Serikali iwaongezee Alama za ufaulu wanafunzi waliofanya mitihani mwaka jana

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
2,946
2,929
Saalam!

Nchi kadhaa duniani zimeathirika kiuchumi, kielimu, kisiasa nk.

Kutokana na hali hiyo, Serikali nyingi zimechukua hatua za kuzikwamua sekta mbalimbali hasa za kiuchumi kuziongezea mitani.

Athari hizo nasi zimetukumba kiuchumi, kielimu nk.

Wanafunzi walilazimika kufunga shule kwa miezi mitatu bila kusoma wala tuition kwakuwa nchi ilichukua tahadhari ya ugonjwa wa covid19.

Kwa mantiki hii, niiombe serikali kupitia wizara yenye dhamana ya elimu kuwaongezea alama za ufaulu watoto ambao matokeo yao siyo mazuri.

Kufanya hivyo itakuwa Kama zilivyofanya serikali zenye uwezo kifedha kuingiza mitaji kwenye sekta na kuziokoa na kufirisika

Wapo watoto ambao walikuwa wanafanya vizuri kabla ya covid 19,baada ya kukaa nje ya masomo kwa siku90 walianza kufanya vibaya

Serikali ifikirie hili.

Asante
 
Iwaongezee ufaulu?

Nipe kiboko naona humu bila kuchapana mambo hayaendi.

Muongezee wa kwako ufaulu. Msitake kucheza na elimu kabisa.
 
Ni kweli nyumbani ni nyumban mara unakwaruzana na mzazi unadhan masom.yanaenda hap tusubri tuone kiukwel.matokeo sio mazuri mkuu
 
Hakuna hicho kitu hapa duniani kuwaongezea watoto maksi, huyo aliefeli mwambie arudie mitihani tu, kwani hao waliofaulu waliongezewa maksi?

Kwanza mitihani yote ilitungwa kwa standard moja, hapo hakuna mlango wa kutokea.
 
Back
Top Bottom