Very weird way of planning for a country. Fine kuwa sehemu ya chanzo cha mapato ya nchi, ina maana wananchi wanaofanya makosa wakireform kutakuwa na nakisi katika makadirio ya matumizi.
Ikiwa hivyo ina maana mapolisi wataanza kushika innocent people ili kupunguza hiyo nakisi na kama hiyo itatokea basi tutakuwa tunavunja rule of law.
Labda, tuangalie upande mwingine. Inakuaje kama huridhiki na notification iliyotolewa, je utakuwa na haki ya kukata rufaa? Maana hali ilivyo sasa polisi anaanza kuchukua leseni halafu anmachukua kadi ya gari na baadae ndio anakubook kwa kosa.
Katika mazingara haya upende usipende utalipa notification na hutarudishiwa vitu vilivyochukuliwa mpaka ulipe notification.