Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 464
- 687
Demokrasia hasa hii ya vyama vingi sio utamaduni mkongwe katika uongozi wa nchi nyingi duniani. Kihistoria mfumo mkongwe wa uongozi ni mfumo wa kifalme. Katika mfumo huu wakuu wa nchi hawapati haki ya kutawala kwa kuchaguliwa na wananchi, bali hupata haki ya kutawala kwa kuzaliwa kwenye familia ya kifalme. Katika mazingira hayo, mfalme hawajibiki kwa wananchi wake, bali wananchi na ardhi yao huwa ni mali yake binafsi yaani subjects.
Uzoefu wa dunia wa kuwa na wafalme wasiopigiwa kura wala kuwajibika kwa wananchi, ni kupuuzwa kwa wananchi, utozaji wa makodi makubwa, ufujaji wa rasimali za umma, uonevu, upendeleo, ubaguzi na uchawa. Mambo haya ndiyo yaliyowachochea waingereza kumuaasi mfalme wao, John wa uingereza (1199-1216) mpaka alipokubali kusaini mkataba wa Magna Carter June 15, 1215 kukubali kujipunguzia madaraka, kuleta utawala wa sheria, kupunguza kodi, na kuacha kuadhibu watu nje ya utaratibu wa kisheria (customs and liberties of London)
Hali ya namna hiyo hiyo huko Ufaransa, mnamo Juni 20, 1789 ilisababisha kuanza rasmi kwa French revolution, vuguvugu lililokomesha utawala mfalme Luis XVI na kupelekea kuzaliwa kwa mfumo wa jamuhuri, ambapo, nchi zinaongozwa na mtu anayechaguliwa badala ya mfalme wa kurithi, na kwa kufuata sheria zilizotungwa na bunge badala ya amri za kifalme.
Matarajio ya mtindo wa utawala wa Jamhuri ilikuwa ni viongozi watawaogopa na kuwaheshimu wananchi maana ndio wanaowaweka na kuwatoa kupitia kura zao, na kwamba viongozi ndio watawajibika kwa wananchi badala ya wananchi kuwajibika kwa viongozi; zote mbili zikiwa ni tofauti na hali ilivyo katika tawala za kifalme. Faida hizi za kufuata utawala wa jamhuri zilipoonekaka mapinduzi dhidi ya tawala za kifalme yakaenea Ulaya yote na ndio ukawa mwisho wa wafalme katika maeneo mengi duniani.
Mambo yaliponoga, dunia ikaona kuchagua tu haitoshi, ikaja hoja na haja ya uwepo wa ushindani wa watu wanaoomba kuwa viongozi kueleza watafanya nini wakichaguliwa, na hapa ndipo demokrasia ya vyama vingi ilipozaliwa. Hii ikiwa ndio hatua ya juu kabisa ya kujengeka kwa falsafa ya mamlaka ya wananchi na utumishi viongozi.
Haitegemewi katika nchi ambayo ni jamuhuri na yakidemokrasia, viongozi kuwapuuza na kutokuwajali wananchi. Hili likitokea ni wazi kuwa hapo hakuna jamuhuri bali kuna mfalme anaeigiza kuwa jamuhuri. Msingi wa jamuhuri ni mamlaka ya wananchi, na utumishi wa viongozi. Katika jamuhuri, viongozi ndio wanajipendekeza kwa wananchi kwakuwafanyia mambo mazuri ili waendelee kuchaguliwa tofauti na utawala wa kifalme ambapo ni wananchi wanaojipendekeza kwa mfalme ili awahurumiwe au wapendelewe.
Ikifika wakati serikali haiogopi tena wananchi, kuwa na hakika serikali hiyo haiwezi kuwajibika tena kwa wananchi. Hili likitokea basi tutakuwa tumerudi nyuma kwenye enzi za ufalme ambapo utawala wa sheria utakuwa ni kiini macho, serikali zitatoza makodi makubwa, zitafuja mali za umma, zito onea watu bila kujali chochote na wananchi hawatakuwa na chakuifanya.
Ni muhimu kwa wadau wote kuhakikisha wanailinda msingi mkuu wa jamuhuri ambao ni mamlaka ya wananchi. Vyombo vyote vya dola vinayo nafasi yenye umuhimu wa kipekee kujipima kuona kama wanayoyafanya yanalinda mamlaka ya wananchi kwa kiasi gani. Jambo lolote lile linalopora mamlaka ya wananchi ni kinyume na katiba na halipaswi kuvumiliwa.