Serikali kuajiri walimu 35,000 mwaka wa fedha 2016/2017

Serikali kuajiri walimu 35,000 mwaka wa fedha 2016/2017

Wakati wadau mbalimbali na wananchi wakiishinikiza serikali kutoa ajira mpya za walimu, serikali imesema kuwa imepanga kuajiri walimu elfu thelathini na tano tu (35,000) katika mwaka ujao wa fedha wa 2017/2018
Idadi ya ajira hizo itajumuisha walimu waliohitimu masomo ya Ualimu kwa mwaka 2015 na 2016 na kwamba hadi sasa kilichobaki ni kuidhinishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amesema ajira za waalimu ni sawa na ajira za sekta nyingine, hivyo amewaomba waalimu kuendelea kuwa wavumilivu hadi pale serikali itakapo tangaza utaratibu wa kutoa ajira mpya.
“Rais ametangaza utaratibu utakaotumika kutoa ajira mpya, hivyo amewaomba walimu kuendelea kuwa wavumilivu hadi serikali itakapo tangaza kuanza kwa utaratibu huo” amesema.
 
Serikali hii imekosa dira, inajiendea tu, watu wengi wanalia hawana AJIRA lakn ziktoka pia watabaki wengine wanalia kwa kukosa nafasi,

Kilio hakitaisha kikubwa kumwomba mungu atuokoe majanga haya
 
Mi naona hata members wanaoleta taarifa za ajira za serikali waalimu wakapimwe akiri wala siyo bure Haya matamko ya kupuuziwa kabisa. Serikali yenyewe haina maelewano huyu kapangua hoja ya mwezake kasema hiki. Jaffo ndiye aliyendanganya kwenye bunge tukufu Nani hasiye mjuwa.
 
Toka waanze kusema ajira wanatoa mwaka umepita sasa, kila siku matamko na matamko ikiwemo na mikanusho isiyoisha!
 
Hayawi hayawi ss yamekuwa, Serikali yatangaza kupandisha vyeo wafanyakazi wake, kuwaongeza mishahara, kuwapandisha madaraja na kuwalipa malimbikizo ya mishahara wafanyakazi wake wote kuanzia januari mwaka 2017. *kupata vichekesho kama hivi Tuma neno VICHEKESHO KWENDA 15671*
Umenchekesha aiseee.uwiiiiii
 
Huu mwezi ukipita kimya bila ajira kutolewa, kila mhusika ajiongeze kwa namna yoyote ile. Maana kama ni kuisoma namba imeeleweka kwa kila mhusika.
 
Hela za kulipa watumishi wapya zmenynuliwa ndege na ujenzi uwanja chato, wanasubr ubak mwez 1 wa bajet 2016/2017 kuisha hafu ndo waajiri ili waombe bajet nyngn tena!

Nchi hii nikama gari bovu! Dreva nae kalewa viroba! Mwsho utafka sema unachelewa tu!
 
Baada ya serikali kusitisha utoaji wa ajira mpya ili kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma nchi nzima.Imepanga kutoa ajira mpya kwa waalimu 35,000 katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Hayo yamesemwa Disemba 2, 2016 na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo katika kikao cha maelekezo ya utendaji kazi kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Jaffo amesema watakao ajiriwa ni wale waliohitimu kozi za ualimu mwaka jana na watakaohitimu mwaka huu.

Kuhusu kikao cha maelekezo kwa watumishi wa umma, amewaagiza Wakurugenzi wa Idara wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Manispaa ya Ilala kuwapangia malengo ya kazi wakuu wao wa idara ili kupima utendaji kazi wao.

“Kila Mkurugenzi hakikisha mnakaa na wakuu wa idara muwekeane malengo ni nini cha kufanya katika mwaka wa fedha husika, wapo watakao tekeleza malengo hayo na wapo wasiotekeleza na kwamba hapo utajua utendaji kazi wao,” amesema na kuongeza.

“Wakuu wa idara pia wakae na watumishi wa chini ili kufanikisha utekelezaji wa malengo hayo. Tunataka utendaji kazi wa watumishi ujibu matatizo na kero za wananchi.”

Aidha, Jaffo amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa kujiamini ili kuboresha utendaji kazi wao.

“Wafanyakazi wafanye kazi kwa kujiamini na kutumia elimu zao na wasio waadilifu wawe waadilifu ili kuepusha migogoro wasifike ofisini na kuwaza kutumbuliwa,” amesema.

Kuhusu madeni ya watumishi wa serikali, amesema TAMISEMI imemaliza kuhakiki madeni ya watumishi hao na kwamba hivi karibuni watalipwa fedha zao.

Chanzo: Dewji blog
Matamko, usanii, porojo...go to hell
 
Back
Top Bottom