Serikali ipige marufuku vilabu kuwa na matawi.

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,709
Reaction score
1,735
Nakumbuka kwenye miaka ya sabini serikali ilipiga marufuku vilabu (hasa Simba na Yanga) kuwa na matawi, lakini hivi sasa naona kasi ya uundwaji ikijitokeza kana kwamba ni vyama vya siasa. Wito wangu kwa serikali ipige marufuku na kuruhusu viwe na vikundi vya mashabiki tu ( fan groups/clubs) si matawi.
 
Hoja ya muhimu, maana matawi yanafanya watu waache kufikiria kuendeleza timu za huko waliko na kuwa watumwa wa Timu mbili za darisalama. Pengine haya matawi ndio huwezesha mazingira ya kuuzwa mechi kwa timu za mikoani maana nao ni wadau wa hizo timu.
 
Hongera mkuu kwa kuliona hili na wewe, maana utakuta viongozi wa vilabu wanashindwa uongozi lakini wanayatumia matawi kuwabeba. Masuala ya matawi viachiwe vyama vya siasa tu.
 
matawi yakipigwa marufuku simba ndio watakuwa waathirika wakubwa sana na uamuzi huo kwasababu simba ina matawi kibao nakumbuka mwaka juzi simba walichukua ubingwa bila ya kupoteza mechi hata moja lakini katika hizo points nusu yake ilitoka kwa manyema rangers, azam fc, costal union, ashant fc, moro united, majimaji ya songea, twiga sports, mtwiba sugar, African Lion ambazo zote hizi ni branch za simba sports. Binafsi huwa sioni mantiki ya simba kucheza na Azam fc, ni kama kufanya mazoezi tu kwasababu nani asiejua kuwa Bakharesa alikuwa simba kama kiongozi akaenda kuanzisha azam, rage alikuwa kiongozi wa moro united kabla ya kurudi simba
 
Sidhani kama vilabu hivi ni matawi ila nilichokua namaanisha ni matawi ya WANACHAMA nchi nzima mkuu.
 
Back
Top Bottom