Serikali iweke wazi tu kuwa hakuna mikopo ya wajasiriamali inayotolewa na mabenki i.e. TADB

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Nov 30, 2022
607
553
Habari,

Kumekuwa na taarifa nyiiiiiingi kutoka serikalini kuwa wajasiriamali wanapata mikopo kutoka benki mbalimbali ikiwemo TADB, mimi nakataa taarifa hizi kwa 100%.

Nimeona wanaopata mikopo hiyo ni vigogo na mafisadi kwani mkulima ambaye anaanza au anataka kupanua shughuli zake za kilimo amekuwa akiwekewa vikwazo kedekede hasa benki kutaka mchanganuo wa mapato na matumizi pamoja na taarifa ya akaunti ya benki ya mkulima ya mwaka mzima yenye mzunguko wa fedha wanaotaka wao kisa tu mjasiriamali hawezi kutoa 10%,ni mjasiriamali gani yupi mdogo anayeweza kutekeleza haya?

Lakini mkulima mkubwa yeye anachofanya kila leo ni kuzungusha na kufaulisha mkopo huo wa kilimo kila mwaka na baadae anatangazwa amefirisika hawezi kurejesha mkopo wa kilimo aliochukua na mwishowe benki zinakufa kisa tu mkopaji anatoa 10%.

Udalali wa taasisi/mawakala wa mikopo ya kilimo pia kunachangia wajasiriamali kutokidhi vigezo vya kukopesheka i.e. PASS ambao wamekuwa wanataka kulipwa kwanza % kadhaa na mjasiriamali eti ndiyo wamsaidie kupata mkopo wa kilimo baada ya kulipa kiasi fulani cha sehemu ya mkopi i.e.25% ya mkopo anaotaka mjasiriamali,sasa ni mjasiriamali yupi anayeweza kupata fedha hizo kabla ya kuanza kilimo kama siyo uhuni?

Mimi nashauri kama serikali inataka kuinua wajasiriamali i.e. wakulima wadogowadogo basi waondoe urasimu huu uliopo kwa kuanzisha madirisha ya wajasiriamali moja kwa moja yatakayotoa mikopo ya kilimo kutoka serikalini kupitia viongozi wa maeneo anapokaa mjasiriamali husika i.e. Maafisa ugani ambao watamsikiliza mjasiriamali na kutembelea shamba lake na kuona kilimo anachotarajia kufanya wakamsaidia kuandaa andiko lake likapitishwa na serikali na serikali kutoa hundi kwa mjasiriamali kulingana na kiasi akichoomba na mradi husika hata kwa awamu na kukaguliwa na maafisa ugani kwa kila hatua na kuona kama ametimiza hatua ya kwanza au ya pili ya mradi na kuendelea.

Lakini hii ya kudai mjasiriamali atafanikiwa kupitia mikopo ya ushirika au vikundi ni uongo kwa ni rahisi wanavikundi au wanaushirika kuzembea na fedha ikapotea heri jitiada ya mjasiriamali mmoja mmoja na siyo vikundu au ushirika kwani maafisa ushirika ni mchwa unaokula vyama vya ushirika au vikundi hivyo.

Mwisho serikali ioneshe tu njia na nia ya kumsaidia mkolo wa kilimo kwa mjasiriamali mmojammoja kulingana na dhamana alizo nazo i.e. Shamba lake na ikiwezekana kuanzisha bima rasmi kwa wakulima wajasriamali itayoweza kufidia mkopo iwapo kutatokea janga au tatizo lolote kwenye mradi husika iachane na hadithi za kusema imeoeleka pesa nyingi kwenye mabenki kwaajili ya wajasiriamali na imeanzisha sijui mabeki ya kilimo huo ni uhuni.

Naomba kuwasilisha.
 
Hao PASS ndio TAKATAKA kabisa, serikali MAKINI ingewafutilia mbali
 
Back
Top Bottom