Serikali inataka kuua na kuzorotesha shule binafsi?

Serikali inataka kuua na kuzorotesha shule binafsi?

WATAKUJA KUSEMA WALIYOSOMA NJE VYUO HUKO HAKUNA KUWAPA AJIRA TZ

OVA

Unaweza ukakuta Kule kwenye Secretariet ya Ajira Tayari wanapigwa kabali hawachomozi

Watakuwa wanahoji Uzalendo Wao wa kuacha Vyuo vya ndani Na kwenda kusoma Vyuo vya Mabeberu hahaha
 
Kuna anayetengeneza matabaka hivi sasa zaidi ya magfool? Acha ujuha wewe...
Shule hizi zimejikita katika kutoa elimu bora!
Private ni wezi Wa mitihani tunawalia timing tu!
 
Kuna taarifa kuwa kuanzia 2021 watakaokuwa wanapewa kipaumbele kwenye kuajiriwa katika taasisi za serikali eti ni wale waliosoma shule za serikali inasemekana rais ametoa maagizo hayo hiii ni hatariii Sana tena Sana
Wakati mwingine jitahidi kushirikisha ubongo
 
Private ni wezi Wa mitihani tunawalia timing tu!
Mbona unabwabwaja sana...mara wabaguzi, sasa wanaiba mitihani!
Wewe nenda kwenye yale mainterview yako, hapa hapakufai...
 
Kwa hyo mkulu akitoka bado hali itaendelea kuwa huvyo?mi naona tuautishane sana,akiondoka watakuja na yao na siajabu walio soma binafis watapewa kipaumbele.wewe unayemtakia mtoto Elimu bora kaza buti tu mkulu akienda sana mwisho ni 2025,atakaye kuja atakuja na grisi,hii haina miongozo kila mkulu huja na miongozo yake.rejea Kwa jk,mtoto akipata mimba baada ya kujifungua arejee school.Je?sasa hivi?
Anatuharibia generation kila mahali kavurunda...itachukua muda sana kuja kustabilize!
 
Wenye hela zao hawaangaiki na shule bure, ila kama pangu pakavu patie mchuzi huna jinsi elimu bure itakuhusu.. Mwenye uelewa na kusoma vizuri atatambua wapi ampeleke mwanae. Sidhan km shule binafsi zitakufa kisa elimu bure si kweli kwani mwanzo kayumba na binafsi ziliwahi kulingana viwango,!? Ni hapana! binafsi zilikuwa juu na wazazi walipeleka watoto wao. Kwahyo sithan km elimu bure ni tatizo, sana sana imesaidia watu wenye kipato cha chini sana
 
Shule za binafsi zinatengeneza matabaka,zife tu!
Anayetengeneza matabaka ni Magu na ushahidi upo wazi na mwenye akili timamu anaona mchana kweupe wewe kama huna uwezo wa kusomesha watoto wako katika Shule hizo usizituhumu kwa ubaya. Binafsi nilisoma shule za serikali kuanzia Std I - A' level kwa wakati huo zilikuwa na hali bora kidg lakini miaka hii hali ni mbaya zaidi kwenye Shule hizo sabb serikali imezitelekeza. Muulize Polepole Gamba mwenzio Azania tuliyosoma wote wakat ule inafanana na iliyopo leo? Ubashite mtupu umejaa kwenye matokeo ya kidato cha 4 na 6
 
Private ni wezi Wa mitihani tunawalia timing tu!
Huo ni ujinga unawaza! naomba fanya kitu kimoja nenda katembelee hata siku moja shule za Binafsi uone mazingira bora utoaji elimu yaliyopo pale kisha linganisha na shule za serikali. Tatizo Magufuri sio muwazi aache kuwahadaa watz serikali ndiyo ilisabbsha wazazi kupeleka watoto wao Shule binafsi
 
Kule kwenye shule za binafsi watoto karibia wote wanaomaliza wanakuwa na uwezo wa kutema yai. Sasa nikiona mnanikejeli mimi ninaeongea kiingereza cha kuungaunga na grammatical errors kibao lazima niwe na hasira na ninyi wazazi mnaonikejeli kila kona. Na siishii tu kwenu nyinyi wazazi bali ninawapatiliza hadi na uzao wenu ulioko huko kwenye english medium schools a.k.a. private schools. Hiyo itakuwa mwaka 2050 nikiwa madarakani.
 
Tatizo kubwa tulilo nalo sasa hivi kutokutazama mambo kwa marefu na mapana yake kabla ya kuyazungumzia au kutoa ushauri na mwisho maamuzi.
Ubaguzi wa aina yoyote katika haki za msingi za raia haukubaliki si kutendwa tu bali hata kutamkwa.
Haki ya kupewa huduma za afya, maji, barabara, elimu na zinazofanana na hizo kwa kutumia pesa za uma kwa utaratibu uliowekwa haitakiwi kubagua masikini au tajiri, mwanamke au mwanaume bali asiyetaka kuitumia haki hiyo aamue kwa hiari yake mwenyewe.
Kimsingi haki hizi zikiondolewa kwa baadhi ya watu inawapa haki nyingine ya waliobaguliwa kutolipa kodi zinazogharamia huduma hizo.
Tukumbuke kwa watanzania wote ni ndugu na Tanzania ni moja. Sera, sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayoashiria matabaka ya raia ni batili kiasili na haifai kwa mustakabali wa taifa.
 
huyu asitutishe, tutapata taabu wakati wake ila muda wake utaisha atasepa zake na wanetu wataendelea kupata mikopo, kwa sababu najua hawezi kuja mwingine mwenye tabia kama za jiwe hili.
 
Tatizo kubwa tulilo nalo sasa hivi kutokutazama mambo kwa marefu na mapana yake kabla ya kuyazungumzia au kutoa ushauri na mwisho maamuzi.
Ubaguzi wa aina yoyote katika haki za msingi za raia haukubaliki si kutendwa tu bali hata kutamkwa.
Haki ya kupewa huduma za afya, maji, barabara, elimu na zinazofanana na hizo kwa kutumia pesa za uma kwa utaratibu uliowekwa haitakiwi kubagua masikini au tajiri, mwanamke au mwanaume bali asiyetaka kuitumia haki hiyo aamue kwa hiari yake mwenyewe.
Kimsingi haki hizi zikiondolewa kwa baadhi ya watu inawapa haki nyingine ya waliobaguliwa kutolipa kodi zinazogharamia huduma hizo.
Tukumbuke kwa watanzania wote ni ndugu na Tanzania ni moja. Sera, sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayoashiria matabaka ya raia ni batili kiasili na haifai kwa mustakabali wa taifa.
umeongea vema sn mkuu
 
tajiri anapenda kunyonya maskini ana chuki na wivu pamoja ma unyonyaji wa tajiri lakini umaweza kuwa tajiri kwa kushirikiana na tajiri kwa maskini hata ukishirikiana naye ni UMASKINI kwa kwenda mbele
 
Issue ni hive, mtoto wako mpe elimu bora na sio bora elimu. Wanatudanganya hapa watoto wao wasome shule nzuri halafu waje wawe maneja wa watoto wetu. Akili ya kupewa changanya na ya kwako.
 
Back
Top Bottom