Serikali Inaiona Hatari Hii?

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
japo si mwanamazingira, lakini suala la mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa ni dhahiri na linaweza kutamalaki mahala popote Mungu akiamua.

Tunakumbuka ya Kimbunga Katrina kilivyoitafuna New Orleans.

Tunakumbuka namna New Zealand ilivyotikiswa juzijuzi tu hapa.

Tunakumbuka namna Tsunami ilivyotafuna kisiwa cha Java hiko Bangladesh.

Na sasa dunia na macho yote hayako tena kwa Gaddafi; dunia sasa inahaha kujinasua na tishio la kinu cha nyuklia cha Japan baada ya nguvu ya Mungu kudhihirika kupitia Tsunami.

Tanzania na hasa hukanda huu wa Pwani, na hasa hasa Dar Es Salaam vipo kwenye mdomo wa mamba. Bahari ya Hindi.

Ikulu ya Dar Es Salaam iko salama kiasi gani tunaposikia nchi yenye technolojia na watu makini kama Japani inatikiswa na nguvu hii ya Mungu? ?

Wakazi wa maeneo tambarare kama Mbweni wako salama kiasi gani tunaposikia nchi yenye technolojia na watu makini kama Japani inatikiswa na nguvu hii ya Mungu?

Wakazi wa Kigamboni watakimbilia wapi siku nguvu hii itakapodhihirika nchini kwetu?

Najua wabongo ni watu wa majungu. Mtasema huu ni uchuro.

Naenda zangu Church.
 
mnh sawa sio uchuro ila siku zote ATAKAEJIKWEZA ATASHUSHWA NA ATAKAE JISHUSHA ATAKWEZWA...............
 
Ogopa sana viongozi wanaoamka na kushika makutano ya miguu yao kila siku. Pia ogopa sana viongozi wanaoshika matumbo yao waamkapo asubuhi. Hawa wote hufikiri vitu viwili tu. Matumbo yao na wan**** tu. Kama unataka kuthibitisha hili njoo Dodoma wakati wa bunge vyakula huwa vya shida na changudoa kutoka sehemu mbalimbali hufika ili kuwahudumia. Kwa namna hii itawezekanaje basi wafikiri kuwaepusha wananchi wao na majanga kama haya? Yaani Dar, Tanga, Pangani na sehemu nyingine zipo katika hatari kubwa sana. Siku ikitokea Sunami kweli nchi nzima itanusa harufu ya mizogo.
 
Back
Top Bottom