Serikali kampuni za udalali tunakufa njaaaa

lusaka city

Senior Member
Mar 17, 2015
146
116
Habari za usiku wapendwa wanajamvi Leo nimeleta Uzi huu kwa niaba ya watu wanaomiliki kampuni za udalali hapa bongo.yafuatayo ni baadhi ya matatizo yqnayopelelekea kampuni nyingi kufungwa kwa ukata wa kazi na pesa.

1.serikali kubadilisha mfumo wa makusanyo mbali mbali.

Moja ya kazi ambazo zilikua zinatupunguzia njaaa ni pamoja na kushika tenda za makusanyo ya ushuru kama wa maegesho,ushuru wa stand za mabasi,ukusanyaji taka nk katika halmashauri mbali mbali hapa nchini .baada ya mfumo wa makusanyo kurudishwa mikononi mwa halmashauri husika tumepoteana sana

2. Baadhi ya taasisi kutumia madalali wasio wa mkoa husika.
Taasisi mbali mbali kama vile bank zinatumia madalali ambao wanapitishwa na makao makuu ya taasisi husika.mfano crdb,nmb,CBA kazi za mikoani madalali wanatafutwa dar kwa nini kusiwekwe utaratibu wa utakao wawezesha na makampuni ya mikoani kufanya kazi katika mikoa yao ata kwa kushirikiana na huyo Dalali mgeni.itasaidia kupunguza njaaaaa kwetu

3.madalali wa mitaani wasio na sifa

Hili ni tatizo sugu sana hawa jamaa wa mtaani hawalipi Kodi wala kutambulika sehemu yoyote wamekua wakichukua kazi juu kwa juu yaani na wapo wengi kweli serikali iwekwe mkazo juu ya hawa jamaa kufanya kazi

Wanajamvi nawasilisha tuendelee kuongezea nyama kwa matatizo mengine...........
 
Nikisikia tu dalali basi mawazo yangu ni mtu mjanja mjanja, tapeli, mishenitown, mwenye info nyingi na zingine za uogo ili mradi apate hela...
Sasa kwa utawala huu mtu wa kwanza kabisa kuwa affected ni huyo dalali.
Any way naweza kuwa wrong kimtazamo juu darari.
 
Najua udalal ni fani kama zilivyo fan zingine. Kama mambo yamebana jarib kubadilisha upepo kwenye fan zingine kwa kuwa fulsa bado zipo nyingi ndugu yangu. Tuliza akir pambana na mazingira utafanikiwa
 
Back
Top Bottom