Serikali ina dira gani kupitisha mpango wa kujitolea Hospitali za umma?

nashukuru mzima

JF-Expert Member
Jul 11, 2017
1,014
1,896
Habari.

Kwanini serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya na wizara ya TAMISEMI wameweza kupitisha muongozo wa ajira za kujitolea katika hospitali za mikoa na wilaya na zikitaka Hospitali hizo kulipa kupitia mapato yao ya ndani.

Narudi kwa mada serikali yetu:

1. Je serikali imejiandaa Vipi kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana waliosoma afya ilhali ikihamisha vijana wajitolee kwa malipo ya nusu ya mshahara?

2. Upungufu wa watumishi wa umma katika idara ya afya kwanini serikali inataka kupunguza kupitia watoto wadogo kujitolea kwa kazi nyingi na ujira mdogo.

3. Vijana wanajitolea wanafanyishwa kazi nyingi pasipo na utaratibu sahihi hasa kwa watumishi wa umma walioajiriwa serikalini.

4. Malipo yanatolewa pasipo kuzingatia wakati na utaratibu sahihi Je yanaleta changamoto kubwa katika maisha ya wanaojitolea.

Nauliza Je serikali ina dira gani katika vijana wanaojitolewa nje ya Kuwapa ahadi hewa ya Kuwaajiri?
 
Serikali inavyooneka iko busy zaid na kukusanya Kodi pamoja na kushindana na vyama pinzani .

*Bila katiba mpya serikali haina Dira.
 
Ushauri wangu ni huu jaribu kuangalia upande wa pili wa ajira
1. SGR project
2. BRT project
3. New Mining Site
Jaribu huko
 
Kuna Uzi uko hapa JF tembelea uka usome

Kujitolea ni utumwa, Kataa utumwa wa kujitolea.
 
Back
Top Bottom