Serikali Iongeze Juhudi Kujenga barabara Mpya Jiji la Dar. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali Iongeze Juhudi Kujenga barabara Mpya Jiji la Dar.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Math2009, Oct 30, 2009.

 1. M

  Math2009 Member

  #1
  Oct 30, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 11
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Kuna Mwana JM hapa ameelezea kero yake ya msongamano wa magari jiji la
  Dar es salaam,ni kweli hii ni kutokana kwamba Dar es salaam hakuna Barabara.hizo zilizopo ni kama za kwenda ******.Mimi sasa hivi niko hapa Addis Ababa, Ethiopia kwa masomo, watanzania wengi wakija hapa wanapigwa butwaa..maendeleo ya haraka ya nchi hii ndio yaliyonifanya mpaka nikarukia Jamiiforum.nchi hii sasa hivi ina barabara za juu sio chini ya kumi,na barabara zake zote za jiji minimum ni njia tatu,matatu yakwenda matatu yanarudi.sehemu nyingine ni njia nane manne yakwenda manne yanarudi,na sasa hivi wana Afica's largest comfusion flyover ever built.Serikali imeweka juhudi kwenye ujenzi wa barabara,bila barabara hakuna maendeleo..Tanzania kuna nini?viongozi wengi mnaenda nje ya nchi mbona hamjifunzi?Nimesikia kuna wahisani wengi wamejitokeza kujenga barabara kwa gharama zao zote,lakini wamekataliwa heti kwa sababu baadhi ya viongozi wanataka nao hapo wapate chochote,lakini wahisani hao hawako tayari kwasababu hiyo ni misaada ambayo nchi zilizo endelea zinatoa kwa nchi zinazoendelea,ndio hao wengi wao wako hapa Addi Ababa,kwasababu serikali ya hapa rushwa ni vita vikali sana.tena na tena naomba serikali iongeze juhudi kwenye ujenzi wa barabara mpya
   
 2. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Math2009,

  Yako ni sauti ya mtu aliaye nyikani. Serikali yetu haina nia ya kujenga nchi kama ilivyo serikali ya Ethiopia. Ya kwetu inakusanya fedha nyingi za kodi, lakini inaacha viongozi wazichote karibu zote. Baadhi yake zinatumika baadaye kuwahongeni muwachague tena.

  Dar kuna barabara zinajengwa kama njia za waenda kwa miguu. Mfano ni barabara inayotoka Msasani kwa Mwalimu kupitia maji machafu hadi Barabara ya Ali Hasan Mwinyi. Nyingine inatoka Masaki hadi Namanga. Hizi "zimejengwa" juzi juzi, lakini hazitoshi hata kupishana baisikeli mbili.

  Hatutabadilika mpaka tutakapobadilisha viongozi.
   
Loading...