Serikali inawadhihaki wafanyakazi!

Serikali inawadhihaki wafanyakazi!

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
26,021
Reaction score
25,417
Katika biblia hakuna kosa lililo dogo wala kubwa kuliko lingine. Makosa yote ni sawa mbele za Mungu. Jambazi, mchawi, fisadi, kibaka na mzinzi, wote watapata hukumu iliyo sawa sawa. Dhana hii ni tofauti na jinsi tunavyoichukulia hapa duniani ambapo kila mtu huadhibiwa kulingana na uzito wa kosa alilotenda.

Kosa kubwa kuliko yote hapa Tanganyika ni kuendelea kuikumbatia serikali dhaifu na ya kifisadi inayoongozwa na CCM. Serikali hii ‘sikivu’ imeshindwa kabisa kuboresha maisha ya wafanyakazi katika nchi hii. Kila mwaka tunaambiwa serikali haina fedha huku tukishuhudia ufisadi wa kutisha, matanuzi ya kipuuzi ya viongozi wa serikali, kulipana posho kubwa kubwa, misamaha ya kodi, ufisadi na maovu mengine kama haya yakitendwa na serikali ya CCM kila kukicha. Yote haya yanafanyika kwa gharama za wananchi na mwisho wa siku wananchi wameendelea kuishi maisha ya kusikitisha wakati nchi ikiwa imebarikiwa kuwa na rasimali kedekede kama vile almasi, misitu, tembo, twiga, dhahabu, tanzanite na utajiri mwingine chekwa!

Kitendo cha serikali ya CCM kugoma kuongeza mishahara ya watumishi kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 ni uhaini, ugaidi na uuaji ambao haukubaliki hata kidogo. Watumishi wa umma wamekuwa wakiishi kama yatima katika nchi hii huku kikundi kidogo cha mafisadi wasiozidi 50 wakiendelea kutumbua rasimali za taifa na kuishi kama vile wako peponi. Ni lini hasa serikali hii ya kijangili itaacha kuwadharau, kuwanyonya na kuwaonea wafanyakazi katika nchi hii kwa kuthamini mchango wao katika maendeleo ya taifa?

Mwaka wa jana tumeshuhudia serikali hii ikigoma kupunguza kodi ya mishahara na badala yake ikapunguza kwa 1% tu, kiwango ambacho ni sawa na bure. Tumeshuhudia wajumbe wa Bunge Maalum la Matusi (BMM) wakilipwa mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kutukana tu na kazi hiyo ya kutukana wameifanya kwa muda mrefu hadi imebidi waongezwe muda mwingine wa kuendelea kutukana na kukejeli maoni ya wananchi. Pesa kama hizi zinazopotea bila sababu ya msingi, zingepaswa zitumike kuboresha mishahara ya walimu. Walimu tumekuwa tukiishi kama wakimbizi. Huwezi kuamini kwamba mshahara wa mwalimu mwenye shahada hauzidi Tsh 300,000 kwa mwezi. Kila mtu ni shahidi kwamba wajumbe watukanaji wa bunge la katiba wanalipwa zaidi ya kiasi hicho cha pesa kwa siku wakati mwalimu anayeeelimisha taifa hulipwa chini ya kiwango hicho kwa mwezi na wakati mwingine kukaa zaidi ya miezi 6 bila kulipwa mshahara. Jamani, usawa wa binadamu upo wapi katika nchi hii?

Natoa wito kwa wafanyakazi wote, hasa walimu, kujitahidi kuwahi kufika kazini. Mkifika kazini tieni saini kwenye vitabu vya mahudhurio, kisha endeleeni kupiga soga mpaka muda wa kazi unapoisha mrudi majumbani kwenu. Ndio. Hatuwezi kila siku tuwe t--------- na mafisadi kama ngazi ya kupandia na kuning’inia madarakani huku sisi tukiendelea kuishi maisha ya dhiki. Ifike wakati walimu tujitambue na tukatae kunyonywa na mafisadi ilhali tunao uwezo wa kukataa unyonyaji huu. Mkakati huu wa kutofundisha utasaidia kuzalisha wajinga na wajinga wakishakuwa wengi itakuwa sio rahisi kutawalika. Hapo ndipo sasa wafanyakazi tutakapoanza kuthaminiwa. Malipo yetu yataboreshwa na tutakuwa hatucheleweshewi mishahara. Ule utaratibu wa kufundisha chini ya kiwango umeonekana kwamba haulipi tena. Kufundisha chini ya kiwango huzalisha watu wenye elimu nusu ambao ni rahisi kutawalika. Ni bora sasa tuanze mapango mpya (BRN) wa kutokufundisha kabisa na tuzalishe vilaza halisi wasiotawalika ili tuheshimiane.

