Serikali kuifutia leseni Kampuni ya Simu ya Yussuf Manji

Serikali kuifutia leseni Kampuni ya Simu ya Yussuf Manji

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,277
2679a94fc2273da2db07da755321dc79.jpg
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imetangaza kusudio la Kampuni ya Mycell inayomilikiwa na Quality Group Limited QGL ambayo imekuwa ikiongozwa na mfanyabiashara maarufu nchini Yussuf Manji.

Kwa mujibu wa sheria, TCRA iliyoanzishwa mwaka 2003 ina jukumu la kusimamia, kutoa na kufuta leseni za mawasiliano kwa kampuni yoyote ambayo imeshindwa kutekeleza majukumu iliyoyabainisha.

"Kampuni ya Mycell imeshindwa kurekebisha ukiukwaji wa masharti ya leseni", inasomeka taarifa iliyotolewa na kuwekwa kwenye tovuti ya mamlaka hiyo.

Kutokana na upungufu huo, "TCRA inauarifu umma kuhusu kusudio la kufuta leseni za Mycell za kujenga miundombinu kitaifa, kutoa huduma kupitia miundombinu hiyo, kutoa huduma kupitia mtandao na kutumia masafa ya mawasiliano".

Kuonyesha juhudi ilizochukua kabla ya uamuzi huo, TCRA imesema Januari 27, 2016 ilitoa amri ya utekelezaji kwa kampuni hiyo kwa kukiuka masharti ya leseni walizopewa na kushindwa kutoa huduma kinyume cha kifungu 21 (a) na (b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielekrtoniki na Posta (Epoca) ya mwaka 2010.

Hata hivyo, Mycell haimo kwenye orodha ya kampuni zilizopewa leseni na TCRA ambazo zimo kwenye tovuti ya mamlaka hiyo.

Mamlaka hiyo imeeleza kwenye taarifa yake ya kusudio la kuifuta Mycell kuwa iliipa kampuni hiyo leseni nne tofauti Novemba 21,2008.

Inafafanua kuwa leseni hizo ni ya kujenga miundombinu kitaifa, kutoa huduma kupitia miundombinu hiyo, kutoa huduma kupitia mtandao wa mawasiliano na kutumia masafa ya mawasiliano.

Kwenye ujumbe wake alioutoa Oktoba, 2011 wakati Quality Group ikitimiza miaka 35 tangu ianzishwe nchini, mwenyekiti Yusuf Manji alitanabaisha vipaumbele vya utekelezaji walivyonavyo.

"Mycell inatekeleza mpango wa biashara unaoiruhusu kukodisha masafa iliyopewa na TCRA kwa kampuni ya nje yenye uwezo na uzoefu mkubwa. Inatarajia kujenga miundombinu imara itakayofanikisha miradi mbalimbali", alisema Manji.

Alisema mpango huo unatokana na fursa kemkem zilizopo kwenye sekta ya mawasiliano nchini hasa kwa kuzingatia njia za kawaida za kufikishiana ujumbe ambazo zimekuwa hazikidhi mahitaji yaliyopo kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia hasa ya habari na mawasiliano (Tehama).
"Sekta hii ina fursa nyingi kwa kampuni zenye teknolojia ya kisasa kuwekeza na kukua. QGL inaona kwamba kuna haja ya kuwekeza kwenye miundombinu na kuziruhusu kampuni za mawasiliano kuongeza ufanisi. Gharama za kupiga simu na data zipo juu nchini ikilinganishwa na ilivyo kwa nchi za Asia zinazonufaika na Tehama kwa kiasi kikubwa", alisema Manji kwenye ujumbe wake wa mwaka 2011.

Mwaka 1997,Manji alianza kuiongoza QGL akihudumu kama ofisa mtendaji mkuu kabla ya baadaye kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kundi hilo, nafasi aliyojiuzulu lakini baadaye akarejea tena kuendelea kuiongoza.
 
Hakuna Rangi ataacha kuona,zile milioni miatano tano za kampeni zilizokamatwa wakati wa kampeni ya urais ndani ya ccm katika Hotel St.Gasper Dodoma ndio inammaliza Manji.
Hakika Manji siyo muelewa mzuri wa kusoma alama za nyakati.
Ristam alisoma mchezo mapema yeye akawahi kusepa yupo salama.
Manji atabaki Historia
 
Mycell wameshindwa kutekeleza majukumu gani?

Kuna vikampuni vingi uchwara vya mawasiliano vilianzishwa wakati wa JK...lakini vimebakia kuwa vikampuni vya kwenye makaratasi tu...

Vimeishia kuhodhi spectrum kiasi kwamba makampuni mengine yanashindwa kufunguliwa...yaani sawa kabisa na mtu aliyehodhi ardhi bila kuiendeleza..

1. Kujenga miundombinu kitaifa (National Network Facilities Licence)

2. Leseni ya kutoa huduma kupitia miundombinu hiyo (Network Services Licence)

3. Leseni ya kutoa huduma kupitia mtandao wa mawasiliano (Application Services Licence)

4. Leseni ya kutumia masafa ya mawasiliano (Radio Frequency spectrum usage Licence).

We jaribu kugugo 'mycell' uone unapata kitu gani cha maana...
 
Huyu jamaa mpaka 2020 itakuwa imebaki story tu..

Wakati wake ulikuwa ukisikia hiyo Tender na Quality Group wamepeleka maombi ni bora ukae kando tu kuliko kupoteza pesa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa mpaka 2020 itakuwa imebaki story tu..

Wakati wake ulikuwa ukisikia hiyo Tender na Quality Group wamepeleka maombi ni bora ukae kando tu kuliko kupoteza pesa..

Sent using Jamii Forums mobile app
Tembo hata umsumbue vipi hawezi kukonda mpaka azidiwe uzito na umbo na Paka wako unaemlea vyema
 
Muda utaongea tu.. Ile nguvu na ushawishi aliokuwa nao wakati uliopita hawezi kuwa nayo tena..

Sent using Jamii Forums mobile app

Hata huo Muda utaongea kuwa nguvu ya maamuzi waliyonayo umebaki Miaka 7 na nusu

Kama kina Manji waliweza ku survive Heka Heka za Nyerere za 1967 kwny Azimio la Arusha wakayumba na baadae wakaimarika Basi sasa hivi hili ni dhoruba dogo ukilinganisha na walipotoka
 
Hata huo Muda utaongea kuwa nguvu ya maamuzi waliyonayo umebaki Miaka 7 na nusu

Kama kina Manji waliweza ku survive Heka Heka za Nyerere za 1967 kwny Azimio la Arusha wakayumba na baadae wakaimarika Basi sasa hivi hili ni dhoruba dogo ukilinganisha na walipotoka
Sawasawa muda ni mwalimu mzuri, kitu kizuri ni kwamba haya maandishi yetu hapa yanaishi. Tutakuja kufufua makaburi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii serikali ya awamu ya 5 ukitaka kufanya biashara fuata masharti. Manji alishafanya mazoea na uongozi uliopita ni lazima makampuni yake yabadilke yafuate masharti.
 
Back
Top Bottom