Serikali inapohangaika na mitihani ya Form 4 na Form 6 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inapohangaika na mitihani ya Form 4 na Form 6

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by bibikuku, Aug 15, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nimeikuta habari hii nikaona niilete hapa tujadili;

  WIZARA YARUDISHA MIHULA YA ZAMANI YA MITIHANI FORM FOUR NA SIXW

  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imerudisha utaratibu wa mihula kama ilivyokuwa zamani kutokana na kile ilichoeleza kuwa utaratibu wa sasa unasababisha walimu kutumia muda mwingi kusimamia na kusahihisha mitihani wakati wa masomo.

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema kwamba mwakani utaratibu wa kufanya mitihani kwa Kidato cha Nne na wa Kidato cha Sita utakuwa kama ilivyokuwa zamani.


  • Wakati hivi sasa mitihani ya Kidato cha Nne imekuwa ikifanyika Oktoba, mwakani itafanyika Septemba.
  • Kwa upande wa Kidato cha Sita ambao mitihani imekuwa ikifanyika Februari, mwakani itakuwa Mei.
  • Utaratibu wa likizo utaendelea kuwa Juni na Desemba.

  “Mwakani tunarudi kama ilivyokuwa mihula ya zamani. Kidato cha Nne wafanye mitihani Novemba badala Oktoba na Kidato cha Sita itakuwa mitihani Mei kama zamani ili walimu wabaki kufundisha shuleni badala ya kuzunguka kwenye mitihani na kusimamia,” alisema Naibu Waziri.

  Uamuzi huo unalenga kuondoa kile ambacho baadhi ya wabunge walilalamikia kuwa baadhi ya walimu wamekuwa badala ya kufundisha, kutumia muda mwingi kusimamia mitihani na pia kwenda kusahihisha.

  Kwa utaratibu uliorejeshwa, usahihishaji kwa Kidato cha Sita utafanyika kipindi ambacho wanafunzi watakuwa likizo ambacho ni Juni.  Source: wavuti - wavuti

  MY TAKE; Najiuliza sana, form six baada ya mtihani Mei, watakuwa na muda gani hadi kupata matokeo yao, na kisha ku-apply vyuo vikuu na bodi ya mikopo ili ikifika Septemba wawe wameshaingia vyuoni tayari?
   
 2. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Another episode in a silly season,wizara inaongozwa na under performers,dr kawambwa alitimuliwa udsm baada ya kushindwa kuandika maandko yanayo defend position yake.Mulugo alipata zero form six na anakashfa ya shule yake kuiba mitihan
   
 3. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,273
  Likes Received: 2,949
  Trophy Points: 280
  Serikali ya kukurupuka unadhani itaweza.
   
 4. m

  massai JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huyo mulugo mpaka jina kafoji.hamna kitu hapo,hii sisiemu kwa kweli ni janga la kitaifa.huyo mulugo achunguzwe ni hewa hamna kitu hapo
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Duh! Ule utaratibu wa kumaliza shule kwa form six na kukaa nyumbani mwaka mzima wanaurudisha tena!?
   
 6. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ukirudi huo utaratibu, mafataki mjini watawamaliza wadogo zetu.
   
 7. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Filipo inawezekana kabisa vijana wakaanza kukaa mwaka mzima home kusubiri matokeo na kisha kufanya applications za vyuo kama enzi za mwinyi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Hawakai nyumbani, bali wataenda JKT!
   
 9. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Yaani mtoto amalize Form IV Novemba, aende Form V July? Si nzuri kwa watoto wetu, hasa wa kike. Kwa nini tusifuate mifumo ya kwingineko duniani?
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kiini cha kufeli kwetu kama taifa ndicho hiki. Tunachezea elimu yetu kama mwanasesere
   
 11. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2012
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,202
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  kichwa cha mwenda wazimu.....ndo mfumo wetu wa elimu, kila waziri akiingia huingia na "kichaa chake"
   
 12. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  kwaiyo alifafanua sasa itakuweje kwa form six na bodi ya mikopo pamoja na lini haswa wanaingia chuo?au mfumo nao umebadirika?
  una nasikia hasira sana awa mabozo mawaziri wanapoongea maneno yanayoacha maswali badala ya kutoa utatuzi!!!
   
 13. Vodka

  Vodka JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 909
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwani tatizo nini kwa mfumo wa sasa naona hayo mawazo yao si sahihi.
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Mbona kama hii taarifa inachanganya!
   
 15. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Inawezekana wamefanya typing error
   
Loading...