Serikali kuendelea kuchukua hatua kwa wanaotenda ukatili dhidi ya watu wenye makundi maalumu hususan Wazee

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima @gwajimad amesema kuwa idadi ya Wazee Nchini Tanzania imeongezeka kutoka 2,507,568 hadi kufikia 5,008,339 ambayo ni sawa na 8.1% ya Watanzania milioni 61.7 .

Akiongea na Wajumbe wa Baraza la Wazee Kata ya Mkonze, Mkoani Dodoma leo kuelekea siku ya kupinga ukatili dhidi ya Wazee inayofanyika kila June 15 kila mwaka, Gwajima amewaomba Wakuu wa Mikoa kuhakikisha elimu ya kina inatolewa kwa Wananchi juu ya haki, ulinzi, usalama na ustawi wa Wazee.

"Serikali itaendelea kuchukua hatua stahiki kuwashughulikia ipasavyo wale wote watakaobainika kufanya vitendo vya ukatili kwa makundi mbalimbali katika jamii hususani kwa Wazee"

Maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya Wazee mwaka huu yatafanyika katika ngazi ya Mikoa kote nchini na kauli mbou ni "Wazee wanastahili heshima na usikivu wetu”
 
Back
Top Bottom