Serikali inapokosoa serikali, wananchi waende wapi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inapokosoa serikali, wananchi waende wapi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Nov 25, 2008.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hivi sasa imekuwa kawaida kwa viongozi wa serikali kuinyoshea vidole serikali hiyo hiyo wanayoiongoza, je hii ni haki kwa wananchi ?

  Je kuna uhalali wowote kwa serikali inayoshindwa kutimiza wajibu wake kuendelea kubaki madarakani ?

  Je, Waziri Mkuu anapodiriki kusema kuwa matatizo yanayoikabili serikali yanasababishwa na watendaji wake, hii maana yake ni nini ?

  Je, Raisi anapolalamika na kuilaumu serikali kwa kutumia ubabe kushugulikia matatizo ya wanannchi, kweli yupo sahihi ?

  Je Waziri Mkuu anaposema watuhumiwa wa EPA wana nguvu ya kuitetemesha nchi, je hizo nguvu wanazitoa wapi ?

  Je Raisi anapowaruhusu wezi kurudisha mali waliyoiba bila kushtakiwa, anatumia vigezo gani kwenye katiba ?

  Kama Mkuu wa Brela anashindwa kutaja wamililki wa Kagoda na bado anaendelea na kibarua chake, hicho kiburi anatoa wapi ?

  Je, je, je, ?????? Najiuliza, sipati majibu - hivyo naenda kulala.
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mbona majibu unayo hapo juu? Na jibu la nini kifanyike liko wazi. Ukimwajiri mfanyakazi nyumbani kwako halafu akashindwa kazi unamfanyaje?? Shidi hapa inatoka na waajiri (WaTZ) kutojua kuwa wao ndo wenye kazi na kwamba hatima ya vibarua wao walioshindwa kazi iko mikononi mwao. Laiti wangejua hilo, tungeshamaliza party na mvinyo wote kwenye chupa!!!
   
 3. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #3
  Nov 25, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma habari leo kwenye gazeti la majira, Mkullo anadai eti mabalozi waliwadanganya Mawaziri wao kuwa JK alipanga kuwa samehe Mafisadi wa EPA ambao wangerudisha pesa. Kwa Mujibu wa Mkullo eti JK alisema warudishe pesa kwanza halafu ndo hatua za kisheria zifuatwe. Hivi katika hotuba yake ya mwisho bungeni wenzangu mlimuelewaje. Je mkullo yuko sahihi?

  Pinda na JK wameonyesha kutokuwa na meno ya kushughulikia watendaji wa serikali. Wamebaki kulalamika tu as if huu mfumo wa serikali yetu umeshushwa kutoka mbinguni na haustahili kufumuliwa. Cha msingi ni wananchi kuwashughulika wao kama wameshindwa kazi.
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu mag3 kwa kweli inashangaza!!!!!!!!!!!!
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Nyambala,

  Hakika inashangaza wananchi nao wanapoafiki na kusema Raisi wao anaangushwa na watendaji ama wasaidizi wake, je hao wananchi tuwabatize jina gani ?

  Je mwananchi anayemsifia Raisi hata wakati ni wazi anaboronga, huyu ni mzima ama kalogwa ?

  Je mwananchi anyewacharukia wengine wanaothubutu kuita upuzi kuwa ni upuzi, hao nao wanaonyesha mfano gani ?

  Yaani maswali ni mengi - wewe acha tu.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani haka ni kama kale ka msemo amabako wengi wa hicho chama cha majambazi wanapenda tukaamini kwamba CCM siyo mbaya ila ina wanachama na viongozi wabaya as if CCM ni gari au nyumba.
   
Loading...