Serikali kuanza kusajili machinjio za kuku

Serikali kuanza kusajili machinjio za kuku

Mishi Zawa

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2015
Posts
1,673
Reaction score
2,575
IMG-20190305-WA0016.jpg
IMG-20190305-WA0013.jpg

Nasema kama mlidhani naishia kwa machinga mmeumia. Lazima kodi ilipwe tu. Nchi inaendeshwa kwa kodi ya wananchi.

======

Dar es Salaam. Serikali imejipanga kujenga machinjio ya kuku ya kisasa katika miji mikubwa ili kurahisisha upatikanaji wa kitoweo hicho.

Mbali na kufanya hivyo imeweka mikakati ya kuanzisha machinjio inayotembea ili kutoa huduma katika maeneo ya pembezoni mwa miji zikiwa ni juhudi za kuongeza sifa ya kitoweo hicho kukidhi vigezo vya kushindani kwenye masoko ya kimataifa.

Hayo yamesemwa leo, Jumatatu Februari 25, 2019 katika mkutano uliowakutanisha wadau wa ufugaji kuku pamoja na taasisi isiyo ya kiserikali ya Victoria Finance kujadili namna nzuri za utoaji mikopo kwa wafugaji wa kuku ambao wanakabiliwa na upungufu wa mtaji.

Mtafiti na mratibu wa ndege wafugwao kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk John Kaijage amesema machinjio yaliyopo sasa hayaridhishi kwa wanunuzi wa nje kununua na kutumia bidhaa hiyo.

"Tembelea tu machinjio mnayoyajua kama pale Kisutu uone jinsi hali ilivyo, hautavutiwa nayo hata kidogo. Sasa kama wewe hali ni hivyo itakuaje kwa wanunuzi wetu?" Amehoji Dk Kaijage

"Na hii tutaipendekeza katika bajeti ijayo ili tuweze kutengewa pesa na tunataka maeneo haya yawepo hadi katika kila yalipo machinjio ya ng'ombe," ameongeza.

Katibu mkuu wa chama cha wafugaji kuku nchini, Alloyce Makoye amesema kuanzishwa kwa machinjio hayo kutaongeza thamani ya bidhaa hiyo na kutaongeza uhakika wa ufugaji wa kisasa.

"Kuku watakaochinjwa watakuwa salama kwa afya kutokana na kufanyiwa vipimo, uchinjaji holela usiozingatia viwango hautakuwepo tena," amesema Makoye.

Kwa upande wake, mkurugenzi mtendaji wa Victoria Finance, Julius Mcharo amesema ili kuyafikia masoko hayo wafugaji wanatakiwa kuwa na mtaji wa kutosha, kuongeza uzalishaji na kuwa na uwezo wa kukabiliana na magonjwa.

"Ndiyo maana tumeamua kukutana nao hapa ili kupata majibu sahihi ya changamoto zao na njia sahihi za kuwapatia mikopo hiyo," amesema Mcharo.
 
Kiukweli nchi inaendeshwa kwa kodi na tunaona kutoka kwa wakoloni wazungu, mtu akikwepa kulipa kodi anapata shuruba gani ---to court.

Ila kwa hizi nchi zetu zinazoendelea kukua kiuchumu kulazimisha mwananchi alipe kodi hata kama biashara inadoda au lah mmmh!!.

But taratibu na tutafika siku isiyofahamika.
 
Kulipa kodi sio tatizo ,tatizo ni mifumo isiyofaa.

Mfano: Hakuna mifumo bora na mazingira mazuri ya makazi ,nyumba za biashara.
Watu wanapanga bidhaa barabarani wakati huo huo jirani kuna waliolipia frem na kodi kubwa kwa bidhaa hiyo hiyo. Hayo yanaachwa yaende holela kwa faida ya watawala kisiasa huku wafanyabiashara halali kwenye maeneo husika wakipata hasara. Mwanasiasa anajali madaraka yake na maslahi yake kwa kuumiza mitaji ya wengine lakini wanadai kodi tuuu.

Kodi ni mlolongo badala ya kuwa moja tu inayowekwa kwa mzalishaji na yule anayeagiza toka nje basi. Hata kama ingekua kubwa lakini ingekua haina usumbufu kama huu wa kuwatengenezea TRA mazingira ya rushwa na usumbufu mkubwa kwa wananchi.

Mkapa alijaribu kuja na kile alichokiita kuziba mianya ya rushwa. Lilikua ni jambo jema.

Kwa nini watu walipe kodi direct badala ya kuziweka zote kwa jumla na kuiweka kwa mzalishaji ili au msambazaji.
Ili wale wa rejareja wasiwe na suala la ukubwa wa biashara Bali uwezo wake wa kununua kwa whole salers. Ukinunua katoni ya maji inakua imeshalipiwa kodi zote huko kiwandani hivyo kiwanda ndio kitauza kwa bei ya kuangalia faida hali kadhalika muuzaji mdogo na wa kati.

Haya mambo ya TRA kuingia ingia kwenye maduka ya watu na kutidha watu wakishirikiana na baadhi ya Maafisa wa Polisi wasio waadilifu itaondoka kwa kuweka kodi zote mahali pamoja kwa mzalishaji tu.Hata magendo yangepungua mana ukidhanunua kiwandani au kuagiza nje unakua umeshalipia kodi kazi iliyobaki ni leseni ambayo ingekua na kiwango kimoja tu kwa watu wote wa rejereja kama ilivyo kwa wamachinga.
Let say Sh. 200,000/- kwa mwaka kwa maduka ya rejareja ,400,000/- jumla ,300,000/- mini super market na 700000/- supper market.


Tulitegemea kuona Kwenye duka Leseni tu ya biashara basi. TRA iwe ni huko kwa wazalishaji na wanaoagiza mizigo .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli nchi inaendeshwa kwa kodi na tunaona kutoka kwa wakoloni wazungu, mtu akikwepa kulipa kodi anapata shuruba gani ---to court.

Ila kwa hizi nchi zetu zinazoendelea kukua kiuchumu kulazimisha mwananchi alipe kodi hata kama biashara inadoda au lah mmmh!!.

But taratibu na tutafika siku isiyofahamika.
What are getting in return? Maji ya bomba ni tatizo linaloikaboli 3/4 ya watanzania. Shule hazina walimu wa kutosha na zahanati hazina dawa.
 
What are getting in return? Maji ya bomba ni tatizo linaloikaboli 3/4 ya watanzania. Shule hazina walimu wa kutosha na zahanati hazina dawa.
Binti yangu sky kiongozi yeyote afrika hana uwezo wa kutekeleza hayo unayosema hata ukipewa wewe hicho kiti HUTAFANYA hayo uliyoandika.

Elewa hilo na tembea nalo mfumo umeundwa kufanya vinavyoonekana.
 
Back
Top Bottom