Serikali ina fedha, sasa vipi mishahara ya tazara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ina fedha, sasa vipi mishahara ya tazara?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, May 17, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ni jambo kama siyo la kusikitisha na kustaajabisha, basi la kuhuzunisha kwa jinsi mambo yanavyokwenda kisiasa siasa tu wakati watu wanaishi maisha ya taabu kweli kweli nchini Tanzania.

  Hivi majuzi hapa, mbunge wa Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) alitamka kuwa Serikali haina fedha ndiyo maana imeshindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake. Punde si punde, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo akakanusha vikali madai hayo na kuita ni uzushi na kujitafutia umaarufu.

  Zikatoka na Takwimu za Mkulo na Zitto za hali ya Serikali kifedha.

  La kushangaza, wafanyakazi wa TAZARA waliogoma tangu siku kadhaa zilizopita kwa kukosa mishahara, hadi leo Mei 16, bado hawajapokea mishahara yao na wanaendelea kugoma.  Hivi hawa wafanyakazi wa TAZARA siyo kielelezo dhahiri cha Serikali isiyojali wafanyakazi wake? Hata ikiwa TAZARA ina uongozi, msimamizi mkuu na wa mwisho wa TAZARA na mashirika/makampuni yote nchini ni nani kama siyo Wizara ambayo ndiyo Serikali?

  Mbona kauli za viongozi wetu waliopewa dhamana ya madaraka na kuiongoza nchi wanatamka kauli zinazopingana na hali halisi?

  Kweli mtu unawezaje kupitiliza nusu mwezi bila mshahara na unahitajika kufika kazini kuendelea kazini na kuzalisha kwa ufanisi il hali una hakika kuwa kufanya kazi kwako tangu saa mbili asubuhi hadi kumi jioni kutakuacha bila muda wa kufanya kazi ya ziada ili kupata kipato cha kuitunza familia kwa siku hizo?

  Kwa hivi, mfanyakazi atakapotumia muda wa kazi kwa shughuli binafsi kutafura 'mkate' wa siku kwa familia yake ambayo matatizo na mahitaji ya siku hayajali kuwa hujalipwa mshahara, atakuwa anastahili adhabu? Ndiyo, kwa mujibu wa sheria, anastahili kuadhibiwa, laiti sote tungekuwa tunaishi kwa sheria bila kujali utu...
   
Loading...