SOLIDARITY FOR EVER!
:yield:

CCM wataiua nchi.jpg

fisadi.jpg

huduma safi.jpg

bonge ya shule.jpg

huduma bora.jpg

darasa chini ya muti.jpg
 
attachment.php

Duh! Kazi kweli kweli! Haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania!!!!
 
attachment.php

Habari ndo hiyo! Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya ya ufukara!
 
^^
Uko sahihi kabisa, Upande wa pili wa shilingi hata sie wananchi tuna matarajio yanayopindukia kwa wanasiasa. Nakumbuka in early 1980s wafanyakazi hawakuruhusiwa kuwa na pato zaidi ya ajira zao, leo hii ni tofauti, unaweza kuwa mtumishi mjasiriamali kuliko kuhesabu tarehe za mshahara au kupandishiwa mshahara huku bei zikipanda kuliko thamani ya mshahara uliopewa.
Politicians are not always friends of truth

Umenena vizuri sana mkuu wangu. Sasa kilichopo ni kusaini kwenye madaftari ya mahudhurio na kurejea mashambani kulima au kufanya ujasiriamali. Wafanyakazi hatukubali kunyonywa tena. Serikali haina nia njema na ustawi wa wafanyakazi. Hatujawahi kusikia waziri au mbunge kacheleweshewa mshahara. Kwanini walimu tu ndio mishahara yetu ichelewe, licha ya kwamba mishahara yenyewe ni duni sana?
Unyonge sasa baasi!
 
Mbona huo utaratibu wa kusaini na kisha kupiga story ulisha anza.Walimu serikali inatuchukulia kama maboya lkn wajue walimu wa ss wa digital.Mwaka ujao wa serikali rais alivyoahidi asipo tekeleza bc ufauli utazidi kushika!!
 
Pesa nyingi zinaishia kwa wanasiasa,kama hili Bunge maalum la katiba kazi yake kubwa ilikuwa kutengeneza matusi na mipasho tu na mwisho wa siku wanaondoka na 300K,za bila kutoa jasho.

I wish JK angeliona hili hizo pesa akawaongeza walimu kuliko hawa jamaa wenye misamiati ya matusi na mipasho.
 
Katika biblia hakuna kosa lililo dogo wala kubwa kuliko lingine. Makosa yote ni sawa mbele za Mungu. Jambazi, mchawi, fisadi, kibaka na mzinzi, wote watapata hukumu iliyo sawa sawa. Dhana hii ni tofauti na jinsi tunavyoichukulia hapa duniani ambapo kila mtu huadhibiwa kulingana na uzito wa kosa alilotenda.

Kosa kubwa kuliko yote hapa Tanganyika ni kuendelea kuikumbatia serikali dhaifu na ya kifisadi inayoongozwa na CCM. Serikali hii ‘sikivu' imeshindwa kabisa kuboresha maisha ya wafanyakazi katika nchi hii. Kila mwaka tunaambiwa serikali haina fedha huku tukishuhudia ufisadi wa kutisha, matanuzi ya kipuuzi ya viongozi wa serikali, kulipana posho kubwa kubwa, misamaha ya kodi, ufisadi na maovu mengine kama haya yakitendwa na serikali ya CCM kila kukicha. Yote haya yanafanyika kwa gharama za wananchi na mwisho wa siku wananchi wameendelea kuishi maisha ya kusikitisha wakati nchi ikiwa imebarikiwa kuwa na rasimali kedekede kama vile almasi, misitu, tembo, twiga, dhahabu, tanzanite na utajiri mwingine chekwa!

