Serikali ina lengo gani kutetea Sheria ya Ndoa inayoruhusu watoto wenye miaka 14 kuolewa?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mapungufu na changamoto zilizopo katika Sheria hii zinaleta mkanganyiko katika kusimamia na kutafsiri masuala yanayohusu ndoa nchini Tanzania.

Kwa mfano Sheria ya Ndoa inakinzana na Sheria ya mtoto ambayo inamtafsiri mtoto kama mtu yoyote alieko chini ya umri wa miaka 18, wakati Sheria ya ndoa inaruhusu msichana chini ya umri wa miaka 18 kuolewa.

Kwa misingi hiyo, Sheria inatoa mwanya kwa ndoa za utotoni. Vile vile Sheria hii inakinzana na kanuni za adhabu ambayo imeanisha kwamba ni kosa la ubakaji kwa mtu yoyote kufanya Ngono na mtoto chini ya umri wa miaka 18 isipokua kama ameolewa.

Binafsi nilitarajia kuona Serikali inakuwa mstari wa mbele kufuta Sheria zinazoruhusu watoto kuingia kwenye Ndoa, badala yake imekuwa ya kwanza kutetea watoto waoelewe bila ridhaa yao.

Katika kesi namba 5 ya mwaka 2016, Mwanaharakati Rebeca Gyumi alipinga vifungu namba 13 na 17 vya sheria hiyo ya ndoa namba 5 ya mwaka 1971 kama ilivyorejewa mwaka 2002.

Kifungu cha 13 (1) kinaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri kuanzia miaka 15, lakini kwa mtoto wa kiume kuanzia miakam 18.

Kifungu cha 13(2) kinaruhusu ndoa ya watoto wenye umri wa miaka 14 kwa kibali cha mahakama pale itakapojiridhisha kuwa kuna mazingira maalumu ya ndoa hiyo.

Kifungu cha 17 kinaeleza kuwa mtoto wa kike chini ya miaka 18 ataolewa kwa ridhaa ya wazazi au walezi na kama wazazi wote na walezi hawapo, basi hatahitaji ridhaa.

Gyumi alidai kuwa vifungu hivyo vinakiuka Katiba ya nchi kwa kuminya utu na haki ya mtu kujieleza kama zilivyoainishwa kwenye Ibara ya 12 na 18 ya Katiba.

Pia alidai vifungu hivyo vinakiuka Ibara za 13,12 na 18 zinazotoa haki ya usawa mbele ya sheria, kutokubaguliwa, kuheshimu utu wa mtu na uhuru wa kujieleza.

Mahakama Kuu katika hukumu yake Julai 8, 2016 ilikubaliana na hoja za Gyumi na ikavibatilisha vifungu hivyo.

Pamoja na mambo mengine ilisema mtoto katika umri wa miaka 14 hana ufahamu kujihusisha na mambo ya ndoa na kwamba suala la ndoa ni uamuzi wa mtu binafsi na si uamuzi wa wazazi au mtu mwingine.

Hivyo iliamuru umri wa kuolewa uwe kuanzia miaka 18 na kuendelea, huku ikiiamuru Serikali ndani ya mwaka mmoja iifanyie marekebisho sheria hiyo kwa kuondoa vifungu hivyo.

Serikali ilikata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu hiyo, pamoja na mambo mengine ikidai vifungu hivyo vinalenga kuwalinda watoto dhidi ya ngono na kupata watoto nje ya ndoa.

Mahakama ya Rufani katika hukumu yake Oktoba 23, 2019, ilikubaliana na hukumu ya Mahakama Kuu na kuunga mkono hoja zote ilizozitoa ikisisitiza havina manufaa yoyote kwa mtoto wa kike.

Ilisema ndoa ni mkataba na kwamba ndoa ya mtoto mdogo ambayo ridhaa anatoa mtu kwani inakosa sifa za kikanuni za kimkataba ambazo ni umri stahiki na hiyari.

Sasa licha ya Mahakama Kuu kubatilisha Kifungu cha 13(1), 13(2) na 17 cha Sheria namba 5 ya Ndoa ya mwaka 1971 vinavyoruhusu Watoto kuolewa, nashangazwa kuona Serikali ilikata rufaa na kutetea Sheria hiyo kandamizi kwa Mtoto na bado iko mtaani ikikusanya maoni ya wadau badala ya kufuta Sheria hiyo ya hovyo.

Ni wazi sasa Serikali ifuate matakwa ya Katiba ya Nchi yanayoagiza Haki Sawa, Kutobaguliwa na Kuheshimu Utu, lakini pia isiwe chanzo cha kuhalalisha Ukatili dhidi ya Watoto kwa kuvunja Haki zao kwa Sheria hatarishi.
 
Ukute vitoto vyetu vyenyewe vinapeeeeeendaaa kweli kweli!

Inasikitisha sana
 
hawa wanaharakati uchra wakishamalizana na hili la ndoa, wataanza kupigania na ndoa za mashoga. Watakapoanza na hilo pia muwasapoti.
 
Back
Top Bottom