Pamoja na Serikali kutangaza vita na madereva wazembe lakini ninahakika kuwa hiyo vita hawawezi kushinda maana vyombo vinavyosimamia usalama barabarani vinaudhaifu mkubwa katika suala zima la kusimamia sheria ya usalama barabarani.
Tabia ya kuendekeza rushwa na mpango mbaya wa kazi kwa kiasi kikubwa ndiyo huchangia madereva kutojali. Baadhi wa Askari wa kikosi cha usalama barabarani hutumia nafasi yao hiyo ya kazi ili kuomba rushwa na kuneemeka. Hivyo bila kutafuta muarobaini wa askari hao itakuwa ni maneno tu ya kujazia vifungu kwenye bajeti ila hakuna kitakachobadirika. madereva wanauhakika kuwa hata wakivunja sheria hakuna baya litakalowapata labda dereva atake mwenyewe hivyo mzee Mkulo tuimbie wimbo mwingine huo ushaimbwa sana kuendelea kurudia ni kupoteza muda.