Serikali inawadhihaki wafanyakazi!

Serikali inawadhihaki wafanyakazi!

Pesa nyingi zinaishia kwa wanasiasa,kama hili Bunge maalum la katiba kazi yake kubwa ilikuwa kutengeneza matusi na mipasho tu na mwisho wa siku wanaondoka na 300K,za bila kutoa jasho.

I wish JK angeliona hili hizo pesa akawaongeza walimu kuliko hawa jamaa wenye misamiati ya matusi na mipasho.

hao nguruwe pori waliorundikana dodoma ndio waliokula mihogo yote hadi wamesababisha nguruwe wadogo tufe njaa.

bunge la nyani.jpg
 
Mtoa mada suala la mshahara kwa watumish ni kweli changamoto na pia kodi ya serikal ndo majanga kabisaaa,lakin me nataka niweke sawa kumbukumbu kwa wengine,mshahara wa mwalim wa shahada si 300,000/= ni 589,000/=,pia hapa kuna dhana kuwa natural resourdes zinaendeleza nchi,jaman kuna nchu hazina natural resources na zimeendelea,nchi ili ipige hatua inapaswa kuwekeza kwenye human development,kutoa elim boraa kwa kila mtu anayestahili hapo ndo tutaendelea si hivi tunavyofikiria,je Japan ina rasilimali gani????na imeendelea,

mkuu, mimi naongelea mishahara ya walimu, sio watumishi wengine, kama unavyotaka kusema hapa. kumbuka kwamba walimu ndio tunalimpwa mshahara wa chini kabisa ktk nchi hii.
 
Lakini wenzetu makada wa chama chetu hawatuelewi!Naomba Mungu siku moja watuelewe tunaongea nini?
Nilisikiliza clip ya Prof.Tibaijuka ya kuhusu serikali mbili ati Tanzania ni masikini sana mpaka UN wanajua hilo,na yeye kama Prof.wauchumi,nilitamani ningepata nafasi nimuulize kama ameitendea haki elimu yake, na kigezo kipi kinachoifanya Tanzania iwe masikini.Nchi yenye asali na maziwa.

Tanzania tu matajiri mno,na hili wazungu na wale wanaitwa wawekezaji wanalijua,na wanajua viongozi wetu pamoja na shule waliyokwenda wanakubali kupewa SHANGA na VYANDARUA na kutoa RASLIMALI zetu zote,halafu wanakuja na kutuambia ati sisi masikini.

Sielewi kama ni ukiwa na elimu kubwa unakuwa mjinga sijui,labda tatizo ni hii shule ya kuunga unga niliyonayo.Serikali na viongozi wake wako busy na CDM na UKAWA na kuwaacha wengine wakiondoka na mali za nchi na kuwachekea eti hawa ni wenzetu.

muda ukifika wataelewa tu. sasa hv wanajifanya kuziba nta masikioni na kuvaa miwani ya mbao!
 
Ndugu ukisubiria Msanii akuongezee mshahara utasubiri sana...Mie apa na zaidi ya wiki sijaenda kazini nipo mji mwingine full ujasiriamali nikirudi kazini nafanya wiki moja then naandaa mlolongo wa excuse mpaka Boss wangu alishakoma na Mimi alijaribu kunimaindi nikamwambia wewe una majumba ya kisasa zaidi ya moja mwenzio bado napanga nikampigia mahesabu ya mshahara wangu akaona kua ata tukutuku tu kumiliki ni shida mwisho kw mpole...so fanya kazi kulingana na kamshahara unakoliwa

mkuu, hii ndio njia ya pekee iliyobaki. inabidi tugawanye muda: 10% kazini & 90% ujasiriamalini. no way!
 
hao nguruwe pori waliorundikana dodoma ndio waliokula mihogo yote hadi wamesababisha nguruwe wadogo tufe njaa.

Kaka,hasira ya nini tena wangu?Ndio inabidi tubadilike tuachane na kulalamika.Tuamke sasa kaka maana hawa nguruwe pori wakimaliza mihaogo,watatumaliza na sisi!
 
muda ukifika wataelewa tu. sasa hv wanajifanya kuziba nta masikioni na kuvaa miwani ya mbao!

Miwani waliyovaa ikifika siku kamili tutawasaidia kuivua.Na mmojawapo anayekaribia kuvua hiyo miwani ni JK,akitoka huko ndiyo atajua kama aliweka masikio nta au alivaa miwani ya jua badala ya miwani ya kuonea.
 
Kwanza nina mashaka kama ww ni mtanzania!!!!! hiyo nchi unayoishi ww ambayo mwl wa primary analipwa 1.5m yaitwaje ndg?
Pili hapo kwa red sijui unataka kuwapa walim ujumbe gani, ila kumbuka dogo zako wako shuleni hata kama ww hukubahatika lkn wao wanamwitaji huyo mwl, ama laa basi watoto wako wataenda shule pia

huyo mburula atakuwa hayupo tz. yupo majuu akihangaika kubeba maboksi.
 
