Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,798
- 71,218
Tuhuma nzito hadi hatua zimechukuliwa serikali kimya tuu. Hatua hizo kama zingemhusu Makonda na mkewe pekee tungesema potelea mbali, lakini zimegusa hadi vijana wetu waliokuwa wanafaidika na bahati nasibu ya Visa katika utafutaji wao wa maisha huko nje.
Hivi maofisa wengine wa serikali hawawezi kuchukuwa hatua zozote kama jambo litamhusu Makonda kwa sababu ni "mpendwa" wa Rais?
Maana hasa hizo tuhuma zinazohusu kupoteza maisha zinasubiri waambiwe na Rais fuatilieni? Au wanaamini kila afanyacho Makonda kina ruhusa ya ofisi kuu?
Nadhani sasa kwa vile mtu binafsi kama Msando kaandikia "American Embassy" kupinga jambo hilo, basi kwa sasa taasisi za haki za binadamu na kidemokrasia vikiwemo vyama vya Siasa viandike navyo barua kwa "The Embassy of United States of America" kuomba watoe Ushahidi walio nao kuwa Makonda ameshiriki vitendo vya kuondoa haki ya kuishi watu kadhaa.
Usije kuta USA wanatukosanisha bure wakati Makonda ni kijana mwema na mfano wa kuigwa na wengine kwa utakatifu wake.
Na serikali yetu 'sikivu' inalijua hilo hata mpendwa Rais wetu kipenzi cha 'wanyonge' anatambua utendaji uliotukuta wa kijana huyu.
Tushinikize taasisi hizo ziandike hizo barua ili US watoe Ushahidi wao na kama ni 'fake' waumbuke.
Sent using Jamii Forums mobile app