Serikali inaelekea kufa - Mbunge wa CCM Ole Sendeka

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
Sendeka azua balaa
Kauli ya Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka kwamba Serikali inaelekea kufa kutokana na mgawanyo mbovu wa rasilimali, imechafua hali ya hewa bungeni baada ya wabunge wenzake wa CCM akiwamo Kapteni John Chiligati kumpinga na kumshambulia.

Juzi, Sendeka akichangia hotuba ya makadirio ya Wizara ya Ujenzi alitoa hoja hiyo nzito ya kuitabiria kifo Serikali inayoongozwa na chama chake akiifananisha na mbwa mwitu aliosema kuwa wakipata kitoweo, hunyang'anyana bila kufuata utaratibu wa nani apate kipi, kiasi gani na kwa wakati gani.

“Nimesimama kuomba mwongozo wako kufuatia hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe Magufuli ya mwaka huu inayoashiria na kuweka rekodi ya kuendelea kuonyesha ubaguzi katika ugawaji wa barabara za lami katika nchi hii na kudhihirisha wazi kabisa kwamba Serikali inavyofanya kazi sasa na kwa miaka ya karibuni."

"Inafanya kazi (Serikali) katika mtizamo unaoonyesha kwamba imeanza safari kwenye kifo chake kutokana na sifa moja kubwa nitakayoitaja, kwamba barabara zilizogawanywa katika nchi hii zinatazama maeneo walikotoka viongozi wakubwa na walioko katika vikao vya maamuzi na wanakotoka watendaji wakuu wa Serikali na ukitaka nitatoa mfano."

Kama kuwasha moto kwenye petroli, hoja hiyo ya Sendeka jana ilijibiwa vikali na baadhi ya wabunge wa CCM. Kepten John Komba wa Mbinga Magharibi alisema anashangazwa na wanaopinga bajeti hiyo baada ya kuona kuna miradi ya barabara katika mikoa ya kusini wakati katika maeneo yao kuna lami hadi mazizini na kwenye kumbi za disko.

“Leo imekuwa nongwa watu wa kusini wanapokombolewa kwa barabara mbona tulikuwa na viongozi wa kitaifa kina Kawawa (hayati Waziri Mkuu na Makamu wa Rais), lakini waliona kwanza wasaidie maeneo mengine sasa leo hii kidogo imekuwa nongwa!” alihoji Komba.

Komba alisema safari hii kisungura kidogo kimeelekezwa kusini hivyo ni vyema wabunge wakubali badala ya kupiga kelele.

Source: Mwananchi
 
Hilo ni tatizo la kutokuwa na sera ya taifa ya maendeleo kila waziri huja na mtazamo wake wa maendeleo.
 
bajeti ya wizara haikugusia jimbo lake ndiyo maana karopoka. anyway kifo cha serikali ya kikwete haihitaji utabiri, inahitaji maandalizi ya kuizika rasmi
 
bajeti ya wizara haikugusia jimbo lake ndiyo maana karopoka. anyway kifo cha serikali ya kikwete haihitaji utabiri, inahitaji maandalizi ya kuizika rasmi


Kwani ile barabara inayoanzia Makuyuni kwenda Singida Kupitia Babati kateshi etc inapita mkoa gani
 
Back
Top Bottom