JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
Agizo la serikali kwa wafanya biashara wadogo (machinga) mjini Kibaya wilayani Kiteto Manyara limeanza kutekelezwa kwa machinga kuanza kupatiwa vitambulisho.
Katika kile kilichoelezwa kuwa ni kutambulika kwa wafanya biashara hao, serikali imeweka utaratibu maalumu wa machinga kuchangia mapato kulingana na mitaji yao.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo mfanya biashara mdogo anayetambuliwa na serikali ni yule mwenye mtaji wa chini ya mil 4.
Mhandisi Tumain Magesa, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto akigawa vitambulisho kwa wafanya biashara hao mjini Kibaya aliwataka wakate leseni kwanza kwa Mkurugenzi mtendaji wa halmadhauri ya Wilaya.
Hata hivyo malalamiko kwa wafanya biashara hao yalikuwa ni kutaka kutolipia mapato TRA kutokana na madai ya makadirio makubwa ya kodi
Akitoa ufafanuzi juu ya ulipaji wa kodi meneja wa TRA Kiteto Wiljones Kisamba alieleza kuwa elimu kwa mlipa kodi itaendelea kutolewa ili kila mmoja aelewe
Alisema TRA wamekuwa wakitoa elimu kila Mara tatizo kwa wafanya biashara ni kutuma wauzaji ambao hawatoi mrejesho kwa waajiri wao
"Huwa tuna mazungunzo na wafanya biashara katika makadirio hayo, tatizo lililopo wanapoitwa hawaji wenye mali wanakuja wauzaji ambao hawatoi mrejesho kwa matajiri"
Emmanuel Papiani mbunge wa Jimbo la Kiteto aliomba TRA kuwa karibu na wananchi na kujenga mahusiano mema ya ulipaji kodi.
Katika uzinduzi huo jumla ya vitambulisho 200 vilitolewa kwa wafanya biashara hao wadogo kama Njia ya kutambulika na Serikali katika kazi hizo..
Sent using Jamii Forums mobile app