Serikali kuajiri walimu 35,000 mwaka wa fedha 2016/2017

geee kay

Senior Member
Joined
Mar 21, 2015
Posts
112
Reaction score
63
Baada ya serikali kusitisha utoaji wa ajira mpya ili kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma nchi nzima.Imepanga kutoa ajira mpya kwa waalimu 35,000 katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Hayo yamesemwa Disemba 2, 2016 na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo katika kikao cha maelekezo ya utendaji kazi kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Jaffo amesema watakao ajiriwa ni wale waliohitimu kozi za ualimu mwaka jana na watakaohitimu mwaka huu.

Kuhusu kikao cha maelekezo kwa watumishi wa umma, amewaagiza Wakurugenzi wa Idara wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Manispaa ya Ilala kuwapangia malengo ya kazi wakuu wao wa idara ili kupima utendaji kazi wao.

“Kila Mkurugenzi hakikisha mnakaa na wakuu wa idara muwekeane malengo ni nini cha kufanya katika mwaka wa fedha husika, wapo watakao tekeleza malengo hayo na wapo wasiotekeleza na kwamba hapo utajua utendaji kazi wao,” amesema na kuongeza.

“Wakuu wa idara pia wakae na watumishi wa chini ili kufanikisha utekelezaji wa malengo hayo. Tunataka utendaji kazi wa watumishi ujibu matatizo na kero za wananchi.”

Aidha, Jaffo amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa kujiamini ili kuboresha utendaji kazi wao.

“Wafanyakazi wafanye kazi kwa kujiamini na kutumia elimu zao na wasio waadilifu wawe waadilifu ili kuepusha migogoro wasifike ofisini na kuwaza kutumbuliwa,” amesema.

Kuhusu madeni ya watumishi wa serikali, amesema TAMISEMI imemaliza kuhakiki madeni ya watumishi hao na kwamba hivi karibuni watalipwa fedha zao.

Chanzo: Dewji blog
 
serikali ya kisanii
 
Si ni huyu huyu alisema zitatoka mapema mwaka huu mwezi february baadae akaliambia bunge kuwa zitatoka mwezi july baada ya bageti kupita.
Je zilitoka kama hazikutoka tutamwamini vip?
 
Wakati wadau wakiishinikiza serikali kutoa ajira mpya za walimu, serikali imesema kuwa imepanga kuajiri walimu elfu thelathini na tano tu (35,000) katika mwaka ujao wa fedha wa 2017/2018

jafo..jpg

Selemani Jafo - Naibu Waziri TAMISEMI

Idadi ya ajira hizo itajumuisha walimu waliohitimu masomo ya Ualimu kwa mwaka 2015 na 2016 na kwamba hadi sasa kilichobaki ni kuidhinishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Akiongea na na East Africa Radio katika maojiano maalum mara baada ya kumalizika kwa mkutano wake na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amesema ajira za waalimu ni sawa na ajira za sekta nyingine, hivyo amewaomba waalimu kuendelea kuwa wavumilivu hadi pale serikali itakapo tangaza utaratibu wa kutoa ajira mpya.

“Rais ametangaza utaratibu utakaotumika kutoa ajira mpya, hivyo amewaomba walimu kuendelea kuwa wavumilivu hadi serikali itakapo tangaza kuanza kwa utaratibu huo” amesema.

Chanzo: EATV
 
Watakuja kukanusha sasa hivi......

Jamaa toka achaguliwe ni kula na wateule wake tu .........

What Goes around come around........

@Gambiadecide.........
 
Ni mwaka kesho,wanaongelea si mwaka huu.2017/2018 bado walimu watasubiri sana
 
Hayawi hayawi ss yamekuwa, Serikali yatangaza kupandisha vyeo wafanyakazi wake, kuwaongeza mishahara, kuwapandisha madaraja na kuwalipa malimbikizo ya mishahara wafanyakazi wake wote kuanzia januari mwaka 2017. *kupata vichekesho kama hivi Tuma neno VICHEKESHO KWENDA 15671*
 
2017/2018 itakuwa ile miezi miwili ya kusitisha Ajira itakuwa imetimia mbona Mapema sana?
 
Moyo mashine. 2017/18 itafika tu si mbali sana. Too long is not forever
 
Back
Top Bottom