Serikali imefuta soko huria? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali imefuta soko huria?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pundamilia07, Sep 12, 2008.

 1. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Coaster, DCM nazo kuondolewa Dar

  2008-09-12 11:18:07
  Na Richard Makore


  Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), inatarajia kubadili mfumo wa usafiri kwa mabasi ya abiria (daladala) jijini Dar es Salaam kutoka kwa umiliki wa mtu mmoja mmoja kuwa wa makampuni makubwa binafsi na ya umma na kuondoa magari yote yanayobeba abiria chini ya 65.

  Hatua hiyo ilitangazwa jana na Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Kanda ya Mashariki, Walukani Luhamba, alipokuwa akizungumza na Nipashe.

  Alisema baada ya mfumo huo kukamilika, Jiji la Dar es Salaam litakuwa na huduma safi na bora za usafiri kama zipatikanazo nchini Japan.

  Aliishauri serikali kulifufua Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), ili liweze kuingia katika biashara hiyo kusaidiana na makampuni binafsi yatakayojitokeza.
  Alisema, UDA bado ni shirika zuri na kinachotakiwa kufanywa na serikali ni kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wake waliohusika kuliua na wale wanaoendelea kulimalizia.

  Luhamba alisema mchakato wa kusajili makampuni hayo utaanza baada ya miezi sita ijayo, ambapo muombaji atatakiwa kutuma maombi maalum ya kutaka kutoa huduma ya usafiri jijini.

  Aliongeza kuwa Sumatra imeweka utaratibu mzuri ambapo kila kampuni itakayojitokeza itapewa barabara yake kwa ajili ya kupitisha magari itakayokuwa nayo.

  Alitaja baadhi ya barabara zitakazokabidhiwa kwa kampuni hizo kuwa ni pamoja na zile za Morogoro, Ali Hassan Mwinyi, Nyerere na kwamba kila kampuni haitaingilia barabara ya mwenzake.

  Kuhusu umiliki wa mtu mmoja mmoja anayemiliki daladala alisema, atatakiwa kuingia mkataba na kampuni kubwa husika na hivyo kukabidhi gari lake huko.

  Sumatra jana ilirudia kauli yake kuwa mabasi madogo maarufu kama \'vipanya\' hayatapata usajili pamoja na magari yote yaliyotengenezwa kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita.

  Ofisa huyo alisema katika kuboresha usafiri hapa jijini wamesajili magari makubwa 3,000 na kwamba hali hiyo imepunguza foleni wakati wa asubuhi na jioni.

  Aidha, alisema kila siku mabasi madogo 15 yanaondolewa katika mfumo wa kutoa huduma ya usafiri na yatazuiwa kuingia katikati ya Jiji.

  Alifafanua kuwa baada ya mchakato wa kupata makampuni makubwa ya mabasi, mabasi aina ya Coaster na DCM nayo yataondolewa na kubakiza magari makubwa yenye uwezo wa kuchukua abiria zaidi ya 65 kwa wakati mmoja.

  Alifafanisha hali ya usafiri Dar es Salaam, kwamba itakavyokuwa kama Japan, nchi ambayo ina magari mazuri na makubwa na kwamba hilo linawezekana.


  Wadau,
  Huyu ofisa aliyekaririwa hapo juu ameongea hayu kama maoni yake binafsi au maoni ya serikali?

  Je, ni lini serikali itajitoa katika kufanya biashara? Leo hii bado kuna ofisa wa serikali anaongelea kufufua UDA?

  Leo bado kuna ofisa wa serikali bado anaongelea kuleta kampuni kubwa badala ya kuwajengea uwezo wananchi waendelee kutoa huduma kwa maana ya kujijengea uwezo wa kiujasiriamali? Huyu ofisa anakwenda mbali na kuonesha kuwa maamuzi yamekwisha tolewa kuwa kila mwenye gari lake akalikabidhi kwa kampuni kubwa.

