Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali iko mbioni kujenga shule maalumu ya wavulana kwa ajili ya Kanda ya Ziwa, ambapo ujenzi huo utafanyika mkoani Simiyu.
Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Juni 16, 2025, wakati akizungumza na wananchi wa mkoa huo mara baada ya kuzindua rasmi shule ya sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Simiyu.
“Tunajenga shule maalumu ya wavulana ya kanda hii ya ziwa, lakini itakuwa hapa Simiyu. Madhumuni yake ni hayo hayo kama ya shule ya wasichana kuwalea watoto wetu wenye vipaji, hasa wa masomo ya sayansi, katika mazingira bora ya kujifunzia, wakike kwao, wakiume kwao, ili tufikie lengo la kuzalisha wataalamu bora wa Tanzania,” amesema Rais Samia.
Ameongeza kuwa ujenzi wa shule hiyo unalenga kuongeza fursa za elimu ya ubora kwa watoto wa kiume wenye uwezo mkubwa kitaaluma, ikiwa ni mwendelezo wa juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuinua kiwango cha elimu nchini
Chanzo: Mwananchi_official