Serikali iwe makini na Lissu maana hana cha kupoteza

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,219
Nimekaa na kutafakari sana matendo anayafanya huyu Lisu na nimekuja na mawazo binafsi kwa vyombo vya usalama na mamlaka za juu za kiuongozi.

Ni lazima serikali itambue na kuelewa Tundu Lisu hakuanza leo kuikosoa serikali ila alianza zamani tofauti ya Lisu huyu wa awamu ya tano na Lisu wa awamu zilizopita ni kuwa Lisu wa awamu zilizopita hasa ya tano alipolipuka mahali alizimishwa na vitu tusivyovijua ama alikuwa akifanyia watu fulani kazi ambazo sisi hatuzijuwi lakini huyu wa awamu ya tano ndio sura ya yule yule wa awamu ya nne...

Yaani sasa tumemgunduwa huyu Lisu ni wa aina gani. Kiukweli kabisa kile anakifanya kwa sasa sio siasa ila kama ni mtaalam wa mambo ya kisiasa tunaweza kusema anatumwa na mabwana zake ktk siasa kuja kuchafua then wanasubiri what next..

Kiukweli kabisa kama kweli huyu angekuwa yule Lisu wa awamu ya nne basi huenda nilitegemea angemuunga mkono rais kwa kazi anaifanya ila badala yake sasa amekuwa kuwadi wa nchi za Magharibi akisahau kuna nyumbani na kwa dhambi anaifanya inaweza kuleta majanga makubwa ndani ya familia yake mwenyewe akalia na kukumbuka majuto ni mjukuu. Well hapa nilikuwa namuelezea tu aina ya huyu mtu.

Lisu amekata tamaa na kwa aina ya siasa ameifanya kwa kipindi kifupi ni dhahiri shahiri nafsi inamsuta na kutoamini kwanza kuwa hai na pili jinsi tukio limetokea. Lisu anaweza kutuficha kwa muda mrefu sana ila nina uhakika anajua dhambi yake na ni kwanini haya yote yametokea na ni kwanin amejivika koti la kuhukumu serikali ya Magu ndio ilitaka kumpoteza.

Katika hali kama hii ni bora serikali kujikita katika smartness yaku resolve issue bila kujibizana naye maana huyu bwana anajua kile anakifanya maana yupo katika hali ya kukata tamaa ameshaamua kama mbaya na iwe ila yeye anaharibu.

Mambo yanaendelea yamepangwa kwa ustadi mkubwa hivyo ni muhimu serikali badala ya kumjibu ikatafuta njia za kumfanya asisikie hamu ya kuongea na akaendelea na matibabu yake akiwa bubu na hili linawezekana.

Kiukweli mahali amefika sio pazuri na sisi kama serikali ni vyema kujipanga tukijua Tundu sio CHADEMA ila ni zaidi ya tunachokijua wapo washabiki wake mpaka CCM na tujiulize why?

Njia ya ukimya na kutojibizana na Lisu ndio msumari wa mwisho kwenye maneno ya Lisu ifike mahali ajutie kazi zake bovu na akumbuke shida anawapa familia yake..
 
TumainiEl Dah nilidhani ndugu yake umeleta mrejesho wa upelelezi wa waliomfanyia shambulio Lissu kumbe umekuja kumsema zaidi mtu aliyeshambuliwa kwa risasi zaidi ya 20. Hongera ndugu
 
Back
Top Bottom