Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,318
- 25,111
Miongoni mwa sekta ambazo zimekuwa hazifanyi vyema kwa muda mrefu ni haswa kwenye sekta ya elimu.
Sekta hii imechezewa na kukumbwa na mabadiliko ya mara kwa mara ambayo kimsingi yamekuwa hayana tija kubwa.
Shule binafsi ni miongoni mwa shule ambazo zimekuwa zikifanya vyema hasa kutokana na uwekezaji na mikakati iliyojiwekea katika kutoa elimu.
Serikali hivi sasa imejipambanua kwa sera yake ya elimu bure, jambo ambalo limesababisha idadi kubwa ya watoto kupelekwa kwenye shule za Serikali.
Hali hii imepelekea idadi kubwa sana ya wanafunzi wanaopelekwa shule binafsi kupungua kwa kiwango kikubwa sana, jambo linalotishia uhai wa shule hizi ambazo zimewekezwa kwa fedha nyingi na pia kutishia kupoteza ajira kwa walioajiriwa huko!
Mbaya zaidi ni huu ubaguzi ambao "mkubwa" ameounyesha hadharani kwenye suala la mikopo ya elimu ya juu.
Kwa kweli hii itapelekea zaidi kudidimiza shule binafsi kwani wazazi wengi hawana uwezo wa kusomesha watoto wao vyuo vikuu.
Tutarajie mwakani idadi ndogo zaidi ya wanafunzi kupelekwa shule binafsi, na hata waalimu wengi walioajiriwa huko kwenye shule binafsi kupoteza ajira zao, siyo hayo tu bali hata kufungwa kwa shule nyingi kutokana na kukosa wanafunzi na kushindwa kujiendesha.
Ikumbukwe pia zipo shule nyingine ambazo zilijengwa kwa mikopo kutoka benk, hizi nazo hazitobaki salama mnada utazipitia.
Sasa hivi kwenye kusoma namba, tupo "conic section".