Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,938
Bei ya daladala kwa safari fupi jijini Dar es salaam ni Sh.400 na ndefu 600-750 na ndefu zaidi sh.1000 kama sijakosea.
Bei hii ilipangwa wakati mafuta yakiuzwa chini ya 2000 Tshs. Sasa bei imekuwa juu lakini bei bado ni ileile na ikumbukwe kuwa wamiliki wa daladala ni wafanya biashara ambao wanataka kupata faida na si kutoa huduma tu.
Najua wananchi wataumia ila biashara yoyote duniani lazima bei ziendane na gharama za uendeshaji.
Waumiaji wakubwa ni makondakta na madereva maana boss yeye anachohitaji ni hesabu yake tu suala la mafuta halimuhusu.
Viongozi wanakaa kimya maana wanaogopa kushuka thamani ya kisiasa ila lazima wajue kuwa kuna watu wanaumia.
Hata dukani bidhaa hupanda na kushuka kulingana na gharama za manunuzi(uendeshaji).