Serikali isipoingilia kati sakata la uagizaji mafuta hali itakua Mbaya sana mbeleni

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
5,211
4,170
Asalaam ndugu zangu Watanzania. Nimeona nililete mbele yenu jambo hili ili tupaze sauti zetu kwa Serikali iweze kuingilia kati jambo hili.

Nimesoma kwenye gazeti kwamba makampuni yanayo agiza mafuta yameshindwa kuagiza mafuta kwa sababu za kukosa Dola.

Jambo hili limenishitua sana. Nikawaza kama wameshindwa kuagiza mafuta na Serikali ikashindwa kuingilia kati, athari yake itakuaje kwa Wananchi?

Madhara yake yatakua makubwa sana na kupelekea ugumu wa maisha kupindukia.

Sote tunajua nishati ya Mafuta yanagusa moja kwa moja maisha ya kila Mtanzani hivyo Mfumuko wa bei Utakuwa Mkubwa sana kwenye kila sekta hasa ya Usafirishaji.

Ni wito wangu kwa Serikali ni vyema jambo hili ikalichukulia kwa umuhimu sana bila kulifumbia macho maana kama halitachukuliwa kwa umuhimu basi tutegemee maumivu makubwa sana kwa Wananchi.
 
Back
Top Bottom