Kitendo cha serikali ya CCM kugoma kuongeza mishahara ya watumishi kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 ni uhaini, ugaidi na uuaji ambao haukubaliki hata kidogo. Watumishi wa umma wamekuwa wakiishi kama yatima katika nchi hii huku kikundi kidogo cha mafisadi wasiozidi 50 wakiendelea kutumbua rasimali za taifa na kuishi kama vile wako peponi. Ni lini hasa serikali hii ya kijangili itaacha kuwadharau, kuwanyonya na kuwaonea wafanyakazi katika nchi hii kwa kuthamini mchango wao katika maendeleo ya taifa?

Mwaka wa jana tumeshuhudia serikali hii ikigoma kupunguza kodi ya mishahara na badala yake ikapunguza kwa 1% tu, kiwango ambacho ni sawa na bure. Tumeshuhudia wajumbe wa Bunge Maalum la Matusi (BMM) wakilipwa mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kutukana tu na kazi hiyo ya kutukana wameifanya kwa muda mrefu hadi imebidi waongezwe muda mwingine wa kuendelea kutukana na kukejeli maoni ya wananchi. Pesa kama hizi zinazopotea bila sababu ya msingi, zingepaswa zitumike kuboresha mishahara ya walimu. Walimu tumekuwa tukiishi kama wakimbizi. Huwezi kuamini kwamba mshahara wa mwalimu mwenye shahada hauzidi Tsh 300,000 kwa mwezi. Kila mtu ni shahidi kwamba wajumbe watukanaji wa bunge la katiba wanalipwa zaidi ya kiasi hicho cha pesa kwa siku wakati mwalimu anayeeelimisha taifa hulipwa chini ya kiwango hicho kwa mwezi na wakati mwingine kukaa zaidi ya miezi 6 bila kulipwa mshahara. Jamani, usawa wa binadamu upo wapi katika nchi hii?

Natoa wito kwa wafanyakazi wote, hasa walimu, kujitahidi kuwahi kufika kazini. Mkifika kazini tieni saini kwenye vitabu vya mahudhurio, kisha endeleeni kupiga soga mpaka muda wa kazi unapoisha mrudi majumbani kwenu. Ndio. Hatuwezi kila siku tuwe t--------- na mafisadi kama ngazi ya kupandia na kuning'inia madarakani huku sisi tukiendelea kuishi maisha ya dhiki. Ifike wakati walimu tujitambue na tukatae kunyonywa na mafisadi ilhali tunao uwezo wa kukataa unyonyaji huu. Mkakati huu wa kutofundisha utasaidia kuzalisha wajinga na wajinga wakishakuwa wengi itakuwa sio rahisi kutawalika. Hapo ndipo sasa wafanyakazi tutakapoanza kuthaminiwa. Malipo yetu yataboreshwa na tutakuwa hatucheleweshewi mishahara. Ule utaratibu wa kufundisha chini ya kiwango umeonekana kwamba haulipi tena. Kufundisha chini ya kiwango huzalisha watu wenye elimu nusu ambao ni rahisi kutawalika. Ni bora sasa tuanze mapango mpya (BRN) wa kutokufundisha kabisa na tuzalishe vilaza halisi wasiotawalika ili tuheshimiane.

SOLIDARITY FOR EVER!
:yield:

View attachment 155218

View attachment 155219

View attachment 155220

View attachment 155221

View attachment 155222

View attachment 155223
wazo ulilolitoa ndio mtaji wa serikali ya ccm,dawa halisi ni kuhamasisha wafanyakazi wote kuinyima kura ccm 2015 hiyo ndio kiboko halisi kwa serikali ya ccm
 
Ebu acheni unafiki mmelazimishwa Kuwa walimu? Mbona kuna walimu tena wa primary wanalipwa zaidi ya 1.5mill? Kwanini mnaasume walimu wote wanalipwa 300,000? Jeendelezeni mpande vyeo au tafuteni kazi zingine zinazolipa lkn kuchukua mshahara bila kazi ni Zambi kubwa zaidi ya ufisadi. Kumbukeni mkataba wa ajira ni voluntary sio lazima uamuzi mnao wemyewe acheni uhuni hautawasaidia
 
