Serikali kujenga hospitali ya kikanda ya kitalii Geita

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Serikali imetangaza kujenga hospitali ya rufaa ya kikanda Geita ambayo itakua pia kituo cha utalii wa matibabu kwa nchi jirani za Congo, Rwanda na Burundi.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili na Waziri wa Afya Mhesh Ummy Mwalimu akiwa Katika maadhimisho ys siku ya Mtoto wa Africa Katoro Mkoani Geita.

Amefafanua kuwa Ujenzi wa Hospital hiyo unatokana na kuongezeka kwa kasi kwa Idadi Watu Kanda ya Ziwa wanaokadiriwa kufika million 13.4 Hivyo huduma za Hospital ya Bugando hazitoshelezi mahitaji halisi ya wakazi hao.

-------

Wizara ya Afya imetangaza kujenga hospitali ya rufaa ya kikanda mkoani Geita ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za kibingwa. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo Jumapili Juni 16, 2019 katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kitaifa Katoro mkoani Geita.

Waziri Ummy amesema licha ya kuwepo kwa Hospitali ya Bugando Mwanza, Serikali imeona ni vema kujenga hospitali nyingine Geita kutokana na idadi kubwa ya wananchi. Amesema Kanda ya Ziwa inakadiriwa kuwa na watu 13.4 milioni. Waziri Ummy amesema hospitali hiyo itakuwa kituo cha utalii cha matibabu kwa nchi jirani za Congo, Rwanda na Burundi .

Aidha, ametangaza kujengwa kwa hospitali nyingine wilayani Geita katika Jimbo la Busanda kutokana na idadi kubwa ya watu wilayani humo. Tayari ujenzi wa hospitali hiyo unaendelea katika jimbo la Nzera na Waziri Ummy ameahidi wizara itatoa Sh500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa hospitali nyingine ya wilaya itakayojengwa Katoro.
 
Safi
Maendeleo hayatakiwi kufanywa kwenye kanda moja tu.

Na akipatikana Rais toka mkoa wa Dodoma (inawezekana Kabudi) ahamishie hospitali ya Muhimbili huko huko Dodoma.
 
Wapeleke na Bandari ya Daresalaam wachukue na Uwanja wa Denge wa DAR
 
Huu ni umimi wa huyo nduli wa magogoni.

Serikali imetangaza kujenga hospitali ya rufaa ya kikanda Geita ambayo itakua pia kituo cha utalii wa matibabu kwa nchi jirani za Congo, Rwanda na Burundi.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili na Waziri wa Afya Mhesh Ummy Mwalimu akiwa Katika maadhimisho ys siku ya Mtoto wa Africa Katoro Mkoani Geita.
Amefafanua kuwa Ujenzi wa Hospital hiyo unatokana na kuongezeka kwa kasi kwa Idadi Watu Kanda ya Ziwa wanaokadiriwa kufika million 13.4 Hivyo huduma za Hospital ya Bugando hazitoshelezi mahitaji halisi ya wakazi hao.
 
Miaka mitatu ni mingi ndugu,huu mpango jiwe atautekeleza mapema sana,now anakusanya nguvu na kuanzisha miradi,tayari ana mbuga,uwanja wa ndege,bandari kavu,zahanati nyingi zinapandishwa hadhi n.k tupo njiani chato kuwa makao makuu ya mkoa,wilaya ya kankonko na biharamulo kua sehemu ya mkoa mpya
Na baaado Geita gold city inakuwa jiji baada ya miaka mitatu ijayo
 
Serikali imetangaza kujenga hospitali ya rufaa ya kikanda Geita ambayo itakua pia kituo cha utalii wa matibabu kwa nchi jirani za Congo, Rwanda na Burundi.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili na Waziri wa Afya Mhesh Ummy Mwalimu akiwa Katika maadhimisho ys siku ya Mtoto wa Africa Katoro Mkoani Geita.
Amefafanua kuwa Ujenzi wa Hospital hiyo unatokana na kuongezeka kwa kasi kwa Idadi Watu Kanda ya Ziwa wanaokadiriwa kufika million 13.4 Hivyo huduma za Hospital ya Bugando hazitoshelezi mahitaji halisi ya wakazi hao.
wakolomije bana!

uzuri wenyewe tunawapiga chini 2020.

embu mtuondokeeni kwenye chama chetu mkaanzishe cha kwenu WUF (Wakolomije United Fools).
 
Serikali imetangaza kujenga hospitali ya rufaa ya kikanda Geita ambayo itakua pia kituo cha utalii wa matibabu kwa nchi jirani za Congo, Rwanda na Burundi.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili na Waziri wa Afya Mhesh Ummy Mwalimu akiwa Katika maadhimisho ys siku ya Mtoto wa Africa Katoro Mkoani Geita.
Amefafanua kuwa Ujenzi wa Hospital hiyo unatokana na kuongezeka kwa kasi kwa Idadi Watu Kanda ya Ziwa wanaokadiriwa kufika million 13.4 Hivyo huduma za Hospital ya Bugando hazitoshelezi mahitaji halisi ya wakazi hao.
Serikali ya ccm au serikali ya Wanyonge? fafanua mkuu
 
Kaona aibu kdg kujenga chato.kaisogeza jirani....uwanja utapata wateja tu....
 
Makaò makuu pia yahamishiwe uko Geita haswa Chato maana kuna watalii wenği sanaaàaa
 
Back
Top Bottom