Serikali imetoa agizo leo la kusimamisha withdraw kwa wanachama wote wa hifadhi za jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali imetoa agizo leo la kusimamisha withdraw kwa wanachama wote wa hifadhi za jamii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mahololelo, Jul 20, 2012.

 1. m

  mahololelo Member

  #1
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kuna tetesi kwamba serikali imetoa agizo leo mifuko yote ya hifadhi ya jamii kuacha kutoa mafao ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi wote watakao acha au kufukuzwa kazi kabla ya muda wa kustaafu kufika kuanzia leo.Taarifa hii imetolewa na meneja wa NSSF Mkoa wa Mara,Ndg MVUNGI pamoja na HR meneja wa barrick north mara leo wakati wanatoa ufafanuzi juu ya mambo yanayohusu sheria mpya ya mifuko ya hifadhi ya jamii.MWENYE TAARIFA KAMILI ATUJUZE
   
 2. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 670
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Sina uhakika na hili, lakini kama itakuwa hivi sasa huu utakuwa ni wizi wa mchana kweupe. Maana ule ni mchango wangu uliokatwa kihalali toka mshahara wangu. Maana yake ni sawa na kunambia nirudishe mishahara niliyolipwa huko nyuma. Sheria nyingine nadhani zinahitaji kuangaliwa upya kama haya ni ya kweli!
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hivi hii sheria mpya inaathiri sisi wafanyakazi wa mikataba mifupi?
   
 4. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Kuufuatia kuanzishwa kwa SSRA ( social security regulatory authority)serikali ilipitisha sheria inayoyataka mashirika yote ya hifadhi ya jamii kuacha kutoa mafao kwa wafanyakazi wasio fikisha umri wa kustaafu. Mtazamo unaotumiwa na serikali ni kwamba endapo mtu atatumia mafao yake leo kabla ya kutimiza umri wa kustaafu umri ambao hatakuwa na uwezo wa kufanya kazi tena mtu huyo atakuwa na uzee wa tabu. Hi ndiyo sababu inayotumiwa na serikali.
  Lakini mimi nafikiri serikali imefanya hivyo kwa sababu kuu mbili
  1. Mifuko ya hifadhi ya jamii ni source kubwa ya mikopo kwa serikali yaani ndipo mahali serikali inapata readily available funds hivyo kuwaruhusu watoe mafao kwa watu wengi ni kupunguza availability ya funds za kujikopesha. Ikumbukwe pia kuwa kwa sasa mifuko hii haina pesa kwa kuwa pesa yote imekopeshwa serikali ( eg bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu} au kutumika katika miradi mikubwa yaani long term investments ambayo hailipi haraka.
  2. Serikali ina lengo la kukwepa wajibu wake wa kutunza wazee hivyo ina discourage watu kutumia pension zao sasa ili waje wajitunze wenyewe watakapo zeeka.
   
 5. Captain Phillip

  Captain Phillip JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 900
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu nimepata taarifa muda si mrefu kutoka mgodi wa Bulyanhulu kuwa hali huko pia ni tete kufuatia tangazo hili.Watu wanarizain kwa kasi ya ajabu wakiamini kuwa sheria bado haijaanza kutekelezwa.
   
 6. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Kama ni kweli ni aibu sana kwa taifa. Ni unyonyaji mkubwa kuliko wa mkoloni kwa sababu; sio lazima mtu aajiriwe hadi afikie umri wa kustaafu, anaweza akaamua kuacha kazi akafanya mambo yake. Nadhani huu ni mwendelezo wa madhaifu makubwa ya watunga sheria wetu wanagonga meza na ndiooooooooo nyingi za kishabiki. Kimsingi hili litakuwa taifa la ovyo sana linaloongozwa na wababaishaji. Its not fare na kama ni kweli shame on them
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  msituharibie siku, na mpango wa kuacha kazi mwezi wa tisa ili nijiajiri kwa NSSF yangu.
   
 8. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Think twice before making a final decision. This country of ours is now making sure we all get confused. Isije ikawa kweli ukapata concussion.
   
 9. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Hii Sheria itatumika mpaka Dec 2015.

  CHADEMA KAZENI BUTI HAPO HAPO. KATIKA CAMPAIGN MSISAHAU HUO MSTARI KABISA.

  ''Watanzania mkitupa dola wafanya kazi watakua wanapata mafao yao ya hifadhi za jamii within one month''

  Viva CCM for being blind on this
   
 10. w

  wikolo JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hii siyo tetesi mkuu isipokuwa ndo ukweli wenyewe. Ukiacha au kuachishwa kazi huruhusiwi kuchukua mafao yako hadi utimize umri wa kustaafu.
   
 11. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Haya ndo mambo mtu akiandamana au akigoma naweza kumuunga mkono. Ingawa mimi nijuavyo wapo kwenye mchakato wa kufanya hivyo
   
 12. L

  LIpili Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 14, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii mifuko imekopwa sana na serikali na huwa hawalipi madeni yao, kitendo cha kuendelea kuruhusu withdraw kabla ya umri wa kustaafu kitapelekea mifuko hii kufilisika muda wowote.
   
 13. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Mkuu sina hakika na ukweli wa hii habari lakini kila ninapoilazimisha akili yangu isiiamini najikuta nashindwa.
  Sababu ni kuwa Serikali imeikopa hii mifuko kwa kiwango cha kutisha.
  Pia badhi ya mifuko imejiingiza kwenye miradi ambayo ROI yake ni ya kutia shaka.
  Sasa kwa sababu hizo unaweza kukuta wame-forecast wakaona huko mbele watachemsha hivyo watumie njia hiyo as a way to retain some amount of money...
   
 14. B

  Baba Emmanuel Member

  #14
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi Binafsi sipo tayari kukubaliana na haya mawazo ya wasiojua shida zetu watanzania. Wengine hiyo ni hela ya kuweza kuajili baada ya mda fulani na isitoshe Wastani wa maisha ya mtanzania ni miaka 47, Je Miaka 55 hadi 60 itafikiwa na wangapi? Nipo tayari kuandamana hata leo na ikibidi kupigana tu kuondoa haya mawazo ya kifisadi.
   
 15. rom

  rom Senior Member

  #15
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kwa hili tutaandamana............... haiwezekani nipewe hela yanguu..
   
 16. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,725
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Je acturaial report zinasemaje juu ya condiction ya hii mifuko, maana naona kama ipo dhhoofulihali. Je spirit behind this can be liquidity issues, a lot of projects committed which need cash. Anyway watwambie are they going to strenghthen the mazingira ya kazi kwa wabongo maana everyday watu wanaachishwa kazi na mkombozi wao ni hiyomifuko. Kama kweli mna nia njema toeni ufafanuzi maana hawa wafanyakazi ndio watoa kodi na waendesha nchi. Ok wale wakulima mnaowaambia wajiunge na hayo makampuni nao wasubiri 55 yrs. Mazee bongo tuna CURSE.
   
 17. b

  bullof New Member

  #17
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli serikali imepitisha sheria kuzuia watu wanao acha au kufukuzwa kazi kudai mafao yao kabla ya kutimiza miaka 55. Huu ni upuuzi wa hali ya juu, sijui nchi inakwenda wapi. Hivi inaingia akilini mtu anae dai milioni 10 kusubiri afikishe umri wa kustaafu ndiyo apewe hiyo milioni kumi? itakuwaje akifa kabla ya huo muda? na je hiyo milioni kumi itakuwa na thamani wakati huo, au itakuwa kama yale ya wafanyakazi wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki? Mimi ni mmoja wa wahanga wa hiyo sheria ya maangamizi, ingawa ninacho dai ni kidogo nitalazimika kusubiri miaka mingi ijayo ndiyo nipate hicho kitu kidogo.

