Serikali kuajiri walimu 35,000 mwaka wa fedha 2016/2017

Serikali kuajiri walimu 35,000 mwaka wa fedha 2016/2017

2017/2018 af walim 35 elf tu kat ya karb walm 70 ef waliohtm 2015 na 2016. mwaka 2016 umepta kmya kmya 2 ngoj 2subir vtendo au kaul ya kiongoz mwngne kairuk au chawene
 
Kupata waalimu competent, nao waingizwe katika mchakato wa kuwa INTERVIEW basi. Sio kusomba kila kichwa, ajira kama za sector zingine!!!
 
Naona ule mterezo wa kada ya Ualimu unafutika sasa.
Na uishe tu, maana hakuna namna. Saizi nao watahusishwa kuhudhuria uwanja wa taifa, mara kigamboni mara duce sijui mara maktaba...wajiandae kuzungukia maeneo ya jiji la Dar bila kuchoka wala kukata tamaa
 
Hio ni mwakani mwezi wa 8 au wa 10 huko,bado walimu wana mwaka 1 mwingine wa kusota mtaani
 
Wakati wadau wakiishinikiza serikali kutoa ajira mpya za walimu, serikali imesema kuwa imepanga kuajiri walimu elfu thelathini na tano tu (35,000) katika mwaka ujao wa fedha wa 2017/2018




jafo..jpg

Selemani Jafo - Naibu Waziri TAMISEMI



Idadi ya ajira hizo itajumuisha walimu waliohitimu masomo ya Ualimu kwa mwaka 2015 na 2016 na kwamba hadi sasa kilichobaki ni kuidhinishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Akiongea na na East Africa Radio katika maojiano maalum mara baada ya kumalizika kwa mkutano wake na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amesema ajira za waalimu ni sawa na ajira za sekta nyingine, hivyo amewaomba waalimu kuendelea kuwa wavumilivu hadi pale serikali itakapo tangaza utaratibu wa kutoa ajira mpya.

“Rais ametangaza utaratibu utakaotumika kutoa ajira mpya, hivyo amewaomba walimu kuendelea kuwa wavumilivu hadi serikali itakapo tangaza kuanza kwa utaratibu huo” amesema.


Chanzo: EATV
Tamko jingine la mwanasiasa,kamwe usimwamini maana kesho litakuja tamko jingine
 
SIASA NDO IMETAWALA TZ, HAKNA KITU KIPYA ZAIDI YA MATAMKO! HAKUNA JIPYA HAPA!
 
Rekebisha hapo si 2016/2017 ni 2017/2018.ni mwaka ujao.sio bajeti ya mwaka huu
 
Tunachotaka kusikia ni trh ngap,mwezi gani na mwaka gani ajira zitatoka hatutaki kusikia hayo makande na maharagwe tena
 
Bajet ya 2016/2017 inaisha June 30,2017 je mwez gani ajira ndo znatoka? Kwa nn hakna uwaz huu zaid ya kujibu kisiasa? Wanachosha kwa matamko ya kila siku!
 
Bajet ya 2016/2017 inaisha June 30,2017 je mwez gani ajira ndo znatoka? Kwa nn hakna uwaz huu zaid ya kujibu kisiasa? Wanachosha kwa matamko ya kila siku!
Sio mwaka huu wakuu,ni bajeti ya mwaka ujao wa serikali yaani,2017/2018.kwa hio ni kuanzia mwezi ws 8 mwakani.
Saiv pesa imeenda kununua ndege
 
Back
Top Bottom