Serikali isiyapuuze madai ya wahadhiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali isiyapuuze madai ya wahadhiri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 13, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,784
  Trophy Points: 280
  Date::6/13/2009
  Serikali isiyapuuze madai ya wahadhiri

  Mwananchi

  KUNA fununu kwamba, wahadhiri na wafanyakazi wa vyuo vikuu vya umma nchini, wanajianda kuitisha mgomo kwa ajili ya kuishinikza serikali iwalipe posho zao za pango za miaka mitatu iliyopita na kuongezewa mafao ya kustaafu.

  Kwa mujibi wa habari iliyochapishwa na Gazeti la Mwananchi jana, wahadhiri hao wanakusudia kuitisha mgomo huo mpaka hapo serikali itakapokubali kuwalipa madai yao na kwamba, walishawasilisha malalamiko serikalini, lakini mpaka sasa hawajapatiwa majibu.

  Katika kutafuta njia ya kuwasilisha madai yao hayo, wasomi hao wanajipanga ili wakutane kujadili namna ya kuibana serikali. Mwenyekiti wa Umoja wa Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), Dk Damas Nyaoro alifahamisha kuwa mkutano wao wa mwisho ulifanyika Aprili, wakati huo huo waliikumbusha serikali kwa njia ya maandishi juu ya madai yao hayo, lakini mpaka sasa hawajajibiwa.

  Waswahili wanasema: "Lisemwalo lipo, kama halipo laja". Kwa maana hiyo ni dhahiri kwamba, wahadhiri hao wanataka kutumia njia ya kugoma ili walipwe haki zao.

  Sote tunafahamu umuhimu wa elimu katika karne hizo; lakini elimu bila walimu na wahadhiri ni kazi bure. Pia wahadhiri ambao kwa ujumla ni wataalamu waliobobea, wasipowekewa mazingira mazuri ya kuishi na utendaji, hawawezi kufundisha kwa moyo. Suala la mhadhiri kupewa nyumba au posho ya pango ni muhimu ili kumchochea afundishe vizuri na taifa lipate wataalamu waliobobea na si waliohitimu alimradi wamepata cheti ama shada zisizo na viwango.

  Kwa maana hiyo, hata kama haijatangazwa rasmi juu ya mgomo wao ni tahadhari kwa serikali hivyo inatakiwa kuchukua hatua mapema, ikiwemo kuchunguza ukweli wa madai yao na kuyapatia ufumbuzi haraka badala ya kungoja mpaka wasimamishe masomo.

  Lakini jambo la kushangaza, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe alipoulizwa kuhusiana na fununu za mgogoro huo, alimhoji mwandishi kama amewasiliana na wakuu wa vyuo! Hivi kama waziri wa elimu hakustahili kulizungumiza hilo? Tunadhani kwamba, hata kama hakuwa na taarifa alitakuwa kueleza bayana kuwa hajui na atalifanyia kazi kwa sababu liko chini ya wizara yake.

  Ni muhimu kwa serikali kuwa makini na suala hilo kwani wakigoma itakuwa kazi kubwa kulitatua na tayari mafunzo kwa vijana wetu yatavurugwa.

  Katika nchi yetu kuna tatizo la watu waliopewa madaraka kutochukua hatua mapema hata kwa mambo nyeti kama hayo, kisha kulazimika kutumia nguvu nyingi kuyapatia ufumbuzi, hatua ambayo husababisha usumbufu kwa wahusika na hasara kwa taifa.

  Inashanga kuona kuwa serikali ambayo iliwaahidi wahadhiri waliokosa nyumba vyuoni kupewa posho ya kodi ya pango. Miaka mitatu ya utekelezaji ni mingi, hivyo kukaa kimya kwake kunaweza kutafsiriwa kwamba imeghaili kuwalipa.

  Kwa sababu hiyo basi, tunaishauri serikali kwamba, ili kuepuka fedheha ichukue hatua za haraka kufuatilia suala hilo kabla halijalipuka, ikiwa ni pamoja na kuwalipa posho zao zote. Kama uwezo ni mdogo wakutane na kujadiliana nao namna ya kuwalipa na maamuzi yatakayofikiwa yatekelezwe kikamilifu.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Serikali ipige mnada 50% ya mashangingi ili kulipa hawa waalimu!
   
Loading...