Serikali: Kuanzia Januari 01, 2018 kodi ya nyumba za kuishi na ofisi, bei ya ardhi, gharama za elimu/afya n.k ziwe TZS

Mungu mkubwa sana, asante sana Dr Mpango. Tanzania mpya inakuja.
 
Yeah, all long term contracts can be quoted on USD or any other stable currency but the actual payments can be done in TZS at the prevailing exchange rate... This is only for local contracts. For contracts that involves purchases from foreign country, this rule/ requirement should not be applicable because it increases exchange rate exposure...
 
Nothing new.

Ni blah blah za siku zote. Waziri anajaribu kujitutumua ili aonekane anafanya kazi mbele ya mfalme muovu aliyegoma kutubu.

Hadithi zao tumezichoka.

Kesi ya askofu kakobe na TRA itakavyokuwa mahakamani.

WAKILI---- Shahidi wewe ni kamishna wa TRA?

SHAHIDI ---Ndiyo.

WAKILI---Ni kitu gani kilifanya muanze kufuatilia ulipaji kodi wa askofu kakobe?

SHAHIDI---Tulianza kufuatilia ulipaji kodi wa kakobe siku ile aliposema ana pesa kuliko serikali.

WAKILI---Ni kosa kusema kuwa una pesa kuliko serikali?

SHAHIDI---Hapana.

WAKILI---Je kuna sheria yoyote inayokataza mtu kumiliki pesa kuliko serikali?

SHAHIDI----Hapana

WAKILI----Ulishawahi kuwa mnafiki?

SHAHIDI ---Hapana

WAKILI---Ulishawahi kujipendekeza kwa wakubwa zako kazini?

SHAHIDI----kimyaa

WAKILI---Jibu mheshimiwa hakimu anakusubilia aandike jibu lako.

SHAHIDI---Sikumbuki,,

WAKILI-----Kakobe alipokuambia ana pesa kuliko serikali wewe ulijua serikali gani?

SHAHIDI---Serikali kuu ya nchi inayoongozwa na mtukufu rais?

WAKILI----Je katika maneno ya askofu kakobe kuna sehemu yoyote kuna maneno uliyoyataja wewe ya (SERIKALI YA MTUKUFU RAIS)

SHAHIDI---Hapana

WAKILI----Sasa kama kama hapana kwa nini wewe unataka kumuongezea maneno askofu kakobe?

SHAHIDI----Simuongezei ila nilikuwa nahisi alimaanisha serikali hii inayoongozwa na mtukufu.

WAKILI---Unakubaliana na mimi kuwa mahakama haiamini katika ushahidi wa kuhisi?

SHAHIDI---sijui

WAKILI ---Kakobe akija hapa na akaisibitishia mahakama kuwa yeye aliposema ana pesa kuliko serikali alimaanisha yeye ana pesa kuliko serikali ya mtaa au kijiji, je utakubaliana na mimi kuwa ulikurupuka kumshtaki kakobe?

SHAHIDI---Kimyaaa

WAKILI-----Unakubaliana na mimi kuwa maisha ya askofu kakobe yanaendeshwa na sadaka za waumini wake kwa kuwa kazi yake ya kila siku nikuwahudumia kiroho waumini wake?

SHAHIDI-----Ndiyo

WAKILI------Unafahamu askofu kakobe ana makanisa mangapi africa na america?

SHAHIDI-----Sijuii

WAKILI -----Unafahamu askofu kakobe ana waumini wangapi africa na america?

SHAHIDI-----Sijui

WAKILI-------Unafahamu kakobe anaingiza sadaka kiasi gani kutoka waumini wake hapa africa na america?

SHAHIDI-----Sijui

WAKILI-----Je kuna sheria yoyote iliyotungwa na bunge au chombo chochote chenye mamlaka inayotaka sadaka zikatwe kodi?

SHAHIDI-----Hakuna.

WAKILI------sasa ni kodi gani mnafuatilia kwa askofu kakobe kama sadaka hazitozwi kodi?wala hujui idadi ya waumini na sadaka anazopata kutoka kwa waumini wake?

SHAHIDI----Kimyaaaaa

Aise kesi itakuwa tamu sana ikifika mahakamani na mimi napenda ifike mahakamani ili watu wasiompenda kakobe waumbuke.

Kesho jumapili tukutane kwenye makanisa ya kakobe yaliyotapakaa nchi nzima tukatoe fungu la kumi na sadaka zingine kuunga mkono kazi nzuri ya MUNGU anayoifanya hapa kwetu.Hakika askofu kakobe ni mpaka mafuta wa bwana ubarikiwe mtumishi wa MUNGU.