  Iko haja atuelezee hayo mawazo ameyapata wapi? na pili huenda anamjua huyu mwenye kampuni kubwa, kuna kaharufu hapa?
   
 2. D

  Darwin JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Pundamilia we sema tu una magari ya daladala.

  Kuna kuikosoa serikali lakini sio kila kitu kinachofanywa na ofisa wa serikali nikibaya.

  Mimi nilisomea nje na najua uzuri wa mabasi makubwa kwa ajili yakuwasafirisha abiria.
  Hakuna msongamano na mabasi yanakufikisha kwa wakati unaoutaka.

  Walioko Europe au Marekani watanifahamu ninachosema.

  Kama wewe unataka soko huria basi fanya kama Arriva wanavyofanya Europe.

  Tangaza biashara yako kwa serikali ili wakupe kazi, ina maana hio ukivunja masharti ya mkataba kazi anapewa mwengine.

  Uwe na mabasi yakuwatosha abiria na yaondoke kwa muda bila kuchelewa.

  Huu utitiri wa magari ya abiria ndio hata serikali inashindwa kukontroo magari kwa wingi wake, na ndio maana kila leo ajali za magari ya abiria zinatokea.

  Kila mtu akipata vipesa vyake tu anatafuta kigari na dereva na kuweka gari barabarani. wanawekwa madereva ambao hata hawana ujuzi ili mradi tu bosi anapata pesa. Matokeo ajali za kila mara

  Hakuna mji wenye kero ya usafiri kama Dar.
  Dar hata kama una gari nawataka kwenda kazini lakini kero yake utaiona, foleni kila barabara.
  Na siku ukisema utumie daladala kwenda kazini basi ujiandae kwa mambo mengi, foleni, kugombania daladala wakati wa asubuhi, unatoka asubuhi msafi ukirudi nyumbani mchafu.

  Kukiwa na shirika moja tu lenye uhakika kusafirisha watu kwenda waendako sijui kama watu wataamua wapande magari yao kwa kila siku.

  Kumbuka pia foleni pia inasababishwa na huu mtindo wa kila mtu ambaye ana uwezo anaweka gari lake barabarani.

  Soko huria
  Liwe shirika moja kubwa hata ni la binafsi ambalo lina magari yakutosha kusafirisha abiria wa Dar.
  Liwe linafuata sheria za mkataba kwamba watu wengi wakilalamika kwamba wanachelewa au wanasongamana basi mkataba upewe mtu mwingine.

  Hapo tutaifaidi Dar yetu.
   
 3. D

  Darwin JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kumalizia, wanasema kama kila mtu atakuja na nyanya sokoni mnunuzi atakua nani?

  Sisi wabongo ndio zetu, utakuta sehemu hapana kitu chochote, ukaja na idea yako ukaanzisha kitu, watu wengine wakiona unapata faida basi wanaanza kile ulichoanza pale pale ulipoanzisha.
   
 4. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Darwin,

  Hakika umesema kila jambo muhimu, ila ningependa kusisitiza tu kuwa kwa hatua hiyo, SUMATRA inajaribu kufanya kazi yake: Kudhibiti. Soko huria lisipodhibitiwa linakuwa soko holela, halina utaratibu. Soko lisilo na utaratibu, matokeo yake ni kuumiza wateja, in this case, wasafiri, na hata mchango wa sekta hii ya usafiri katika uchumi hauwezi kuonekana, kwa kuwa hata wafanya kazi wananyonwa, hawalipwi vizuri, wasafiri wananyonywa, kwa kuwa hawapati huduma bora, serikali inanyonywa kwa kuwa kukwepa kodi kunakuwa kwa kiwango kikubwa.

