Baba J anaona ni sawa tu, Mwanza imechafuka yaani hapafai, lila kona miavuli na maturubai
Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani asubuhi tunaokwenda kazini kwenye Vituo vya Daladala Wanawasha Moto wa Kuni kupika Supu na Chai. Moshi unatanda kituoni Abiria tunanuka Moshi. Utakuta Machinga amesimamisha Mti katundika nyama anaikatakata. Watu wa Afya wako Wapi? Machinga ni Kero penye Mitaro ya Maji taka/mvua wameweka Mbao na juu duka. Kila Kona Siku hizi ni kutambua Tu wapi unataka weka Biashara unaweka bila kizuizi. Na Mwaka huu wa Uchaguzi watavamia kila mahali Kwa Raha zao.Kila mfanyabiashara ana haki ya kufanya biashara LAKINI kwa utaratibu uliopo sasa wa kuwaruhusu Machinga kuzagaa kila sehemu inaleta simanzi kubwa kwa wafanyabiashara wakubwa.
Mfano hai njoo hapa Mwanza mtaa wa Nyerere panatisha. Mbele ya maduka makubwa yamevamiwa na machinga na kuwanyima wafanyabiashara wanaolipa mapato makubwa, leseni na mapato mengine kupata wateja.
Wafanyabiashara hawa wakubwa hawana pa kusemea lakini wanaumia sana rohoni. Hivi kwa nini Machinga wamepewa uhuru wa kufanya watakalo? Hata sababu kubwa ya Wafanyabiashara wa Kilimanjaro kufunga biashara zao mojawapo ni Machinga.
Nashauri suala hili lifanyiwe utafiti na hata kuwa na kikao cha Wafanyabiashara na Serikali ione tatizo la machinga na kulipatia ufumbuzi.
Mkuu mwenyewe alipokua Mwz aliwaambia Wamachinga wakiona hata mbele ya ofisi ya mkuu wa mkoa panafaa kwa biashara zao waweke biashara zao hapo.Yaani asubuhi tunaokwenda kazini kwenye Vituo vya Daladala Wanawasha Moto wa Kuni kupika Supu na Chai. Moshi unatanda kituoni Abiria tunanuka Moshi. Utakuta Machinga amesimamisha Mti katundika nyama anaikatakata. Watu wa Afya wako Wapi? Machinga ni Kero penye Mitaro ya Maji taka/mvua wameweka Mbao na juu duka. Kila Kona Siku hizi ni kutambua Tu wapi unataka weka Biashara unaweka bila kizuizi. Na Mwaka huu wa Uchaguzi watavamia kila mahali Kwa Raha zao.
Hii sasa ndio serikali inayowajali wanyonge.Mkuu mwenyewe alipokua Mwz aliwaambia Wamachinga wakiona hata mbele ya ofisi ya mkuu wa mkoa panafaa kwa biashara zao waweke biashara zao hapo.
Hahah mkuu naona umepigilia msumari ki 'kweri kweri'.Hii sasa ndio serikali inayowajali wanyonge.
Maendeleo hayana chama
Hii ni awamu yetu wanyonge, ninampango wa kuongeza meza tatu za kuuzia mitumba kwenye ile barabara ya kuelekea ferry.Hahah mkuu naona umepigilia msumari ki 'kweri kweri'.
Hahah kupiga honi tu mitaa ile wanazingua siku wakiona meza zako ni balaa hahah,ila ukifanikisha nami ntaleta meza niuze miguu ya kuku,kachori mixer mahindi ya kuchoma.Hii ni awamu yetu wanyonge, ninampango wa kuongeza meza tatu za kuuzia mitumba kwenye ile barabara ya kuelekea ferry.
Maendeleo hayana chama
Muhimu uwe tu na kitambulisho cha ujasiriamali, sisi wanyonge tusipoitumia vizuri awamu hii nakuhakikishia tutajuta maisha yetu yote maana hakuna awamu nyingine tena itakayotujali na kututhamini sisi walala hoi.Hahah kupiga honi tu mitaa ile wanazingua siku wakiona meza zako ni balaa hahah,ila ukifanikisha nami ntaleta meza niuze miguu ya kuku,kachori mixer mahindi ya kuchoma.
Hatima ya hii ni Nini? Miji inachafuka kama Bombay India🙉🙉 Kama hawadhibitiki Siku moja tutalia. Kuna wengine wanafanya Biashara ya mnada Barabarani Siku ya Jumanne Boko Chama ni Kero Kwa Magari yote na wasafir wengine. Foleni mpaka Tegeta hakuna wa kuwaondoa.Mkuu mwenyewe alipokua Mwz aliwaambia Wamachinga wakiona hata mbele ya ofisi ya mkuu wa mkoa panafaa kwa biashara zao waweke biashara zao hapo.