Serikali iweke faini kwa Mabango yanayochafua mazingira

Jun 5, 2019
43
61
Tumekua tukiona kama kuna mikutano ya injili au shule inakaribia udahili, tution n. K basi mabango ya matangazo hubandikwa kiholela kila sehemu.

Ukienda pale ubungo, flyover inapendeza ila imechafuliwa na mabango kedekede ya makaratasi tena yameisha muda wake na bado yapo na yanaharibu taswira ya uzuri wa eneo lile.

Rai yangu kwa serikali na halmashauri kufuatilia chanzo cha hayo mabango ni nanj aliye nyuma na uchafuzi huo. Kama ni mkutano wa injili au wowote basi faini alipishwe huyo mwenye mkutano au mwenye shule kwa ajili ya watakaosafisha na kutoa hayo mabango.
 
Back
Top Bottom