  Hawa wenye dala dala, anaweza kuamka asubuhi moja na kuamua kuwa basi leo linaenda bagamoyo, kuipeleka familia kwa babu kumwona. Wakati huo kuna watu wanalisubiri Mwenge wapate huduma ya usafiri ili kwenda kulijenga taifa. UnadhANI WAKIFANYA HIVYO WENYE MABASI 50, impact yake ni nini kwa usafiri na performance economically?

  tatizo ni kuwa we dont like to think big. Mwenye dala dala anajiangalia yeye tu na wanawe, haijui thamani ya kazi yake kwenye uchumi wa jumla.

  Nilipokuwa shule nilipendekeza mfumo huo huo, kuwa watu walazimishwe kununua hisa kwenye shirika kubwa, litakalokuwa dedicated kutoa huduma ya usafiri kwa uhakika, usafi, na upesi.

  Kwa namna hii, watu wengi watakuwa wanaacha magari yao home na kupanda public transport. faida ni kuwa foleni itapungua kwa namna fulani, na maisha yatakuwa rahisi kwa kuwa pesa ya petroli kwa mtu wa kawaida itaelekezwa kwenye mambo mengine.
   
 5. C

  Chuma JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mbalamwezi mawazo its OK..na lkn si rahisi kama unavyoeleza!!!

  Wenzetu waliweka taratibu wakazifuata...Kumbuka Hii biashara ilikuwa ya Serikali tu, lkn Ikawashinda...Mafisadi wakaua KAMATA na UDA.
  Nimeona ktk safari zangu nje!!! sehemu kama Dubai Hiace zinabeba wafanyakazi, na mabasi Makubwa yanabeba Abiria, lkn Mabasi haya yanasimamiwa na GOVernment...lkn bado FOLENI ni kubwa....sasa wao wamekuja na TOLL system....lkn still haitosaidia...!!! Unachokifikiria sasa wengine washa implement na kina Ugumu wake!!!

  Same na TAXIs...leo zipo private TAX....mtaleta system kuwepo na Kampuni Kubwa still... Dubai wamefanya hivi..taxi zote zipo chini ya Kampuni lkn still hazitoshi...Kumbuka kunapokuwepo system za Kampuni wanachofanya Ku-Monopoly Hasa watu wachache wenye Connections na watu wa Serikali(Either kampuni za wakubwa..watoto wa wakubwa etc)
   
 6. D

  Darwin JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  [​IMG]


  Yaje haya kama mia moja tu, msongamano wa magari dar utakwisha.
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Ndio maana halisi ya soko HURIA!
  Umasikini wetu ulitufanya na bado unaendelea kutufanya wafuata mkumbo tu!
  Yani tuna dhahabu na almasi na kila aina ya utajiri lakini tunabadilishana kwa dawa za ukimwi,neti za mbu, na t-shirt za mitumba!
  Kisa ni hayo hayo ya soko huria pamoja na Absolute advantage sambamba na calculations za ki babylon za opportunity cost....Yani tuna give up madini kwasababu ya kuletewa nguo...Masai wanategemea mitumba toka lini?
  Na huo UKIMWI nani kauanzisha?
  UBINADAMU HAKUNA KABISA!
  AFRIKA TUWE HURU KWANZA.....
   
 8. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Darwin,
  Ahsante sana kwa mchango wako mzuri sana. lakini nilikuwa ninataka kukumbusha kuwa wengi wa watanzania ambao wanafanya biashara hasa ndogo-ndogo, ni watu ambao wameweza kujitafutia mitaji kwa nguvu zao wenyewe bila ya kupata msaada wa serikali au mabenki. Sasa basi unapotaka kuwashirikisha katika mipango ya serikali ni vema ukapata maoni yao halisi ili kuweza kuilinda mitaji yao ambayo wameitengeneza kwenye mazingira magumu sana. Serikali inapofikia hatua ya kusema itawaletea makampuni makubwa na wao wapeleke magari yao huko, hivi kweli hii nikauli sahihi?
  Kwani nini serikali isiratibu shughuli zao na kuwapa uwezo wa kulinda mitaji yao kwa kuwafanya wao ndiyo wawe wadau wakubwa wa hayo makampuni makubwa?
  Tuliangalie hili kwa makini sana kwani tusipoangalia sasa tutarudi hapa baadae kupiga kelele baada yakuona kila shida zetu sisi watanzania ni furaha na faraja za wageni na wenzetu wachache.