Mtoa mada suala la mshahara kwa watumish ni kweli changamoto na pia kodi ya serikal ndo majanga kabisaaa,lakin me nataka niweke sawa kumbukumbu kwa wengine,mshahara wa mwalim wa shahada si 300,000/= ni 589,000/=,pia hapa kuna dhana kuwa natural resourdes zinaendeleza nchi,jaman kuna nchu hazina natural resources na zimeendelea,nchi ili ipige hatua inapaswa kuwekeza kwenye human development,kutoa elim boraa kwa kila mtu anayestahili hapo ndo tutaendelea si hivi tunavyofikiria,je Japan ina rasilimali gani????na imeendelea,
 
Pesa nyingi zinaishia kwa wanasiasa,kama hili Bunge maalum la katiba kazi yake kubwa ilikuwa kutengeneza matusi na mipasho tu na mwisho wa siku wanaondoka na 300K,za bila kutoa jasho.

I wish JK angeliona hili hizo pesa akawaongeza walimu kuliko hawa jamaa wenye misamiati ya matusi na mipasho.

Tetty hili ndo la ukwel,kada inayotafuna pesa hapa Tanzania ni Politician
 
Last edited by a moderator:
Tetty hili ndo la ukwel,kada inayotafuna pesa hapa Tanzania ni Politician

Lakini wenzetu makada wa chama chetu hawatuelewi!Naomba Mungu siku moja watuelewe tunaongea nini?
Nilisikiliza clip ya Prof.Tibaijuka ya kuhusu serikali mbili ati Tanzania ni masikini sana mpaka UN wanajua hilo,na yeye kama Prof.wauchumi,nilitamani ningepata nafasi nimuulize kama ameitendea haki elimu yake, na kigezo kipi kinachoifanya Tanzania iwe masikini.Nchi yenye asali na maziwa.

Tanzania tu matajiri mno,na hili wazungu na wale wanaitwa wawekezaji wanalijua,na wanajua viongozi wetu pamoja na shule waliyokwenda wanakubali kupewa SHANGA na VYANDARUA na kutoa RASLIMALI zetu zote,halafu wanakuja na kutuambia ati sisi masikini.

Sielewi kama ni ukiwa na elimu kubwa unakuwa mjinga sijui,labda tatizo ni hii shule ya kuunga unga niliyonayo.Serikali na viongozi wake wako busy na CDM na UKAWA na kuwaacha wengine wakiondoka na mali za nchi na kuwachekea eti hawa ni wenzetu.
 
daaah,aisee mkoloni anayetutawala ni katili kuliko mjeremani
 
Ndugu ukisubiria Msanii akuongezee mshahara utasubiri sana...Mie apa na zaidi ya wiki sijaenda kazini nipo mji mwingine full ujasiriamali nikirudi kazini nafanya wiki moja then naandaa mlolongo wa excuse mpaka Boss wangu alishakoma na Mimi alijaribu kunimaindi nikamwambia wewe una majumba ya kisasa zaidi ya moja mwenzio bado napanga nikampigia mahesabu ya mshahara wangu akaona kua ata tukutuku tu kumiliki ni shida mwisho kw mpole...so fanya kazi kulingana na kamshahara unakoliwa
 
Ebu acheni unafiki mmelazimishwa Kuwa walimu? Mbona kuna walimu tena wa primary wanalipwa zaidi ya 1.5mill? Kwanini mnaasume walimu wote wanalipwa 300,000? Jeendelezeni mpande vyeo au tafuteni kazi zingine zinazolipa lkn kuchukua mshahara bila kazi ni Zambi kubwa zaidi ya ufisadi. Kumbukeni mkataba wa ajira ni voluntary sio lazima uamuzi mnao wemyewe acheni uhuni hautawasaidia

Uko timamu kweli wewe?
 
Kwanza nina mashaka kama ww ni mtanzania!!!!! hiyo nchi unayoishi ww ambayo mwl wa primary analipwa 1.5m yaitwaje ndg?
Pili hapo kwa red sijui unataka kuwapa walim ujumbe gani, ila kumbuka dogo zako wako shuleni hata kama ww hukubahatika lkn wao wanamwitaji huyo mwl, ama laa basi watoto wako wataenda shule pia
 
Back
Top Bottom