Serikali inatumia gharama kubwa sekta ya elimu

Serikali inatumia gharama kubwa sekta ya elimu

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
Na Mwandishi wetu, Mihambwe

Serikali ya awamu ya tano (5) iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli inatumia fedha nyingi katika kuhakikisha elimu bure na bora inapatikana hivyo ni wajibu wa kila Mdau kuheshimu na kuwa makini nayo.

Hayo yamesemwa na Afisa Tarafa Mihambwe, Gavana Emmanuel Shilatu wakati alipotembelea Shule ya Msingi ya Mitumbati iliyopo Kijiji cha Kisagani kata ya Mihambwe ili kujionea mwenendo wa kitaaluma shuleni hapo.

"Kila mwezi Serikali hutumia zaidi ta Tsh. Bilioni 23.77 kutoa elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka sekondari. Hapo hatujajumlisha mishahara ya Waalimu, haujaweka Mabilioni yanayotumika kutoa mikopo elimu ya juu. Kila mmoja ambaye ni Mdau wa elimu nchini ana wajibu mkubwa kuhakikisha elimu bora na yenye tija inapatikana. Ewe Mwalimu una wajibu wa kuhakikisha unazingatia nidhamu, uadilifu na uwajibikaji kazini." alisema Gavana Shilatu wakati akizungumza na Waalimu wa Shuleni hapo.

Gavana Shilatu alizidi kusisitiza Mwalimu Mkuu na Mratibu Elimu Kata kusimamia vyema taaluma ili kuboresha ufaulu.

"Hakuna sababu ya ufaulu upungue ama uwe mbaya wakati kila hitaji mnapatiwa na Serikali. Nawaagiza Mwalimu Mkuu na Afisa Elimu Kata msimamie vyema taaluma shuleni, sitaki kusikia habari ya kufeli feli shuleni. Simamieni taaluma, elimu ni urithi pekee na ufunguo wa maisha." alimalizia Gavana Shilatu.

Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na Mratibu elimu kata, Mwenyekiti na Mtendaji kijiji cha Kisagani na kupokelewa na mwenyeji wao Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mitumbati.
IMG_20181031_161937_893.jpg
IMG_20181031_161937_895.jpg
IMG_20181030_150445.jpg
IMG_20181030_150045.jpg
 
Mbona hajatoa ushauri kwa wazazi na jamii inayozunguka shule hiyo
 
Serikali inayotoa mabilioni ya fedha kila mwezi kwa ajili ya elimu bure lakini haijui ifanye nini ili elimu katika mashule yake iwe bora.

Kituko.
 
Hongera sana bigi up magufuli kwakuona umuhimu waelimu, tunaomba utukumbuke sisi wafanyakazi
 
Back
Top Bottom