comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Ninavyoona ingekua ni bora serikali sasa ikaandaa hati ya dharura ya mabadiliko ya sheria na mikataba ya madini nchini ijadiliwe bungeni haraka kwa hati ya dharura, Aidha, tokea ripoti ya mchanga wa madini (makinika) itolewe hadharani kumekua na mijadala ya kisheria juu ya hatima ya ripoti hiyo kati ya kampuni ya Accacia na serikali, kwa kuwa kampuni ya Accacia Gold Mine yenye migodi ya bulyankhulu na Buzwagi imeikataa ripoti ya makinika hivyo basi kuna uwezekano mkubwa sana masuala ya sheria na mikataba ya kimataifa juu uwekezaji zikaguswa hapo ni bora tujihami mapema ukifikiria accacia ina ushawishi mkubwa duniani kutokana na uwepo wa watu maarufu sana na wenye ushawishi duniani katika kampuni hiyo.