukamilisha mazungumzo na kukubaliana na wananchi wanaomiliki ardhi husika.


Chanzo: mwananchi
 
Hongera kwao.

Manyara kuna watu jamii ya ethiopia, skinny nigas with mapafu ya farasi, serikali ikiwekeza huko ikavumbua vipaji, maana wapo kina bayi kibao huko. Tutashine olympic kwenye zile mbio wakenya na ethiopia wanasumbua.
 
Back
Top Bottom