Hahahaha
 
Niliwahi kusoma maandishi fulani yaasomeka hivi " kuku ni kuku tu jogoo ni jina".

Tatizo la Dr. Mpango anashindwa kuelewa kuwa mfanyabiashara anapokokotowa faida kwa bidhaa aliyouza huwa anaangalia thamani ya tzs ukilinganisha na usd.

Ikumbukwe wafanyabiashara wa Tanzania wanaagiza bidhaa nyingi toka nje na huko wananunua kwa dola hivyo tamko hili halisaidii kitu dawa hapa ni kuimarisha sarafu yetu inayoporomoka kila kukicha. Mfano yapo matangazo ya kupangisha nyumba kwa Usd hii haimaanishi mpangaji atumie fedha za kigeni kulipa pango bali atalipa pango hilo kwa exchange rate ya siku hiyo anayolipa.

HIVYO DR. MPANGO ANATWANGA MAJI KWENYE KINU

mgoloko ,
Mkuu
Umeandika hivyo kwa sababu unashindwa kutofautisha kati ya nature and nurture.

Ila nikuhakikishie ina faida nyingi sana zaidi ya 10 kwa Taifa Letu.

Naomba niishie hapo.
 
Mizani zote za kupimia Magari Tanzania, zinatoza adhabu zao kwa kutumia fedha za kigeni ( USD ) mpaka leo, Je hili tangazo linawahusu wao pia.? Sabab mkulu anazipenda sana hizi mizan kwa kweli. Na ye ndo alileta huu mfumo wa utozaj kwa kutumia fedha za kigeni
 
Ukibahatika kwenda nchi za wenzetu pesa ya kwao ndio kila kitu. Hakuna mtu utakuta anapokea pesa ya kigeni ikiwemo dola. SA ni mfano mmoja wapo na Canada kama una US dollar hata maji ya kunywa huwezi kununua. Unahitaji canadian dollar tu.

Kwa wanaopinga hivi hawa wenzetu wote ni wajinga kweli.
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa maagizo kuhusu matumizi ya fedha za kigeni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusisitiza kuwa utekelezaji wake uanze tarehe 1 Januari, 2018.

Maagizo hayo ni kama ifuatavyo: -

i. Bei zote hapa nchini zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania. Bei hizi zinajumuisha kodi ya nyumba za kuishi na maofisi, bei ya ardhi, gharama za elimu na afya, bei za vyombo vya usafiri na vifaa vya kielektroniki.

ii. Bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja wasio wakazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni. Bei hizi zinajumuisha gharama za usafirishaji kwenda nchi za nje kupitia Tanzania, gharama za mizigo bandarini kwenda nchi za nje, gharama za viwanja vya ndege na viza kwa wageni, na gharama za hoteli kwa watalii kutoka nje ya nchi. Walipaji wanaotumia fedha za kigeni watambuliwe kwa vitambulisho vyao kama pasi za kusafiria na nyaraka za usajili kwa makampuni.

iii. Viwango vya kubadilishana fedha vitakavyotumika katika kuweka hizo bei katika sarafu mbili viwekwe wazi na visizidi vile vya soko. Ifahamike wazi kuwa ni mabenki na maduka ya fedha za kigeni tu yanayoruhusiwa kupanga viwango vya kubadilisha fedha kutokana na ushindani katika soko la fedha za kigeni.

iv. Mkazi yeyote wa Tanzania asilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yeyote hapa nchini kwa fedha za kigeni.

Aidha Dkt. Mpango ameviagiza vyombo vya dola viwachukulie hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo haya ya Serikali.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

f87f66ef1447bc402ae03ce31ebfbe2b.jpg
Sawa, Magufuli AKATUBU tu, ni jambo Jema sana.
 
Niliwahi kusoma maandishi fulani yaasomeka hivi " kuku ni kuku tu jogoo ni jina".

Tatizo la Dr. Mpango anashindwa kuelewa kuwa mfanyabiashara anapokokotowa faida kwa bidhaa aliyouza huwa anaangalia thamani ya tzs ukilinganisha na usd.

Ikumbukwe wafanyabiashara wa Tanzania wanaagiza bidhaa nyingi toka nje na huko wananunua kwa dola hivyo tamko hili halisaidii kitu dawa hapa ni kuimarisha sarafu yetu inayoporomoka kila kukicha. Mfano yapo matangazo ya kupangisha nyumba kwa Usd hii haimaanishi mpangaji atumie fedha za kigeni kulipa pango bali atalipa pango hilo kwa exchange rate ya siku hiyo anayolipa.

HIVYO DR. MPANGO ANATWANGA MAJI KWENYE KINU
moshi international school,someni ujumbe Huu ova
 
Back
Top Bottom