Kilimo ndicho utu wa mgongo lakini Serikali naona haina msaada wowote wa kuwasaidia wakulima. Nitoe mifano michache tu.
(1) Wakulima tunahimizwa kulima pamba
(2) Wakulima tunahimizwa kulima kahawa
(3) Wakulima tunahimizwa kulima mahindi
(4) Wakulima tunahimizwa kulima maparachichi
(5) Wakulima tunahimizwa kulima alizeti, michikichi kwa ajili ya mafuta nk.
Sasa nije kwenye hoja.
Lini Serikali ikamtafutia mkulima soko ili apate bei nzuri?. Lini Serikali ikatoa ruzuku kwa wakulima ili walime kwa tija. Lini Serikali imefanya ufuatiliaji kuona wakulima wanazingatia taratibu zote za kilimo.
Lini Serikali ikawasaidia wakulima kwa njia ya umuagiliaji?. Jibu ni hakuna. Wakulima wameachwa maskini bila msaada wowote.
Nitoe mfano ulio wa wazi kabisa. Serikali iliwahamasisha wakulima wa Njombe walime maparachichi na wakulima wakaitikia kwa asilimia kubwa. Leo hii wakulima wamepata mavuno makubwa sana tatizo ni soko.
Je mkulima wa kule ndani kijijni anaweza kutafuta soko bila Serikali kuingilia kati?. Mfano mwingine ni kahawa.
Wakulima wa Kagera wamepata kahawa nyingi na jirani yao Uganda wanauza kwa bei kubwa. Hivi sasa Viongozi wa maeneo hayo wanakimbizana na wakulima wanaotorosha kahawa kwenda Uganda. Hapa nani ana kosa.
Mkulima anatafuta bei kubwa kwa maana ya supply and demand. Kama kungekuwa na Serikali sikivu ile tofauti ya bei ya Uganda ingefidiwa na Serikali yetu kuliko kutesa wakulima.
Siyo kuwa wakulima hawataki kulima mazao mbalimbali bali tatizo kubwa ni soko. Leo hii kilo moja ya pamba ingekuwa ni Tshs.3,000 kila mkulima angelima pamba. Ninaiomba Serikali ije na sera ya kuwasaidia wakulima.
Pale ambapo bei imekuwa chini basi Serikali iingilie kati kuwa saidia wakulima kwa kufidia tofauti ya bei. Mbona nchi nyingi zina utaratibu huu.
Tuanzie na fidia ya maparachichi ambayo yamekosa soko.