Halafu inauma sana kila siku kusikia utajiri mkubwa waviongozi na watoto wao. Watoto wa wakubwa ndio wanarithishwa madaraka na utamu wa nchi hii. Nawasikitikia sana wafanyakazi wanaobeba mabango kila Mei mosi wakililia nyongeza za mshahara. There must be a revolution in this country
 
mkuu, mimi naongelea mishahara ya walimu, sio watumishi wengine, kama unavyotaka kusema hapa. kumbuka kwamba walimu ndio tunalimpwa mshahara wa chini kabisa ktk nchi hii.

tpaul samahan wewe ni mwalimu wa shahada,stashahada au ngazi ya cheti???what i know mwalim wa shahada (degree) analipwa tsh 589,000/= kabla ya makato,sasa pia nakukumbusha tu kuwa mwalim wa degree analipwa mshahara mkubwa kuliko afsa utumish wa manispaa,,,,/halmashauri,,,,
any way mshahara ni mdogo,ila usipotoshe,walim mshahara wao si laki 3 kwa degree holder
 
Last edited by a moderator:
tpaul hili la ujasiriamali ndo ulipaswa kulieleza tangu mwanzo
 
Last edited by a moderator:
tpaul samahan wewe ni mwalimu wa shahada,stashahada au ngazi ya cheti???what i know mwalim wa shahada (degree) analipwa tsh 589,000/= kabla ya makato,sasa pia nakukumbusha tu kuwa mwalim wa degree analipwa mshahara mkubwa kuliko afsa utumish wa manispaa,,,,/halmashauri,,,,
any way mshahara ni mdogo,ila usipotoshe,walim mshahara wao si laki 3 kwa degree holder

Kwani wewe Mkoroshokigolini mwalimu? Mimi ndiye mwalimu, tena degree holder, ninajua pesa ninazolipwa...mbona unataka kupotosha watu? Walimu ndio wanaolipwa mshahara wa chini zaidi katika nchi hii, wakifuatia na polisi, magereza, watarishi na janitors. Kwanini hutaki kuelewa? Walimu ni kada muhimu sana katika nchi hii lakini ni watumishi wanaodharauliwa sana na serikali, na hata raia wa kawaida. Ni lini hasa heshima ya mwalimu itapanda?
 
Last edited by a moderator:
Kaka,hasira ya nini tena wangu?Ndio inabidi tubadilike tuachane na kulalamika.Tuamke sasa kaka maana hawa nguruwe pori wakimaliza mihaogo,watatumaliza na sisi!

Tetty unajua hawa watu wanatia hasira sana? Hawa wezi wanatakiwa wafahamu kwamba watanzania wa leo ni werevu sana--hawawezi kutufananisha na wale wa mwaka 1947! Ipo siku hawa nguruwe pori watalia na kusaga meno yao marefu na yenye ncha kali kwenye miamba ya mawe. Kuna siku yaja, na haiko mbali sana, wewe subiri kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Mleta uzi unahoja ya msingi sana, mimi ni mwalimu mwenye shahada mshahara ulio uandika kwamba nalipwa chini ya laki tatu si kweli. Ni 589,000=. Jitahidi uwe unaandika taarifa sahihi ili usipotoshe umma. Kweli pesa tunayolipwa walimu ni kidogo ukilinganisha na kazi au umuhimu wetu katika maendeleo ya nchi hii na dunia kwa ujumla. Serikali iongeze japo kwa 50% ya mshahara uliopo kuweka mambo sawa.
 
Tetty unajua hawa watu wanatia hasira sana? Hawa wezi wanatakiwa wafahamu kwamba watanzania wa leo ni werevu sana--hawawezi kutufananisha na wale wa mwaka 1947! Ipo siku hawa nguruwe pori watalia na kusaga meno yao marefu na yenye ncha kali kwenye miamba ya mawe. Kuna siku yaja, na haiko mbali sana, wewe subiri kidogo.

Bado hatujawaonyesha kuwa waTanzania wa leo siyo wale wa mwaka 1964 au 1947,tunatakiwa tuwaonyeshe hivyo.Tunatakiwa tukerwe na tabia zao hasa za kutugawa,maana kwa kutugawa wanafaidika zaidi.

Na tungeweza kuwaonyesha tumebadilika kwa kuungana na kuwa wamoja kuwaeleza either kwa kwenda mahakamani au kupitia kalamu za waandishi kwamba kwa kweli tumechoshwa.

Nimemsikiliza Nape hana alichoongea zaidi ya matusi na kuongeza mfarakano kwenye jamii.Hivi ukivunja marithiano Zanzibar unatafuta nini zaidi ya vurugu?Hivi wale waliouawa Zanzibar hawatoshi tunataka kuongeza?Kama CCM hawakutaka Katiba mpya why bother?Waache tuendelee na ile ile ya wakati ule ule Rais mwenye uwoga wa Mungu atatengeneza ya Matakwa ya Watanzania.Ila inasikitisha sana.!
 
tpaul samahan wewe ni mwalimu wa shahada,stashahada au ngazi ya cheti???what i know mwalim wa shahada (degree) analipwa tsh 589,000/= kabla ya makato,sasa pia nakukumbusha tu kuwa mwalim wa degree analipwa mshahara mkubwa kuliko afsa utumish wa manispaa,,,,/halmashauri,,,,
any way mshahara ni mdogo,ila usipotoshe,walim mshahara wao si laki 3 kwa degree holder
Wewe ndo unapotosha watu mdau tpaul, inawezekana unapunjwa mshahara na hujui, a degree holder anapokea Tsh 589,000/= kabla ya makato,na wakimkata ni kama 473,000=Halafu wale maafsa watumishi ni kwamba wanapatia pesa kwenye viposhoposho,usijinyongeshe eti kwakua wewe ni mwalim,panga bajet zako fresh kwanza then uanze kulalama kuwa mshahara wako ni mdogo,ukisema kuwa una mshahara wa laki 3 ni kwamba unaibiwa,kama mimi nadanganya basi aje mwalim mwenye degree aseme mshahara wake unaanzia na shilingi nangapi?Kingine kama wewe ni degree holder huna sababu ya kulalama kuhusu mshahara,siamini kama chuoni ulisomea masomo ya ualimu tu,Ualim ni zaid ya kfundisha,jitahid kutumia elimu uliyopewa kufanya mambo beyond ualim
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom