Serikali imepoteza zaidi ya milioni 500 kumlipa mkandarasi hewa Mkoani Simiyu

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, imebaini kuwepo kwa matumizi hewa ya zaidi ya shilingi Milioni 500, yaliyofanywa na Meneja wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Wilayani humo Mhandisi Jeremiah Lema kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Pett Cooperation Ltd, anayejenga mradi wa chujio la maji wa Zanzui bila kibali cha Bodi ya maji Wilayani humo.

Mkuu wa wilaya ya Maswa Rosemary Kirigini, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema kuwa meneja huyo pia anadaiwa kuidanganya kamati hiyo ya ulinzi na usalama kuhusu ununuzi wa Krasha iliyodaiwa kuagizwa toka nchini china.

Mkurugenzi wa kampuni ya Petty Coopertion Ltd inayotekeleza ujenzi wa mradi huo wa chujio la maji wa Zanzui kwa ushirikiano na kampuni ya Josam and Company Ltd Tryphon Elias,akatoa ahadi ya kukamilisha mradi huo tarehe 30 mwezi Mei.

Lugha gongana kati ya Mwenyekiti wa Bodi ya maji wilayani Maswa Aloys Kimisha na Meneja wake Mhandisi Jeremiah Lema kuhusu wananchi kunyweshwa maji ambayo hayajatiwa dawa,ikaibuka mbele ya Mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtakaje, mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka yuko tayari kuwajibika iwapo wananchi wa Maswa watakunywa maji yasiyotibiwa na kuugua magonjwa ya mlipuko kikiwemo kipindupindu.


Chanzo: ITV
 
Nchi hii ilikuwa imeoza kila mahali, tumuombee kwa Mungu magufuli na majaliwa waweze kuisafisha
 
kinachofurahisha zaidi,ndani ya siku 2 tutakuwa tumeshasahau hili suala na kuendeleza majigambo ya nani zaidi kwenye siasa.
 
Hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika na ubadhirifu huo.
 
huku wafanyakazi hewa huku manunuzi hewa... kule mikataba mibovu.

wahusika wachukuliwe hatua za kisheria sio kuhamishwa vitengo.
 
Back
Top Bottom