  Kama wachangiaji wengi walivyo eleza serikali imefanya hivyo ili sasa iwe na nafasi nzuri ya kucheza na michango ya watu kama inavyo penda. Mifuko hii ya jamii ni chanzo cha uhakika chs fedha kwa serikali kwani kwa mujibu wa sheria kila mfanyakazi na mwajiri wanapaswa kuchangia mfuko, wapende wasi pende. Hii si sahihi serikali haikupaswa kuingilia mafao ya watu, kwakuwa mafao hayo yanatokana na mishahara ya mwanachama i.e ni haki za wanachama. Hivi sasa kila mtu ana lalamika, analia na serikali hii isiyo na chembe ya huruma. Serikali imekuwa katili kupita kiasi kwa wananchi wake. Watu wameacha kazi wakitegemea hicho kidogo kama mtaji wa kuanzisha japo kabiashara lakini imekuwa ndoto. Wengine walitegemea hayo mafao kwa ajili ya kujiendeleza kielimu lakini imekuwa ndoto, wengine wameacha kazi kwa kusumbuliwa na maradhi na walikuwa wakitegemea sana hayo mafao kwa matibabu sasa kifo kina wanyemelea:fear:

  Hakuna jinsi ila ni kufikisha hili suala mahakamani, huenda safari hii hawatasema ni jambo la kisiasa lirudishwe bungeni kwa makinda na ndugai kama ilivyokuwa kwa suala la mgombea binafsi
   
 18. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #18
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,841
  Trophy Points: 280
  jamani hebu sasa sisi wafanyakazi wote ambao ni wanachama wa hii mifuko tuamke wao hawawez kuwa na regulatory board wakati sisi wapeleka michango hatuna mtetezi wetu. hivi kweli wanaofanya kazi kwenye mashirika na makampuni binafsi si ndio mnataka vi nssf vyao vipotee kabisa?

  pili mimi huwa ninajiuliza swali hili kwani wanangu watasoma nikiwa mzee ama watasoma nikiwa bado kijana? na je nitaish nyumba nzuri nikisha zeeka ama leo hi nikiwa kijana?

  ikumbukwe akbisa wastaafu wengiambao walikuwa ni govt officials walipopewa hivi viinua mgongo vyao ndipo walipoanza eti kujenga na kunua magari matokeo yake wamefia nyumba za kupanga. mimi mtoa mchango nataka nipewe haki yangu niitakapo manake ndipo ninapoihitaji na ipo ili kunisaidia mimi. uzeeni ya nini sasa?
   
 19. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Hii serikali chokozi nakuunga mkono kuandamana maana sasa tumechokozwa wengi huu ni wizi wa mchana kweupe.
   
 20. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Yaani hii ndio sababu kubwa ya kupitisha jambo hili.

  Serikali katika bajeti zake inatumia sana pesa zetu na ndio tegemeo lake, na pia pesa za Shirika la BIMA la Taifa (NIC)

  Katika bajeti iliyopita mwaka jana serikali ilizidiwa hadi kufikia kukopa STANBIC BANK kwa ajili ya kupitisha bajeti ingawa bado serikali ilishindwa kwa asilimia 80 kutoa pesa kwa bajeti kama ilivyopitisha kutokana na kufirisika kwa Account za Serikali.

  Ndio maana wamekuja na agizo hili ili kupata pesa za kupitisha bajeti ya mwaka huu ambayo toka siku ya kwanza ilionekana haitekelezeki.

  Hivyo Wafanyakazi tusimame kwa mshikamano kupinga hili jambo, kwanza hatukushirikishwa na pili ni dhuruma na uonevu kwani sisi tulioajiriwa katika sekta binafsi hatuna hata SECURITY OF EMPLOYMENT, sasa nikiachishwa leo sina uhakika wa kupata kazi hata ipite miaka 3.

  SI KUNIUA huku!!!!!!!!!!!!!  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
Loading...