  Huyu ofisa wa serikali anapofananisha usafiri uliopo Japan na hali itakavyokuwa Dar es Salaam, tunaona ni sawa? Je, anaweza kutuambia miundo mbinu ya Japan ni sawasawa na ya Dar? au atuambie ni katika eneo gani ambalo sisi tunaweza kujivunia kuwa tupo sawasawa na Japan?

  Ni vema serikali iwe regulatory hasa na wala sio mfanyabiashara. Reglatory officer anapoongelea kufufua UDA ninabaki hoi kabisa!!!!
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Punda this time tutajitahidi usife na mzigo utafika tu.
   
 10. D

  Darwin JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapa umeongea la maana, ila kitu kimoja nikwamba Tanzania kinachotukwamisa ni uongozi mbaya na rushwa.

  Hao wenye mitaji yao walichotakiwa nikuingia ubia tu na na mashirika makubwa ambayo yana uhakika, kwahio nao watapata faida kwenye biashara zao.

  Hata ulaya mabasi ya Eurolines, matrein wanaingia ubia na kampuni nyingine ndogo au watu wenye mitaji midogo ili kufanikisha lengo lao, na watu wanaziona faida.

  Kenya airways wana ubia na mashirika mwengi tu tena yanayojulina kama KLM na faida zake wanaziona.

  Kitu chochote hata kama kina ukubwa gani, lakini kama hakina uongozi mzuri na kina rushwa basi ujue kwamba hakitadumu.
   
 11. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Darwin,
  Nakupongeza angalizo lako zuri.
  Nadhani umeelekea kule ambako nilianzisha hii thread kwa nia ya kuchokoza na kupata feed back. Niliwahi kusikia hapo nyuma (nakiri kuwa sina ushahidi) kwamba kuna wazito ndani na nje ya serikali kuwa wanaandaa mpango wa kuchukua biashara ya usafiri wa jijini. Dhamira yao kubwa ya hawa wazito ilijengwa na ukweli kuwa walalahoi wa mji wa Dar es Salaam huachana na vijisenti vya kila siku kwa kupanda mabasi hasa daladala. Mahesabu yao yalilenga number ya daladala zinazotoa huduma jijini Dar es Salaam na mapato yapatikanayo kwa kila gari linalotoa huduma. Ni wazi kuwa wakazi wa jiji la kwa uchache kabisa hutumia Shs. 60m/= (Shilingi milioni sitini) kila siku kwa ajili ya usafiri wa ndani. Hivyo basi bila ya kujali mambo mengine jitihada zimekuwa zikifanyika in the good name of kuwaondolea wananchi kero ya usafiri. that's fine mimi sina tatizo katika kwaondolea wannchi shida ya usafiri, lakini ikumbukwe kuwa ni wananchi hawa hawa kwa ujumla wao wamewekeza kiasi kikubwa katika usafiri wa ndani wa Jiji la Dar es Salaam. Kipaumbele cha uwekezaji mpya wenye jina la kuondoa kero za usafiri kwa wananchi hauna budi uendane na kuwapa nafasi wawekezaji wa kitanzania ambao tayari wameshawekeza waimarishe huduma hiyo ya usafiri.
  Haileti maana leo hii nguvu kazi ipo na mitaji ipo, tunawaza ni namna gani tutaleta wawekezaji wakubwa waje wachote 60m/= za walalahoi.
  Sababu nzuri isitumike kama kigezo cha kuwanyima nafasi watanzania walio wengi kushiriki katika shughuli za kibiashara.
   
Loading...