Traxtion
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 5,895
- 11,788
Picha zote nilizotumia kwenye uzi huu ni za Kahama
Mimi sio mkazi wa Kahama ila huu mji unahitaji attention
Kahama ni mji unaokua kwa kasi na mzunguko wa hela upo vizuri kwa level za Kitanzania
Population inakua kwa kasi na sababu kuu ni shughuli za uchimbaji madini
Lakini hivi karibuni tumeona mgodi wa Buzwagi umefungwa, inaonekana madini yameisha au yamebaki kidogo
Serikali ikasema itajenga viwanda katika eneo ambapo mgodi huo ulikuwepo, ni idea nzuri lakini viwanda ni heri viwe vingi sana, sio tu mnajenga viwanda kumi. Viwepo viwanda hata zaidi ya 100 huko
Mtazamo wangu ni kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuanzisha Industrial park kubwa Kahama, ikiwezekana iwe kama ile ya SINO-TAN inayojengwa Kibaha
Kwa nini? Kama mji umeweza kukua kwa kasi vile bila mchango mkubwa wa serikali na sio hivyo tu, bado unaendelea kukua hadi sasahivi maana yake serikali inapaswa ichangamkie mji wa Kahama kutumika kutengeneza ajira. Kwa mkono wa serikali Kahama itaendelea zaidi tena kwa kasi ya juu.
Miji inayokua kwa kasi ina faida sana Tanzania, kwa mfano mji kama Kahama ndani ya muda wake wa ukuaji umesaidia vijana wengi sana kujikwamua kiuchumi. Wengi wameenda kuwekeza biashara zao Kahama na matunda yake wameyaona
Tanzania inapaswa kuhakikisha miji yote yenye watu wengi inapewa support na kuongeza mzunguko wa hela ili isizidi kukua.
Inasikitisha kuona miji inakua kwa kasi halafu serikali inaangalia tu mpaka baadae inaanza kujifia au maendeleo yanakuwa ya konokono, kama Moshi tungekuwa nayo serious ungekuwa mji mkubwa wenye fursa nyingi za kiuchumi, badala yake umebaki kuwa mji mdogo wa watu laki 2 sijui, na maendeleo yake ni yale yaliyofanywa miaka ya nyuma
Kwa upande wa Kahama serikali inapaswa kuhakikisha inaboresha miundombinu. Barabara za Kahama zina mashimo, na zimejaa michanga. Zinahitaji kuwa refurbished au zijengwe upya katika viwango vya juu
Pia stendi ya mabasi ya Kahama ni duni, inapaswa kuboreshwa au ijengwe stand mpya lakini isijengwe mbali na makazi ya watu kama tulivyofanya maeneo mengine. To make the town more alive stand kuu ijengwe ndani ya mji
Kwa sasa stendi ya Kahama ndio hii
My take: Serikali haiwezi kutoa ajira kwa kila mtu lakini tunajua inaweza kuandaa mazingira mazuri ya kujiajiri. Ukiondoa kilimo na ufugaji ambavyo hufanywa zaidi vijijini, ukija mijini ili mtu ajiajiri na kupata pesa kunafaa kuwe na mzunguko wa hela
Serikali inapaswa kujenga viwanda, vyuo vikuu, miundombinu bora na kualika wawekezaji waje kuwekeza kwenye miji hii ili pesa izunguke. Inakuwa rahisi kwa Watanzania kujiajiri na kupata maisha mazuri
Sio tu Kahama, Tanzania tuna miji ambayo hatujui kuitumia. Miji yetu ina watu ambao wengi wao ni vijana, na watu ndio utajiri mkubwa kwenye nchi yoyote ile, ili kuuona utajiri wa watu ni lazima tutengeneze mazingira ya kuingiza hela kiurahisi.
Sio tu Kahama, serikali inapaswa ianze kuja na mipango ya kuifanya miji ya Tanzania kuwa alive zaidi kibiashara. Miji kama
1. Morogoro
2. Moshi
3. Mbeya
4. Mtwara mjini
5. Kigoma mjini
6. Iringa
7. Katoro
8. Geita
9. Makambako
10. Bukoba
11. Songea
12. Njombe
13. Sumbawanga
14. Masasi
15. Babati
16. Kibaigwa
17. Gairo
18. Tunduma
19. Tunduru
20. Tandahimba
21. Ikwiriri
22. Mkuranga
23. Buseresere
24. Kasulu
25. Chalinze
26. Songwe
Na mingine mingi ina watu wengi lakini kinachokosekana ni mzunguko wa hela wa kutosha.
Tufikirie, tutafute namna ya kuiamsha miji yetu kibiashara
Si mnaona jiji la Dar lilivyo. Dar es Salaam ni one of Tanzania's biggest success. Licha ya kuwa jiji lenye matatizo mengi lakini ni kitovu cha biashara kwa Tanzania. Ni jiji lililosaidia watu wengi sana kufanikiwa kimaisha kupitia biashara. Naliheshimu sana jiji la Dar
Sasa haya mambo yasiishie Dar tu, tusambaze maendeleo na kuongeza mzunguko wa hela ili vijana wajitafute kimaisha kwenye maeneo mengi kupitia biashara. Isiwe Dar tu